Msimamo wa Eric Shigongo kwa maazimio ya bunge la Umoja wa Ulaya(EU)

Shigongo alipoenda Lumumba kudai pesa zake za kuchapisha T-shirts&Kofia za CCM kipindi cha uchaguzi 2015 hilo ndilo jibu alilopewa:

Mwanangu Erick kunywa maji haya upunguze machungu-By Zakia Meghi.
Hahahaaaaah! Nimecheka mpaka Nina kiu ya kunywa maji!!!
 
Shigongo alipoenda Lumumba kudai pesa zake za kuchapisha T-shirts&Kofia za CCM kipindi cha uchaguzi 2015 hilo ndilo jibu alilopewa:

Mwanangu Erick kunywa maji haya upunguze machungu-By Zakia Meghi.
Hahaha safari hii aambiwe akabangue korosho maana hakuna namna.
 
KWANI HUU WARAKA UNAHUSIANA VIPI NA ccm .... HAPA TUNAONGELEA NCHI BROTHER
Huwezi ukazungumzia mambo kama hayo huku ukijikomba kutafuta cheo!! Kwani hayo mambo yaliyotajwa na hao wazungu, sisi humu ndani tulikuwa hatuyaoni? Hadi leo mtu aje aseme kuwa hayo ni mambo yetu ambayo tunaweza kukaa na kuyazungumza?!! Nani mwenye uthubutu wa kutoka mbele na kuyasema, tofauti na hao wachache tena wapinzani, ambao mwisho wa siku yanawakuta!! Hizo ni njaa tu!!!
 
Ana haki na maoni yake.

Katika maoni yake ameshauri tutumie akili.

Ni akili sasa kupingana na mhisani huku unayemtegemea haoni shida kuchukua bandari yako akajinufaisha yeye?

Kitabu cha Walter Rodney kimezungumza mambo ya kawaida tu ukitaka kujua tunadeal vipi na hawa watu mtafute Issa Shivji atakwambia.

Nigeria kabla ya Boko Haram ilikua ndiyo nchi inayokimbilia kwenye kuendelea lakini haijawahi kusema eti tujifungie na rasilimali zetu. HAIJAWAHI TOKEA.

Aliyejifungia na rasilimali zake ni Zimbabwe kilichompata tuliona na China ilikuepo. Kitu gani spesho zaidi kwa China hapa Tz? Bandari? Madini? Haya wanunuzi wakiambiwa ukifanya deals na Tz tunakuwekea vikwazo unadhani watanunua?
China mwenyewe anahitaji malighafi hadi za miguu ya kuku toka USA wakipimana ubavu watagundua sisi ni mzigo kwao.

Tuache uzembe wa kufikiri, waliompa mgeni madini, wanyamapori, skeletoni, vitalu vya gesi na madini na kila kilichomnufaisha mgeni kutoka Tz ni CCM.
Waliopita walishindwa kuzitumia kwa interests zetu hapo ndiyo yeye abuni ni namna gani watakula huku na Nchi inakula.
 
KATIKA HILI NACHAGUA KUSIMAMA NA RAIS WANGU

View attachment 970211

Nimesoma barua ya maazimio 15 ya Bunge la Umoja wa Ulaya (European Union) kwa serikali yetu ya Tanzania. Maazimio hayo yanabeba masharti magumu kwa sababu kwenye barua yao wanazungumzia ushoga. Lakini pia kuna mambo ya mengine yametajwa kwenye maazimio hayo kama demokrasia na kutetereka kwa Haki za Binadamu.

Tayari Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kama nchi tutapita kwenye wakati mgumu kidogo kwani tutakosa ushirikiano kutoka kwa wahisani kutokana na msimamo wetu.

Mimi nasimama na rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli kuyapinga maazimio hayo kwani inaonesha wazi yamekuja kutokana na msimamo wake thabiti juu ya usimamizi wa rasilimali zetu.

Ndiyo, ni kutokana na msimamo wake juu ya rasilimali zetu kuanzia rais wetu alipozuia mchanga wa dhahabu (makinikia) na kudhibiti Tanzanite, lakini kamwe hatutakubali kuburuzwa na tutaendelea kusimamia mila na desturi zetu.

