Mkuu umeongelea jambo la muhimu mno katika mada yako. Ni kweli kabisa wakati wa awamu ya hayati JPM Wachaga walisimangwa sana kwa ajili tu ya kabila lao. Sasa linakuja hili la Wasukuma, sijui wenye ajenda hii wana nia gani!?
Umoja, mshikamano na utengamano wa kitaifa ni nguzo muhimu mno kwa ujenzi wa taifa letu. Mashabiki wa mambo ya ukabila ni watu hatari mno kwa mustakabali mwema wa taifa letu.