Lugumgya
JF-Expert Member
- Dec 10, 2019
- 629
- 2,053
Salaam!
Mwaka fulani nikiwa, nimeenda kijijini kusalimia, nilipata nafasi ya kumtembelea jamaa yangu mmoja hivi (Ke),ambaye alikuwa akiishi Kijiji Cha jirani!
Nilivyofika tulipiga stori zetu huku tukisikiliza RTD kipindi Cha Harakati. Basi katika kipindi hicho wakasimulia stori ya kijana mmoja kumbaka msichana ambaye alikuwa akitoka kutafuta kuni mistuni. Hapo ndo jamaa yangu (Ke) akanipa kisa chake!
"Ndugu yangu vijana wa siku hizi sijui mmepatwa na nini? Haya matukio ya ubakaji yanashika Kasi Sana, tena hamuogopi hata watu wazima!
Akanambia, siku moja wakati anatoka kumsalimia ndugu yake Kijiji Cha jirani alikutana na vijana wawili mmoja ana Panga na mwingine ana Kisu. Wakamsimamisha, wakaanza kumvuta kuelekea ndani ya vichaka!
Yeye hakutaka kusumbuana nao, aliwaambia hivi "msihangaike kunivuta baba, tulieni nivue tugawane huu UKIMWI"
Anasema Vijana(mabaharia siku hizi), walikula mbio hatari, akawa amejinusuru bila kutumia nguvu.
Je, ushawahi kujisunuru na bila kutumia nguvu?
*_Tuendelee kuchukua tahadhari kudhibiti maambukizi ya Corona_*
Lugumya.
Sent using Jamii Forums mobile app