Nadhan wanaunga mkono kuondoka na au kubaki kwa ASSAD!!
Hili swali MEMBE ANGEJIBU HIVI: NI KUONDOKA.........then kwenye ufafanuzi akibwana atasema alikuwa akimaanisha KUONDOKA KWA WAASI then akiwa na mabalozi atasema ni KUONDOKA kwa ASSAD kama nilivyosema mwanzoni
Take:TUMWACHE ASSAD AWAMALIZE HAWA RAIA MANAKE US+NATO wakiingia waislam wanaongea sana sasa ASSAD GO ON WAMALIZE WAARABU
Anaua watu analinda nchi hahahahaaaa!!!!!!!
Tanzania ya nyerere sio Tanzania ya sasa. kwanza kabisa nyerere alishatengeneza jina kwa sababu kwanza kipindi kile kulikuwa na harakati za ukombozi wa bara la africa, na nyerere ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanaogopwa sana, yeye aliweka makambi mengi hapa tz ya wasouz wakiwa trained kwenda kupigana, na askari wetu wameenda sana kupigana vita angola, namibia, mozambique na zimbabwe sana.Nimetaka kujua tu ili niweke kwenye record ili tusijekuhitilafiana uko mbele, sababu kama hizo hoja zako ndio za muhimu sana ili Taifa liweze kusikilizwa, ninalazimika kureview records kuona kama Tanzania ya Nyerere ilikuwa inasikilizwa au nini kile kilikuwa kinaendelea.
Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.
Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?
Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?
NAdhani hujui unalolisema,.
Kwanza naomba nikujulishe kuwa zile zote ni hila za kimagharibi KUTAKA KUINGIA IRAAN kwa urahisi, wameshakali Quwait na Saudi Arabia na Afghanistan ili iingie kirahisi Iraq, sas hivi INAHAHA KUINGIA IRAAN, na inaona kikwazo kikubwa kipo USSR Urusi , haiwezi kuipiga Syria kwa sababu ya Urusi na msimamo wake juu ya Syria na Iraan, na once ikishaingia Syria basi ni wazi wataingia Iraan kirahisi na hatima middle east yote itakuwa imekaliwa na wamagharibi.
Kinachonishangaza kwanini mnashabikia mambo ya kimagharibi sana na badala ya kuwaonea imani waarabu na mafuta yao? kuna siku PAsco alimshambuli sana mwanakijiji na misimamo yake na wagharibi leo ndio nimeamini, nahisi mwanakijiji anawapenda wamagharibi kwa ajili ya Udini! nilikuwa nikimheshimu sana lakini sasa naanza kuondoa imani na heshima yangu juu ya huyu mtu ! kweli ANANISHANGAZA !
Unachekesha sana sana! ASSAD anua watu wake au ANALINDA NCHI yake dhidi ya mabeberu ya magharibi? hebu nenda deep katika hili, tumeona mengi yamefanywa na hawa wamagharibi wao wakiua wanalinda raia, rais akilinda nchi yake dhidi ya puppets wa magharibi anaua! unacheksha sana tena sana! itakuwa labda nimekosea kusema udini lakini juzi juzi nimeona Pasco akilumbana na mwanakijiji juu ya swala la yeye kuwa mrengo wa magharibi na amediriki kumuita puppet wa magharibi sasa NAAMINI !
my friend,nyerere angekuwepo ningekuambia uende ukamwulize kama alifanikiwa kwa lolote katika misimamo yako ya aina hii. ukiwa huna kitu rafiki yangu huna lolote. hata ukikataa kuwasikiliza wamagaribi utajikuta uumefika maji shingoni na kusalenda tu. nasema tuitoe ccm kwasababu nategemea pengine tukiwa na utawala mpya tutakuwa na sera na vision mpya na kujikwamua kwenye umasikini pengine kanchi ketu kakiwa kanagusa maslahi ya wakubwa kwa namna fulani hasa ya kiuchumi, basi hapo tutaanza kuwa na sauti, ila kwa sasa, matatizo yetu sisi wenyewe tu yametushinda, ya syria tutayaweza? hata ukisema nani atakusikiliza?Hauoni kwamba msimamo wako unamaanisha kwamba tuzipigie magoti nchi zilizoendelea, sababu kama hatuwezi kuchukua hatua yoyote, na sasa unadai hatuwezi hata kusema, Sababu sisi sio wafu ni lazima kuna kitu tunafanya, kama maelezo yako ni fact basi hicho kitu ni kufuata maelekezo ya nchi Tajiri, na kama hali ndio hii ni nini kinakufanya ufikirie tukiiondoa ccm madarakani ndio tutajitoa kwenye hali ya kishenzi namna hii? Naomba nitofautiane na wewe rasmi kwamba, ni lazima tujiheshimu na tujitambue na kujitambulisha msimamo wetu sasa, no matter how poor we are.
