Msimamo wa wana CCM juu ya MCC ni dharau na udanganyifu kwa walipa kodi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,434
Kuna njia lukuki kujadili hili lakini tuliangalie zaidi katika muktadha wa contingent liabilities za serikali pamoja na deni la taifa.

Deni la Serikali kwa Makandarasi:

Wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu 2015, Mh Sumaye na viongozi wengine wa upinzani walieleza wananchi jinsi gani Wizara ya ujenzi chini ya utawala wa Rais Kikwete ilivyolimbikiza Deni la makandarasi, deni ambalo kufikia Mwisho wa mwaka 2015 lilifikia TZS Trilioni Moja, na hii ikiwa ni riba pekee! Je, tulifikaje hapo kama taifa wakati ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya fedha za ujenzi wa Miundo Mbinu hutolewa zaidi na wahisani kuliko fedha za ndani? Hiki ni kitendawili kinachohitaji majibu.

Deni la serikali kwa makandarasi leo hii linakaribia kiwango sawa na Fedha za MCC zilizozuiwa. Serikali ya Rais Magufuli ina haha kulipa deni hili kwa kutumia Kodi za wananchi bila ya maelezo wala ufafanuzi wowote kwa wenye fedha (wananchi). Kipaumbele chochote cha serikali makini kinatakiwa kuwa katika matumizi ya Fedha za walipa kodi kuboresha maisha yao kupitia huduma ‘bora’ za kijamii. Kipaumbele hakitakiwi kuwa katika kulipa madeni ambayo chanzo chake ni uzembe wa serikali yenyewe chini ya CCM.

Fedha za MCC zimekuwa zikijitahidi kuziba pengo hili na mapungufu haya ya serikali ya CCM kwa masharti ambayo katika kipindi chote yamekuwa wazi kabisa na yenye maslahi kwa wananchi walio wengi. Sehemu kubwa ya masharti haya yanahimiza juu ya umuhimu wa Serikali kufuata misingi ya:

1. Utawala bora.
2. Ulinzi na Usimamizi wa haki za Wananchi - kisiasa, kijamii na kiuchumi.”

Je, kuna ukoloni gani katika masharti haya?
Je, kuna lengo gani baya au hujuma katika haya dhidi ya wananchi walio wengi?

Hatua ya wana CCM kuwaeleza wananchi kwamba ‘hawahitaji fedha hizi” wakati ukweli ni kwamba fedha hizi ndio zilikuwa mkombozi wao kutokana na serikali ya CCM kushindwa kutumia ipasavyo kodi za wananchi kuwapatia huduma bora ni dharau kubwa kwa walipa kodi wa nchi yetu.

Deni la Serikali Kwa Mfuko wa Pensheni wa PSPF:

Ripoti ya hivi karibuni ya “National Debt Management Strategy” inaonyesha kwamba Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete ilikuwa haipeleki michango ya watumishi wake kwenye mfuko wa pensheni wa PSPF. Hili ni jambo la ajabu, aibu na la kukatisha tamaa.

Serikali imekuwa ikitegemea sana kodi kutoka kwenye mapato ya watumishi wake, kodi ambayo leo hii serikali ikiulizwa imeitumiaje kusaidia wananchi maskini, haiwezi kuja na majibu ya maana. Serikali imeshindwa kutumia kwa ufanisi kodi inayotoza watumishi wake kila mwezi, na mbaya zaidi, pamoja na watumishi wetu kuvuja jasho kulitumikia taifa lao, michango ya serikali kwa ajili ya maisha yao ya baadae imekuwa haipelekwi kwenye mfuko husika inavyopaswa.

Kwa mujibu wa ripoti husika, deni la serikali kwa mfuko wa PSPF ni zaidi ya TZS trilioni Mbili. Serikali ya Rais Magufuli imeanza kulipa deni hili lililolimbikizwa na Serikali ya Rais Kikwete. Walipa kodi wa nchi yetu – wakulima, mama ntilie, machinga, bodaboda, kwa vyovoyte vile hawahusiki na deni hili ambalo chanzo chake ni uzembe tu wa serikali.