Tunajua hii ni vita ya kiuchumi na kama taifa tunatakiwa kutumia akili nyingi na siyo nguvu, tupo tayari kuungana na rais wetu kwa kutumia akili zetu nyingi tulizonazo. Tuamini kwamba tunaweza bila hata kuwategemea hao wahisani wenye masharti magumu na yasiyotekelezeka.

Nawaomba Watanzania wenzangu tusimame na Rais Magufuli, tusikubali kuburuzwa na matajiri mpaka tukasahau utu na heshima yetu. Kama nchi huru, tunaweza kuamua mambo yetu wenyewe na yenye kasoro tukayashughulikia ndani sisi wenyewe.

Tukipata nafasi tusome kitabu kiitwacho ‘How Europe Underdeveloped Africa’ chaWalter Rodney ndiyo tutaelewa kwamba Wazungu hawana mpango wa kutuendeleza na wasingependa kuona nchi yoyote Africa inaendelea.
Siwezi kusapoti utawala unao ua watu , tia watu kizuizini bila hukumu miaka, kusema uongo, kudhulumu hela ya wazee wetu nk, wewe una bahati huna mtu kama ndugu kati ya wahanga wa haya juu, ungekuwa kama mimi
 
KWANI HUU WARAKA UNAHUSIANA VIPI NA ccm .... HAPA TUNAONGELEA NCHI BROTHER
Ukitoa la ushoga, yaliobaki nipo pamoja na mabeberu.
images-1.jpeg
 
Inasikitisha sana kuona mtu Msomi kama Eric Shigongo (Msomi wa kuandika hadithi za uongo na kweli) akitoa msimamo usiokua wa kisomi. Ningependa angerejea Historia fupi ya Zimbabwe wakati Robert Mugabe 2006-2009, ndani ya huo muda, Robert Mugabe alivyoamua kuchukua maamuzi kama hayo anayotoa ushauri, na ajiulize;

1) Robert Mugabe yuko wapi sasa hivi???

2) Na Zimbabwe ilikua ina hali gani baada ya kuwekewa vikwazo??? ***Hili swali nisingependa kumpatia jibu Eric Shigongo, wala hahitaji kueleweshwa kwani kaisha thibitisha hana akili ya kutafakari.

Ila ninali jibu swali hili, ili wana JF wenye njaa ya kupata ELIMU na KUFUNGUKA vichwa kuelewa kikichotokea kwa Robert Mugabe, baada ya kufanyiwa vikwazo na EU na USA.

Short History of Zimbabwe Currency (Under the Rule of Robert Mugabe),

● Zimbambwe currency was "redenominated" three times (in 2006, 2008 and 2009), with denominations up to a Zim Dollar $100 Trillion banknote issued. The final redenomination produced the "fourth dollar" (ZWL), which was worth 1025 ZWD (first dollars). Use of the Zimbabwean Dollar as an official currency was effectively abandoned on 12 April 2009.

Tafsiri yake,

Historia fupi ya Hela ya Zimbabwe (Chini ya Utawala wa Robert Mugabe),

KUMBUKA; Zimbabwe walikua wakitumia hela yao ikiitwa Zimbabwean Dollar $ (ZWL/ZIM DOLLAR).

● Hela ya Zimbabwe iliporomoka/kudondoka thamani mara tatu (Mwaka 2006, 2008, na 2009), kuporomoka huko mpaka kufikia hatua ya kutolewa kwa NOTE MOJA ya bank (Pesa Ya Karatasi) yenye thamani ya ZIM DOLLAR "TRILLIONI 100". Mporomoko wa mwisho ulipelekea kutengenezwa kwa "Dollar ya Nne" ya karatasi (ZWL), yenye thamani ya 1025 ZWD (Trillioni Elfu 25).

*** Matumizi ya Zimbabwean Dollar yalifikia tamati na kusimamishwa rasmi mnamo Tarehe 12/04/2009.

-------------- × --------------

Exhange Rate Ya ZIM Dollar kwenda kwenye US Dollar yalifikia; 175, 000, 000, 000, 000, 000/= Quadrillion ZIM Dollar ZWL $ =X= US Dollar $ 5.
_83589275_12_06_zimdollars.jpg

NB Sisi Tanzania tuna NOTE MOJA kubwa ya Shillingi Elfu 10 ndio mwisho wetu, wenzetu Zimbabwe walifikia hatua ya kua na NOTE MOJA ya TRILLIONI 100 na TRILLIONI 25,000.