Kimsingi mambo yanayoendelea Syria sio mepesi kama tunavyofikiria. Wamagharibi wanafahamu hilo nasi twapaswa kufahamu pia. Nifafanue kidogo.
Arab spring ilpoanza pale Tunisia, ikasambaa kwa majirani Misri na Libya, ikapaa Yemen, huko ilifanikiwa maana tumeshuhudia huko kote umma ukiinuka dhidi ya madikteta wa muda mrefu wa nchi hizo na kufanikiwa, kwa msaada wa Marekani na Ulaya au la, kuwaondoa madarakani madikteta, kuwaua, kuwafunga maisha au kuwafukuzia mbali.
Lakini siyo pote ilipotokea Arab Spring, umma wa Waarab ulifanikiwa. Bahrain ilishindikana na Jordan ilizimwa. Kwa nini? Kwa nini madikteta wa Bahrain na Jordan walishindwa kungoka? Kama ni mfatiliaji wa siasa za Mashariki ya Kati utajua kwamba wafalme wa Bahrain wana urafiki wa ajabu na waMarekani maana America imeweka base zake pale na wapinzani wa wafalme wale walikuwa ni Waislam wa Kishia wenye uhusiano wa karibu na Iran - adui wa Marekani, hivyo waandamanaji hawakupata moral support kutoka Marekani. Jordan ina makubaliano ya amani na Israel na waandamanaji wa Jordan baadhi ya misingi yao kutaka kuwaondoa watawala wa Jordan ni kuvuruga ile amani ili kurudisha ule uaadui wa enzi baina ya Israel na Waarab. Wamagharibi wanayasoma yote hayo na hawapo tayari kussuport umma kijinga kijinga. Wanafatilia pia hata malengo ya umma husika.
Pale Syria, kundi la watawala ni Waislam wa madhehebu ya ki-Alawite (jamii ya Kishia) na wana uhusiano wa karibu na washia wa Iran. Wasunni walio wengi ndio wanaandamana kutaka Assad na kundi lake la Walawite waondoke madarakani. Kwa hiyo kuna element fulani msuguano fulani hivi wa vita ya kidhehebu (sectarian violence) baina ya Washia na Wasunni pale Syria.
Serikali yoyote makini haipaswi kuwa na upande kwenye misuguano ya kidhehebu, vita ya kijinga kama ile. Sisi watanzania tunapenda demokrasia, lakini hatupaswi kussupport wahuni wanaotumia dini kama kigezo cha kutaka kutawala. Hata Misri Hosni Mubarak msecular ameondolewa na nguvu ya umma eti kwa sababu amekaa pale madarakani muda mrefu, but gues what, badala ya demokrasia itawale baada ya dictatorship ya muda mrefu, Muslim Brotherhood ndio wamekuja kushika bunge na sasa wananyemelea urais. Na itikadi ya Muslim Brotherhood ni itikadi ya udikteta wa Kiislam (sharia kwa sana), kumwondoa Hosni Mubarak na kuweka Muslim Brotherhood ni sawa na kuruka mkojo ukakanyaga ma**.
Misuguano ya kiarab si mambo yetu, sisi twaweza mambo yetu ya Kiafrica. Waarab wanaishi kwenye ulimwengu mwingine anawaweza Marekani tu napo kwa taabu.
Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.
Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?
Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?
Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.
Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?
Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?
Tanzania ni nchi masikini sana hawana upande kwenye mgogoro wa Syria mataifa makubwa ndio yana maslahi na mgongoro huyo ndio maana tumeona msimamo ya Urusi, China, wanatetea utawala wa Syria kwa maslahi yao na Marekani, Uingereza, Ufaransa, wanataka kuangusha utawala wa Syria kwa maslahi yao hapa Tanzania atasema nini zaidi ya kukaa kimya na kulaani mauaji tu.