Pamoja na kutohusika kwao na deni hili, serikali bado inatumia fedha za walipa kodi kila mwezi kulipa deni hili na kupelekea kiwango cha fedha kwa ajili ya maendeleo ya walipa kodi kuwa pungufu. Mapungufu haya yamekuwa yakizibwa na fedha za MCC. Hatua ya wana CCM kuambia wananchi kwamba hawahitaji fedha za MCC wakati ukweli ni kwamba zilikuwa zinasaidia wananchi katika machungu haya ni dharua kubwa kwa walipa kodi wa nchi yetu.

Deni la Taifa – Kipindi cha mwaka 1961 hadi mwaka 2008:

Kufikia mwaka 2008, baada ya miaka 47 ya “uhuru”, Deni la taifa katika kipindi chote hiki lilifikia jumla ya TZS Trilioni 15. Katika kipindi chote hiki cha miaka 47, wananchi maskini hasa wakulima ndio waliokuwa wakivuja jasho kulipa deni hili kupitia kodi na tozo mbalimbali chini ya serikali ya CCM. Lakini badala ya mikopo hii (deni la taifa) kuwa na matokeo chanya kwa maisha ya wananchi walio wengi (maisha bora), katika kipindi hiki, maisha ya wananchi walio wengi yalizidi kuzorota. Wananchi wana haki ya kuiuliza Serikali: Je, mikopo yote tangia uhuru hadi leo imeleta faida gani kwa wananchi walio wengi? Je, fedha zilizotokana na kodi na tozo mbalimbali kwa wananchi katika kipindi hiki zimeletea wananchi walio wengi faida gani?

Katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa Rais Magufuli, wananchi walio wengi wataendelea kuteseka na umaskini. Hii ni kwa sababu, pamoja na mengineyo, sehemu kubwa ya kodi zao zitaendelea kwenda kulipa madeni ya serikali nje ya nchi badala ya kubakia nchini kuletea wananchi maendeleo.

Deni la Taifa Baada ya Mwaka 2008, Kipindi ambacho Edward Lowassa aliondoka Madarakani:

Moja ya maajabu makubwa ya serikali ya Kikwete 2005-2015 ni kwamba katika miaka mitano tu (2008-2013), serikali ilikopa Fedha nyingi kuliko jumla ya deni lote la taifa kwa miaka yote 47 ya uhuru. Katika kipindi hiki cha miaka mitano tu (2008-2013), serikali ya Rais kikwete ilikopa zaidi ya TZS trilioni 20. Leo hii deni la taifa limefikia TZS Trilioni 43, karibia mara tatu ndani ya miaka nane tu. Kwa kipindi cha mwaka mmoja tu (2014-2015), serikali ya Rais Kikwete ilikopa zaidi ya TZS trilioni Mbili.

Kila Mwezi fedha za walipa kodi zinaenda kulipa deni la taifa, deni ambalo halijawa na faida yoyote ya maana kwa wananchi walio wengi kwa miaka ya 55 ya ‘uhuru wao’. Wakulima, wafugaji, Mama ntilie, bodaboda, machinga, wote hawa wanahenyeka kupitia tozo na kodi mbalimbali kulipa deni la taifa, deni ambalo halija wahudumia kwa kujenga ‘productive capacity’ ya nchi iliyotengeneza ajira, kuwapatia wananchi hasa vijana vipato, na hivyo kuwapunguzia umaskini.

Kwa mfano chini, ya serikali ya Rais Magufuli, kwa mwezi February 2015, Serikali ilitumia zaidi ya nusu ya mapato ya kodi ya mwezi kulipa deni la taifa (mikopo) ambayo kwa miaka 55 ya uhuru mikopo hii haijawa na manufaa yoyote ya maana kwa wananchi walio wengi; Sehemu nyingine ya fedha hizi zimekuwa zikienda kulipa madeni ya serikali kwa makandarasi na kwa mifuko ya pensheni kama PSPF, madeni ambayo yametokana na uzembe wa serikali ya CCM. Mzigo huu wamekuwa wakitishwa wananchi maskini badala ya fedha hizi kwenda kuboresha huduma za kijamii kwa kupitia kodi zao.

