Msimamo wa Tanzania kuhusu Syria ni upi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa Tanzania kuhusu Syria ni upi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 14, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tunakumbuka jinsi serikali yetu ilivyojitahidi kutoa msimamo wake kuhusu Libya wakati wa mwamko wa mapinduzi; tulijua kuwa serikali yetu inamuunga mkono Gaddafi na kwa kweli haikupendezwa na kuangushwa kwake.

  Lakini kwenye hili la Syria serikali yetu msimamo wake uko wapi? Inaonesha kujali mauaji yanayoendelea huko na kuonesha concern ya aina yoyote? au kuonesha concern kwaweza kuonekana ni kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi?

  Je hatuwezi kupima kwa misimamo yetu wenyewe na kujua pa kusimamia?
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nadhan wanaunga mkono kuondoka na au kubaki kwa ASSAD!!

  Hili swali MEMBE ANGEJIBU HIVI: NI KUONDOKA.........then kwenye ufafanuzi akibwana atasema alikuwa akimaanisha KUONDOKA KWA WAASI then akiwa na mabalozi atasema ni KUONDOKA kwa ASSAD kama nilivyosema mwanzoni

  Take:TUMWACHE ASSAD AWAMALIZE HAWA RAIA MANAKE US+NATO wakiingia waislam wanaongea sana sasa ASSAD GO ON WAMALIZE WAARABU
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mkuu MM,ni kweli serekali ya syria kwa kweli inastahili kuingiliwa kati na jeshi la umoja wa mataifa kwani haki za binadamu zinakiukwa kwa kasi mno,Tanzani a siku ni vifuata upepo katika INTERNATIONAL SITUATION,tayari marekani na nchi za magharibi zimeshatoa matamko juu syria mara kadhaa lakini serekali inaendelea kugandamiza democrasia na kibaya mauaji yanayotokea huko yanazidi mauji ya kimbaleyi huko rwanda,kwa nchi kama Tanzania kutoa tamko au kutotoa tamko hakutasaidia kitu kwani siku zote huwa tunaangalia wafadhili na wahisani wa bajeti yetu wanasemaje ndipo nasi tutoe matamko juu ya jambo fulani kama tulivyofanya kkt swala la libya,kwa hiyo mzee mm elewa siku zote Tanzania haina influence yoyote ktk politics za hali ya kimataifa zaidi kugawa rasilimali zake kwa kunyonywa,hivyo basi hata kauli mbalimbali zinazohusu international sitution Nchi maskini hutoa kauli baada ya kuona na kusikia nchi tajiri za magharibi zinasemaje juu ya jambo ilo,so tusubiri membe asome upepo ndio aje na yeye ambwambwaje.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Serikali yetu hasa hii iliyopo madarakani ilimuunga Mkono Gaddafi kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa ndugu zetu waislamu.
  Gaddafi alijenga misikiti mingi na madrasa Tanganyika na Zanzibar.

  Lakini huyu Bashar sidhani kama wanamuunga mkono.

  Lakini pia tukumbuke Tanzania ni nchi isiyofungamana na upande wowote
   
 5. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sheke Ponda, Bassaleh, BAKWATA, na wasemaji wengine wa dini nao wangeulizwa msimamo wao juu ya Syria. Mara ngapi tumesikia wakijiapiza na kulaani mtoto mmoja anapoangukiwa na bomu la NATO huko Afghanstan, kelele zinapigwa kuwa waislamu wanauawa? Lakini leo muuaji ni Muislamu mwenzao wote wanajifanya wako bize na sensa as if wana mipango fulani ya maendeleo ambayo itakwama wasipojua Wakristo wako wangapi
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mauaji ya raia syria hayakubaliki kwa sababu iwayo yote. Mimi nadhani wanatakiwa kumkana Rais wa Syria. Wakifanya vinginevyo nitashangaa sana.
   
 7. d

  dav22 JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  syria kizungumkuti aisee...
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kikwete na Membe hawana ubavu huo!
   
 9. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  NAdhani hujui unalolisema,.

  Kwanza naomba nikujulishe kuwa zile zote ni hila za kimagharibi KUTAKA KUINGIA IRAAN kwa urahisi, wameshakali Quwait na Saudi Arabia na Afghanistan ili iingie kirahisi Iraq, sas hivi INAHAHA KUINGIA IRAAN, na inaona kikwazo kikubwa kipo USSR Urusi , haiwezi kuipiga Syria kwa sababu ya Urusi na msimamo wake juu ya Syria na Iraan, na once ikishaingia Syria basi ni wazi wataingia Iraan kirahisi na hatima middle east yote itakuwa imekaliwa na wamagharibi.

  Kinachonishangaza kwanini mnashabikia mambo ya kimagharibi sana na badala ya kuwaonea imani waarabu na mafuta yao? kuna siku PAsco alimshambuli sana mwanakijiji na misimamo yake na wagharibi leo ndio nimeamini, nahisi mwanakijiji anawapenda wamagharibi kwa ajili ya Udini! nilikuwa nikimheshimu sana lakini sasa naanza kuondoa imani na heshima yangu juu ya huyu mtu ! kweli ANANISHANGAZA !
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Tanzania bendera fata upepo huwa haina msimamo inausimamia kwa dhati! linapokuja swala la kimataifa!! masuala mengi tu inashindwa kutoa msimamo angalia swala la Sudan kwamba Bashir anatakiwa na ICC? Mgogoro wa congo DRC?? mgogoro wa Ivory coast?? hata kote huko Libya, Misri Tunisia na sasa Syria hatuna msimamo wa kitaifa!Woga walio nao viongozi wetu ku make decision kwa mambo ya ndani hauishii hapa unaenda hadi kwenye nyanja ya kimataifa!!!
   