Swali, Tupo tayari kua na Pesa ya Karatasi (Note Moja) ya Shillingi Trillioni 100??.

Nawasilisha,
 
maneno ya watu wa mitandaoni hayasumbui wakati kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake juu ya swala hili kama mtanzania... so waache wamtukane kwani amebadilika nini? .....yupo vilevile na atabakia kuwa ERIC SHIGONGO tu
Mkuu ndio huyu aliambiwa anywe Maji.
 
Mi elimu yako nishaipita without hata kufikia iyo hali ya kudhikiri uchi ama kwa nguo na ndio maana akili yangu imetulia sipelekeshwi na siasa bali ntaitetea Tanzania popote nilipo bcoz ndo nchi yangu

Watu kama nyinyi inabidi JPM awe nao makini sana. Akija mwingine mtamkana asubuhi mapemaaaa.....Huamuaminiki nyinyi.....you will do anything to win favours za watawala......

Ni kama hawa jamaa akina Kafulila na Msando na wengineo........waliohamia CCM. Kwa mwenye akili fupi atadhani hawa wana mapenzi na CCM au sera zake..

They just want to be on the right side of the rulers. It takes courage, real courage, kuwa upande tofauti na mtawala...more so in Africa.
 
Watanzania tunaojitambua hatuwezi na wala hatutaki kusimama na dikteta na mtenda maovu dhidi ya Watanzania ikiwemo mauaji.
 
Hata tukisimama na Rais wetu tutasaidia nini. Jambo la busara na kuepuka Mbinyo zaidi ni Kukubali tu ..Tuache ubabe usiotusaidia.. Tusimame nae tusisimame kila mtu anajua tutajuta.....Muda tu ni rafiki mzuri tutazisoma namba zote za Kizungu...Maana za kiswahili tumeshasoma zote.
Kama ulikuwa unalipwa buku, na haija badilika unalia lia nini mzee! Tatizo kona nyingi mlizoea ndo maana mnazisoma za kichina, na zitaenda kuwa za kiarabu sasa kama msipoamua kufanya kazi
 
KATIKA HILI NACHAGUA KUSIMAMA NA RAIS WANGU

View attachment 970211

Nimesoma barua ya maazimio 15 ya Bunge la Umoja wa Ulaya (European Union) kwa serikali yetu ya Tanzania. Maazimio hayo yanabeba masharti magumu kwa sababu kwenye barua yao wanazungumzia ushoga. Lakini pia kuna mambo ya mengine yametajwa kwenye maazimio hayo kama demokrasia na kutetereka kwa Haki za Binadamu.

Tayari Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kama nchi tutapita kwenye wakati mgumu kidogo kwani tutakosa ushirikiano kutoka kwa wahisani kutokana na msimamo wetu.

Mimi nasimama na rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli kuyapinga maazimio hayo kwani inaonesha wazi yamekuja kutokana na msimamo wake thabiti juu ya usimamizi wa rasilimali zetu.

Ndiyo, ni kutokana na msimamo wake juu ya rasilimali zetu kuanzia rais wetu alipozuia mchanga wa dhahabu (makinikia) na kudhibiti Tanzanite, lakini kamwe hatutakubali kuburuzwa na tutaendelea kusimamia mila na desturi zetu.

Tunajua hii ni vita ya kiuchumi na kama taifa tunatakiwa kutumia akili nyingi na siyo nguvu, tupo tayari kuungana na rais wetu kwa kutumia akili zetu nyingi tulizonazo. Tuamini kwamba tunaweza bila hata kuwategemea hao wahisani wenye masharti magumu na yasiyotekelezeka.

Nawaomba Watanzania wenzangu tusimame na Rais Magufuli, tusikubali kuburuzwa na matajiri mpaka tukasahau utu na heshima yetu. Kama nchi huru, tunaweza kuamua mambo yetu wenyewe na yenye kasoro tukayashughulikia ndani sisi wenyewe.

Tukipata nafasi tusome kitabu kiitwacho ‘How Europe Underdeveloped Africa’ chaWalter Rodney ndiyo tutaelewa kwamba Wazungu hawana mpango wa kutuendeleza na wasingependa kuona nchi yoyote Africa inaendelea.
Wasukuma bana! Sijui walichelewa wapi?
Yeye asimame nae, sisi tunakimbia mabeberu ya dunia
 
Back
Top Bottom