Kiasi kingine cha mapato ya kodi kwa mwezi, sio chini ya 30% unakuta kinaenda kulipa mishahara na posho za watumishi wa serikali, na kiasi kidogo sana kilichobakia ndio kinapelekwa kwenye miradi ya maendeleo.

Katika mazingira haya, tunapohimiza wananchi kuongeza bidii ya kazi, kuwahimiza walipe kodi, tusipofanikiwa kutimiza malengo ya ukusanyaji kodi, je nani atakuwa ni wa kulaumiwa?

Tutakuwa ni taifa la watu wa ajabu sana kama tutaendelea kutembea vifua mbele kujiamini kwamba muda sio mrefu tutajitegemea kibajeti wakati ukweli uliopo ni kwamba "ukubwa" wa mapato ya kipindi hiki yanatokana zaidi na "past arrears".

Tunakuwa taifa la ajabu sana kama tunaamini kwamba tutaanza kujitegemea kibajeti wakati kwa kipindi kirefu kijacho, sehemu kubwa ya mapato yetu ya kodi yataendelea kuwa ni “consumption taxes” na sio “production taxes”. Serikali ipo busy 'destroying wealth' instead of 'creating wealth'. Bila ya uangalifu, miezi sita ijayo mapato ya Kodi kwa mwezi yatashuka na kurudi katika kiwango alichoacha Rais Kikwete (TZS 900 Billion), na kiwango hiki kinaweza kushuka zaidi huko mbeleni. Inawezekana kuna mipango mizuri lakini mipango husika inatekelezwa kwa kukurupuka, kwa hisia, kuapiza visasi na kwa kutafuta popular support. Muda sio mrefu, Populist politics zitaanza kutugharimu kama taifa.

Kiburi cha Wana CCM kwamba TZS trilioni moja za MCC sio lolote wakati asilimia 90% ya kodi za maskini zinaenda kulipa madeni, posho na mishahara ya watumishi wa serikali huku vijisenti tu vikienda kwenye miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa inasaidiwa na MCC, ni ujuha uliopitiliza.

CCM ina haja ya kutambua kwamba kiuchumi katika hali ya sasa, mbele kuna kiza kuliko mwanga. Ubabe na kiburi sio njia sahihi ya kukabiliana na hatari hiyo kama taifa.
 
Kukaa hapa na kuanza kujadili faida au hasara ya kutopata misaada wa Tsh 1trl ni kupoteza muda!

Haisaidii lolote kusema kuna faida au hakuna faida kwenye pesa ambayo haipo na haitakuwepo.

Wamarekani wameishaamua kutotoa pesa yao. Finito.

Ni sawasawa na binadamu unatupwa kwenye mbuga hatarishi halafu unaanza kupoteza muda ufikiria na kujadili kwa nini umetupwa na ungepata faida gani kama asingekutupa badala ya kuanza kufikiria njia ya kujinasua haraka katika janga hilo.

Waingereza hupenda kusema, time is money lakini kama utautumia wisely and effectively!

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ‘’We must run while they walk’’ akiwa na maana tusijikite au kubweteka kwenye fikra za zamani wakati wenzetu wanajikita kwenye fikra zijazo au kwa maana nyingine lazima tuwe proactive badala ya kuwa reactive.

Please, pick yourself up, dust yourself off, and start all over again!

Wamarekani wameisha move on!

This is a wake-up call!

By the way, suala la deni la taifa linaingiaje kwenye misaada wa MCC wakati pesa zake zinakuwa chini ya uangalizi wa MCC Resident Country Director?
 
Kukaa hapa na kuanza kujadili faida au hasara ya kutopata misaada wa Tsh 1trl ni kupoteza muda!

Haisaidii lolote kusema kuna faida au hakuna faida kwenye pesa ambayo haipo na haitakuwepo.