 11. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  hivi wewe kinyangarikakimkutikutitifuliwatifulwankwebezi tanzania, utasema nini kama msimamo wako watu na manchi yao makubwa, wakakusikiliza? hivi wewe hapo ulipo ukikutana njiani na mtoto wa miaka mitatu akasema anataka kutoa msimamo juu ya mambo yako utamsikiliza au utacheka tu na kumwacha kama alivy?...sisi tz tuna nini ambacho tumekifanya tukastahili kuheshimiwa kimataifa hata watu wa nchi nyingine watusikilize, what do we have on our hands, hatuna lolote zaidi ya kila siku credibility inapungua kwa rushwa, umbumbumbu, kutopiga maendeleo, kutokuwa na vision yeyote ya future, kuishi kwaajili ya leo, kukubali kuibiwa mali, kukalia maliasili bila kuwa na akili ya kuzitumia kwaajili ya maendeleo hadi nchi kama rwanda wanatudharau kuwa wao wangekuwa tz wangekuwa na maendeleo kama ya ulaya....tuna nini sisi ambacho tutasimamia ili watu wasikie sauti yetu hiyo au watuheshimu?...hapa cha maana tupiganie tu kupata maendeleo ili tuheshimiwe au tujenge heshima kwanza na baada ya hapo ndo tutapata ujasiri wa kuongea. hivi lofa akiwa kwenye kikao cha arusi au kikao chochote kile akiongea si watu wanamzomea? yaani mtu ukiwa mjinga, masikini, mbumbumbu hata kama ungekuwa na point ya kuongea mbele ya watu wenye hela zao watakuzomea na utaondoka point yako haijaandikwa kwenye karatasi, unachotakiwa ni kujenga jina kwanza kwa kufanya kitu kitakachowafanya wakusikilize, wakiona wewe unaendelea tu kuwa lofa mbumbumbu huna lolote, hata mtoto mdogo kama Rwanda anaweza kukudharau....
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Naomba unifumbue macho, post ya mwanakijiji inamaudhui gani ya udini? Alafu kwa nini unapeperusha mada? Post ya mwanakijiji inahoji juu ya msimamo wa serikali yetu juu ya mauaji anayoyafanya ASSAD dhidi ya wananchi wake, umagharibi unaingiaje hapa? Nitakuwa nimekosea nini kusema kwamba wewe ndio unahulka mbaya ya udini?
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Naomba nikuuliza swali, wewe ni materialist?
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa hali halisi iliyopo nchini kwetu hivi sasa ni sahihi kufirikia kwamba msimamo wa serikali yetu ndio msimamo wa watanzania?
   
 15. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Unachekesha sana sana! ASSAD anua watu wake au ANALINDA NCHI yake dhidi ya mabeberu ya magharibi? hebu nenda deep katika hili, tumeona mengi yamefanywa na hawa wamagharibi wao wakiua wanalinda raia, rais akilinda nchi yake dhidi ya puppets wa magharibi anaua! unacheksha sana tena sana! itakuwa labda nimekosea kusema udini lakini juzi juzi nimeona Pasco akilumbana na mwanakijiji juu ya swala la yeye kuwa mrengo wa magharibi na amediriki kumuita puppet wa magharibi sasa NAAMINI !
   
 16. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Wewe unataka Tanzania ijiingize ili nasisi tupigwe sio? umeona Kenya ilivo sasa hivi kwahiyo nasisi tuunge mkono ili iweje? NINI TUNAPATA KUTOKA HUKO?
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Acha ubishi, Mashambulizi ya Pasco dhidi ya mwanakijiji sio maandiko toka mbinguni, yanaweza kuwa na makosa kama vile wewe ulivyofanya kosa hapa kwa kuconfirm udini wa mwanakijiji kutokana na post ambayo haina hata vumbi la ishara ya udini.

  Kwamba Rais analinda Taifa lake kwa kuua Raia wake, any way, inawezekana, sababu hata hapa kwetu wanyama wa ngorongoro wanathaminiwa kuliko wananchi wa maeneo hayo.
   
 18. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  ni vibaya kuwa materialist? hicho nilichoongea ndio uhalisia wa maisha, yawe ni ya individual persons au individual state,...ndio maana unaona jinsi mataifa tajiri yanavyoongea na kusikilizwa?
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Nimetaka kujua tu ili niweke kwenye record ili tusijekuhitilafiana uko mbele, sababu kama hizo hoja zako ndio za muhimu sana ili Taifa liweze kusikilizwa, ninalazimika kureview records kuona kama Tanzania ya Nyerere ilikuwa inasikilizwa au nini kile kilikuwa kinaendelea.
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Anaua watu analinda nchi hahahahaaaa!!!!!!!
   
Loading...