Kigongoi kwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2018
- 447
- 440
Kumekuwa na hoja zinazotolewa na baadhi ya watu kwamba iwepo tumehuru ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2020. Na kwamba tume hiyo iwe shirikishi ili kuondoa malalamiko.
Binafsi sidharau maoni ya watu wenye mawazo ya namna hiyo kwa sababu wanatimiza wajibu wao wa kutoa maoni kama mimi ninavyofanya.
Moja ya hoja ya malalamiko ni kwamba iliyopo inachaguliwa na mwenyekiti wa chama kinachoingia kwenye ushindani.
Nyingine ni kwamba hata wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama.nk
Hoja zote hizo ni za msingi kabisa.
Rai yangu kwa CCM ni kwamba msikubali tume ya namna hiyo kwa sababu siku mkijaribu kufanya hivyo mtaangukia pua kwa sababu zifuatazo:
1. Sio kweli kwamba wanaohamia huko wanaipenda ccm,wengi wanaohama vyama ni kwa sababu ya ugumu wa kufanya siasa wakiwa upande wa pili.
2. Wengi wanaokuja huko wanaunga mkono juhudi za mh Rais, sio kwa sababu wanakipenda chama. Rejea walichozungumza baada ya kurejea,hawasemi Sera zimewavuta.
3.Wanachama mnaodai ni mil 15 mlionao si kweli,na hata kama wapo kuna wale ambao wanaweza kukishangilia chama mchana lakini usiku wa upinzani. Hivyo ni vigumu kuamini kwamba kundi lote hilo ni CCM.
Pamoja na hayo na mengine nasisitiza mzuie mikutano ya upinzani,mkiruhusu hakika mwisho wenu utakuwa mbaya.
Kumbukeni kwamba upinzani upo tena una nguvu saaan. Msikubali tume huru