Wamarekani wameishaamua kutotoa pesa yao. Finito.

Ni sawasawa na binadamu unatupwa kwenye mbuga hatarishi halafu unaanza kupoteza muda ufikiria na kujadili kwa nini umetupwa na ungepata faida gani kama asingekutupa badala ya kuanza kufikiria njia ya kujinasua katika janga hilo.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ‘’We must run while they walk’’ akiwa na maana tusijikite au kubweteka kwenye fikra za zamani wakati wenzetu wanajikita kwenye fikra zijazo.

Please, pick yourself up, dust yourself off, and start all over again!

Wamarekani wameisha move on!

Tunachofanya ni kujibu hoja ya wana ccm kwamba hatua ya MCC sio lolote, sio chochote. Tukishamaliza kueleza kwa hoja jinsi gani huu ni upotoshaji, ulaghai na dharau ya CCM kwa walipa kodi, we will move on to many other issues zinazohusiana na mustakabali wetu kama taifa.
 
Tunachofanya ni kujibu hoja ya wana ccm kwamba hatua ya MCC sio lolote, sio chochote. Tukishamaliza kueleza kwa hoja jinsi gani huu ni upotoshaji, ulaghai huu na dharau ya CCM kwa walipa kodi, we will move on to many other issues zinazohusiana na mustakabali wetu kama taifa.
Mbona hakuna kilichojibiwa?
 
Mjomba lipa kodi fanya kazi....unapunguzaje gape kwa msaada wenye mashart???

Funga mkanda acha kutegemea nguo ya kuazima kwani haistiri makalio

Kwanini kuna gap in the first place?

Masharti ya MCC ambayo yalikuwa wazi kabisa kwa serikali ya CCM katika kipindi chote yalikuwa na athari gani mbaya kwa wananchi walio wengi?
 
Tunachofanya ni kujibu hoja ya wana ccm kwamba hatua ya MCC sio lolote, sio chochote. Tukishamaliza kueleza kwa hoja jinsi gani huu ni upotoshaji, ulaghai na dharau ya CCM kwa walipa kodi, we will move on to many other issues zinazohusiana na mustakabali wetu kama taifa.
Hata ukipangua hoja za CCM sasa hivi inasaidia nini? Au kama unataka kuandika thesis!
 
Bado mnataka tujadili pesa za kupewa!!
Nyie watu mpoje
Pesa hujaifanyi kazi inakuuma kama ya BABAKO!!!
Kwanini tumekuwa tunapewa kwa miaka 56 ya utawala wa CCM?

Kama ni kweli, kwanini Rais Magufuli na Waziri wa Fedha Mpango wanahimiza juu ya umuhimu wa 'pesa ya kupewa" kwa ajili ya miradi ya maendeleo hasa miundo mbinu?

Katika hotuba yake juu ya mpango wa maendeleo na maandalizi ya bajeti bungeni, Waziri Mpango alijadili juu ya umuhimu wa Shillingi trilioni kadhaa ambazo serikali itatarajia "kupewa" na wahisani, kulikoni?
 
Kwanini tumekuwa tunapewa kwa miaka 56 ya utawala wa CCM?

Kama ni kweli, kwanini Rais Magufuli na Waziri wa Fedha Mpango wanahimiza juu ya umuhimu wa 'pesa ya kupewa" kwa ajili ya miradi ya maendeleo hasa miundo mbinu?

Katika hotuba yake juu ya mpango wa maendeleo na maandalizi ya bajeti bungeni, Waziri Mpango alijadili juu ya umuhimu wa Shillingi trilioni kadhaa ambazo serikali itatarajia "kupewa" na wahisani, kulikoni?
Haya ndio wamekataa sasa
Kwahio unataka tufanyeje pesa za misaada sio lazima !?

Sioni umuhimu Ku endelea kujadili pesa za wenyewe ikiwa tuna matatizo mengi yakujadili
 
Kukaa hapa na kuanza kujadili faida au hasara ya kutopata misaada wa Tsh 1trl ni kupoteza muda!

