Msingi bora wa chama cha CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msingi bora wa chama cha CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SOKETI, Mar 6, 2012.

 1. SOKETI

  SOKETI Senior Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Chadema ni chama chenye itikadi, malengo na mwelekeo mwema katika kusimamia misingi bora ya utawala ikiwamo demokrasia, CDM imejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na viongozi shupavu na kutokea kupendwa na watu wengi wanaopenda maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania. Kuwapo na viongozi wanaojituma kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi waliowengi ni mojawapo ya nyenzo zinazokuza chama na kujenga uaminifu miongoni mwa raia. CDM INAITAJI KUJENGA MSINGI ULIO BORA. Kuwa na viongozi wachapakazi katika nafasi za kukiongoza chama, wabunge na madiwani bado haitoshi!. Katika baadhi ya majimbo chadema imekua ikipoteza viti vingi vikiwamo vya Ubunge pamoja na Udiwani kutokana na kukosekana kwa msingi imara. Namna ya kujenga msingi imara ni kuimarisha chama katika ngazi ya chini kwa kukiwezasha kuwa na wawakilishi ktk kila kata, kijiji/mtaa, na kila baada ya nyuma kumi. Kwa kufanya hivyo chama kitakuwa na uwezo mkubwa wa kumfikia kila mtanzania popote pale alipo. ANGALIZO:- Katika uchaguzi utakaofanyika huko Arumeru mashariki wa kuwania nafasi ya ubunge na chaguzi nyingine zinazotarajia kufanyika mwezi ujao, CDM inatakiwa kuwa na wawakilishi wa kila mtaa na ikiwezekana kila baada ya nyumba kumi ili kukiwezesha chama kumfikia kila mwananchi ikiwamo wale watakaoshindwa kuudhuria mikutano ya hadhara/wazi. Naomba kusilisha hoja. NAKALA KWA VIONGOZI WOTE WA CDM.
   
Loading...