Haisaidii lolote kusema kuna faida au hakuna faida kwenye pesa ambayo haipo na haitakuwepo.

Wamarekani wameishaamua kutotoa pesa yao. Finito.

Ni sawasawa na binadamu unatupwa kwenye mbuga hatarishi halafu unaanza kupoteza muda ufikiria na kujadili kwa nini umetupwa na ungepata faida gani kama asingekutupa badala ya kuanza kufikiria njia ya kujinasua katika janga hilo.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ‘’We must run while they walk’’ akiwa na maana tusijikite au kubweteka kwenye fikra za zamani wakati wenzetu wanajikita kwenye fikra zijazo.

Please, pick yourself up, dust yourself off, and start all over again!

Wamarekani wameisha move on!
"CCM ni ile ile" je hii sio fikra ya kizamani?
 
Tunachofanya ni kujibu hoja ya wana ccm kwamba hatua ya MCC sio lolote, sio chochote. Tukishamaliza kueleza kwa hoja jinsi gani huu ni upotoshaji, ulaghai na dharau ya CCM kwa walipa kodi, we will move on to many other issues zinazohusiana na mustakabali wetu kama taifa.


Eti deni baada ya Lowasa kuondoka madarakani!!!!
 
How comes mtu na akili zako timamu unaandika mada ya kulilia misaada? Nilitegemea watu mje na mada za kuibana serikali ipunguze matumizi ya hovyo na iboreshe vyanzo vya mapato ikiwemo kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija ili kutengeza taifa la kujitegemea halafu eti unaleta mambo eti wanaccm? Lini utakuwa mzalendo na nchi yako? Hivi mkeo akinuka kikojoleo huwa unakwenda kwa jirani kushadadia kuwa mkeo ananuka au huwa unakuwa mzalendo na ndoa yako na kisha kuutibu uvundo kimya kimya?
 
Waandishi makanjanja wa kibongo hawana muda wa kufanya uchambuzi kama huu kazi yao ni kuandika habari tu za kuipamba hii serikali.

Waandishi wengi wa nchi hii ni hopeless kabisa na hawasaidi jamii kujua aina ya viongozi walionao zaidi tu ya kuwapotosha kwa habari za kusifu hii serikali utazani wameajiriwa na kitengo cha propaganda cha CCM!

Waandisho fanyeni kazi yenu kwa namna ambayo itamuacha mwananchi(mlaji wa habari) kuamua mwenyewe ni aina gani ya viongzi au serikali aliyonayo.Kuweni "objective" kwenye kazi yenu.

Nazipongeza media chache zilizobaki kusimamia madili na miko ya taaluma hii kwa faida ya Taifa hili na watu wake likiwemo gazeti la Dira.
 
T
Haya ndio wamekataa sasa
Kwahio unataka tufanyeje pesa za misaada sio lazima !?

Sioni umuhimu Ku endelea kujadili pesa za wenyewe ikiwa tuna matatizo mengi yakujadili

Unfortunately, tutaendelea kujadili pesa za wenyewe kwa miaka zaidi ya 30 ijayo kwani tuna deni la nje ambalo sasa ni zaidi ya TZS Trilioni 29. Kwa miaka kumi ijayo, kati ya 10-15% ya mapato ya serikali yatakayotokana na kodi za wananchi yataenda kwa "wenyewe" huko nje.

Rais Magufuli atatumia muda wake na fedha nyingi zaidi za walipa kodi kuwalipa "wenyewe" huko nje kuliko kuwekeza katika miradi ya maendeleo kwa ajili ya walipa kodi.

Miaka kati ya mitano na nane kutoka sasa, kuna dalili kwamba tutaingia katika debt crisis kutokana na fedha za wenyewe. Kwahiyo tuombe uzima na tuwe tayari kujadili kwa kina na kwa mapana zaidi kuliko sasa kuhusu fedha za 'wenyewe' huko mbeleni. Lakini ukipenda, unaweza kushiriki mjadala huu mapema zaidi ili usije kuwa mtu wa kushtukizwa na mgogoro mkubwa huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom