Msikiti unaonuka harufu mbaya na siasa kali.

Msikiti unaonuka harufu mbaya na siasa kali.

Status
Not open for further replies.
KWA hisani ya manispaa ya Kinondoni msikiti wa Mtambani karibu na hospitali ya Dr. Mvungi na ubavuni mwa soko chafu na lenye harufu mbaya kuliko yote Tanzania umetunukiwa kuwa na udi na uvumba wa aina yake.
Udi na uvumba huu wenye harufu sawa ya mizoga iliyonyeshwea na mvua kisha kupigwa na jua na kisha tena kunyeshewa mvua au harufu mbaya ya maiti anayeendelea kuharibika kila kukichwa hakika huwafanya pamoja na imani yao Wsswalihina wa hapo kuishukuru serikali kwa kutosikiliza kilio chao miaka nenda, miaka rudi.

Manispaa hiyo ambayo imeruhusu vilabu vya pombe na maduka ya kuuza vileo yastawi karibu na msikiti huo inaelekea inawapenda sana waumini wa Kiislamu kwa hiyo wanaona raha waumini wakistarehe na harufu hiyo mbaya hata mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Inavyoelekea ni kwamba manispaa hiyo haina diwani wala mtendaji yoyote mwislamu kiasi ambacho maimamu hapa wameanza kudai kuwepo na serikali ya Kiislamu Tanzania- hasira yao ninaielewa mie ambaye nimeshindwa kabisa pamoja na jitihada zangu zote kuendelea kuswali msikiti wa Uvundo- au Mtambani kwa jina maarufu zaidi.

Harufu hiyo sidhani kama ina madhara. Maana kama ingelikuwa na madhara mabwana na mabibi afya wa Kinondoni bila shaka wangekwishaisharuri serikali hima kuondoa uvundo huu ili nao wapate thawabu za serikali isiyopendeka kupendwa!

Kutokupendwa huku bila shaka kunachangiwa si haba na watendaji na madiwani kuonekana kubweteka na kuyaachia matatizo kuendelea kuwa matatizo siku ingia, siku nenda!

Nyambaaf kabisa! Kama hamuwezi kufanya harambee ya kusafisha mazingira yanayozingira msikiti wenu wenyewe, hivi mmeshindwa hata kuagiza tani moja ya karafuu kutoka kwa yakhee wa Upembani au manukato kutoka Uarabuni angalau kupunguza makali ya mnuko? Pumbaaf kabisa nyie!!
 
nina sikitika sana kijana kujiita DARWIN hujui kama DARWIN ni muongo au habari kizo hauna halafu hakuna mtu asiye kuwa na dini katika dunia hii kila mtu anadini kwa sababu dini kwa maana ya yake ni mfumo wa maisha yako tafakari tena kijana.

Afadhali huyo Darwin anatoa nafasi ya watu kumchalenge vile wanavyoamini.
Je ni dini gani inayotoa nafasi hio?
Ndio maana nasema Darwin ni hero wangu

Dini nikuamini kwamba kuna kitu unakiamini na mwisho wake hicho unachoamini ni Mungu [hata mti] , je mimi ambaye siamini kwamba Mungu hayupo utaniambia nafuata dini gani?
 
..duu sasa tunaibebesha serikali hadi zigo la kutusafishia nyumba za ibada...du..no wounder watu wanalazimisha serikali ijiunge OIC..KWA AJILI YA KULALA KWA MIGONGO KUSUBIRI MISAADA...thats too idiot way....people think one day this country will be doing cleric functions ....ya kusafisha majumba ya kuabudu,kujenga majumba ya kuabudu,KUSAFIRISHA WATU KWENDA MECCA,.....THATS WHAT PEOPLE THINK ..SIKU MOJA ITAKUWA nchi ya kiislamu...

na hizi tabia za uomba omba tunazilea ..zinasababisha baadhi ya watu kuendelea kujiona duni.....HUWA NAKWERWA SANA HASA KIPINDI HICHI CHA TANADHANI ..KUNA WATU WANAPENDA KUDHALILISHWA NA PIA WANAOPENDA KUDHALILIKA...UKIPITA MAENEO YA DAR UTAKUTA TANGU ASUBUHI WATTOTO KWA WAZEE WAPO KWENYE MA GATE YA WATU WENYE UWEZO WAMEPANGA FOLENI KWA MAMIA ...WANASUBIRI MGAO WA PESA,NA KILO MOJA YA UNGA.....HATA KAMA NI SADAKA SIAMINI KAMA INAFIKA MAHALI PAKE KWA KUDHALILISHA WATU WAKUABUDU KWENYE GATE LA NYUMBA AU KIWANDA CHAKO....NADHANI BORA WATU WAENDE MAKAZINI NA WATOTO SHULENI....ANAYETOA MSAADA APELEKE MSIKITINI JIONI AWAGAWIE WATU.....HII TABIA NDIO INAYOLEA WATU KUWA OMBA OMBA.........HAWA NDIO VIONGOZI WETU WA KESHO TUNAOWAANDAA KUJA KUWA OMBA OMBA PROFFFESSION WAKIWA WAKUBWA.......NDIO HAO WATAKAOKUJA KUWAPIGIA MAGOTI WATU KAAMA KINA BUSH NA KUSAHAU KUWA OUR COUNTRY IS RICH WITH RESOURCES ...HATUITAJI KUBEMBELEZA MTU...AU KUJIUNGA MAHALI KWA AJILI YA MISAADA...

YOTE HII INAAZIA KWENYE KUWA WAVIVU HADI KUSUBIRI SERIKALI IKUFAGILIE NDANI KWAKO ...BASI WAKUSAIDIE NA KUZAA!!!!

Mkuu hesima mbele ila ningekushauri ukapime hizo akili zako labda zimechnganyika na damu kidogo
Hivi unajua kama huo uchafu unatoka soko lililo jirani na huo msikiti ?
sasa uchafu unatoka sokoni kwanini majirani ndio wasafishe hao wafagizi wa soko wako wapi ?
Hivi unajua kazi ya halmashauri ya jiji na kodi wanayochukua ni ya kazi gani ?
 
Pengine Dar ndio kwanza wanazinduka kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa masta plan za miji. Matatizo kama haya yapo na huko Zenj yanazidi kufanyiwa kazi, Cha msingi ni kujua wapi kunakosewa, Je Idara ya mipango miji inasemaje kuhusu hili?

Labda huko bongo mjifunze toka Zenj.. Soma Amri hii ya Waziri huko Zenj

Hivi karibuni Mh. Waziri wa Tawala za Mikoa Visiwani humo aliitaka mahakama hiyo kutotoa leseni kwa vilabu vya ulevi vilivyopo karibu na Maakazi ya watu na nyumba za ibada, na ni baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi toka kwa wananchi.

Pengine ni wakati ambao tunapaswa kujiuliza kuwa ni sehemu zipi za maakazi ya watu, ni sehemu zipi za biashara ni sehemu zipi za elimu ni sehemu zipi za viwanda na ni sehemu zipi za kilimo ndani ya kisiwa hicho. Kwa haraka haraka sio rahisi kujua hilo na hasa ikizingatiwa hali halisi ya mpango wa mji wa kisiwa hicho. Hata ukiangalia master plan ya Mwaka 1982 chini ya Sheria ya Ardhi ya mwaka 1985,.....

Zaidi tembelea Hapa
 
Last edited:
Mkuu hesima mbele ila ningekushauri ukapime hizo akili zako labda zimechnganyika na damu kidogo
Hivi unajua kama huo uchafu unatoka soko lililo jirani na huo msikiti ?
sasa uchafu unatoka sokoni kwanini majirani ndio wasafishe hao wafagizi wa soko wako wapi ?
Hivi unajua kazi ya halmashauri ya jiji na kodi wanayochukua ni ya kazi gani ?

..akili zangu ni kali kama wembe ..nafikiria miaka 20 ijayo....

....soko ni public utility...linatumiwa na watu wote.....sasa soko limekuwa chafu...tufanyeje???....halmashauri zetu tunazijua ...ina malori ya taka hayazidi 10...kuwahudumia wana kinondoni say milioni 2.....soko letu wote ...je tunangoja hadi halmashauri ipate uwezo wa kununua magari ya taka ya kutosha ....au tunachukua machepe na kuwaalika majirani wote wakiwemo wa dini nyingine kufanya usafi ...ILI TUSIFE KWA KIPINDU PINDU ..NA MAGONJWA YA HEWA ie TB.......nadhani jibu nirahisi ......tunayo kazi ya kufanya ...,tusisubiri serikali......sisi tulioamini kwenye ujamaa..tunaami kwenye kazi za kujitolea.....

.....naomba nitoe changamoto..je tunawalea watoto wetu kuamini kuwa hata usafi ni jukumu la kwanza la serikali???..miimi nimefundishwa ..usafi ni jukumu la MTU BINAFSI[mwili wako],FAMILIA [nyumba yenu],MTAA[Mtaa wenu],JUMUIA [kanisa lenu,msikiti wenu,shule yenu]..ets ..serikali ni ya mwisho kwenye mlolongo[PROVIDES INFTRASTRUCTURES]

..laiti maeneo yenye misikiti mingi jijini kama BUGURUNI,TEMEKE,TANDALE ,VINGUNGUTI,ILALA,MTAMBANI,MSASANI-MAANDAZI RD,..ETC.....yangeamua kusisitiza juu ya usafi na afya ya jamii...basi serikali ingekuwa na kazi rahisi sana ya kuongezea pale juhudi zao zinapoishia...kipindu pindu kingekoma.....najiuliza kwanini kila mara kipindu pindu huanzia maeneo haya ...kama kila msikiti ungepata kisima kirefu,kituo cha afya,kituo cha elimu jamii,...na kuhimiza usafi basi mwelekeo wa wakazi wa maeneo haya ungejikita kukataa uchafu.....

sio kila jambo wanalofanya wakristo ..halifai kwa wenzao...makanisa yote huwa na zamu za kaya kusafisha mazingira.....huwa na vituo vya afya,na malezi [early child hood]...huwa na utaratibu wa kutembelea familia zote duni.......sasa kwa sababu watanzania niu ndugu ..kuna haja ya kubadilishaana uzoefu..ili kuhimiza nyumba zote za ibada zitoe huduma ya mwili na roho kwa jamii.....badala ya kudhani kila wazo lina nia mbaya ..tu kwa sababu limetolewa na dini tofauti..we sail in the same boat!!!
 
PM mchango wako wa mwisho umeuweka sawa..tofauti na Awali.

Kimsingi waislam hadi sasa wamekuwa wanatumia Njia za Diplomasia kuondoa Hali Hio.Huo ushauri unaotoa Hapa Mkuu PM, tayari ushafanyiwa kazi several times...labda tu haujawa publicised...

Wamefanya usafi lkn taasisi husika za kusimamia hazijachukua nafasi yake...Pia wamekuwa wanafanya mazungumzo na wahusika wa Jiji la Kinondoni, Uongozi wa Soko lkn bila ya Mafanikio.

nafikiri njia iliyobaki ni waislam kuchukua Hatua za Mikono yao!!! Nafikiri hio njia pekee iliyobaki ya kulifanya soko la Mtambani liwe safi...
 
tunaishi katika serikali mfu...ukianguka barabarani, ukigongwa na gari, jambazi akikutembelea usiku... unasaidiwa na wasamaria wema waliokaribu hakuna cha ambulance wala 911, kwa maana hiyo basi..kulalamika na kusubiri serikali ije isafishe soko ni sawa na kupiga gitaa halafu unamsubiri mbuzi acheze...hata mkiandamana watasafisha mara moja halafu hamtawaona tena...kwa hiyo basi hapo kuna matatu hamisheni msikiti au pangeni zamu za kusafisha pamoja na majirani zenu wengine au pigeni moyo konde muendelee kuwa wavumilivu
 
tunaishi katika serikali mfu...ukianguka barabarani, ukigongwa na gari, jambazi akikutembelea usiku... unasaidiwa na wasamaria wema waliokaribu hakuna cha ambulance wala 911, kwa maana hiyo basi..kulalamika na kusubiri serikali ije isafishe soko ni sawa na kupiga gitaa halafu unamsubiri mbuzi acheze...hata mkiandamana watasafisha mara moja halafu hamtawaona tena...kwa hiyo basi hapo kuna matatu hamisheni msikiti au pangeni zamu za kusafisha pamoja na majirani zenu wengine au pigeni moyo konde muendelee kuwa wavumilivu
 
Kuna wengi wetu tumeliingiza suala hili la uchafuzi wa mzingira na imani za kidini.Kwamba Waislamu wa msikiti wa Mtambani ni wajinga kwa sababu wanaitaka Manispaa kutimiza wajibu wake wa kufanya usafi ni uchokozi usiokuwa na hoja ya msingi.

Wengine kujiita Darwin n.k kunaonesha kuwa hisia zao ni anti religion na kwa kuwa Waislamu wanakereka na harufu mbaya ni kwa sababu ya Uislamu wao.Wangekuwa na hisia za ki-darwin wangetulia wakavumilia harufu mbaya hata kama wanalipa kodi ili huduma ya usafi ifanyike.

Huyu wa Darwin anaungana na wale waliojichanganya na mada na kuanza kutaja OIC n.k ambao ni anti Islam na wana chuki binafsi ambazo wameona wasitoe hapa.

So to conclude ni kuwa hisia za baadhi ya wachangiaji wa dini tofauti na Uislamu na zile za wasioamini kuwapo kwa Mungu kama Darwin zinajitokeza si katika kukemea Manispaa na kuifanya itimize wajibu wake ila wamejikita na kuushambulia Uislamu.

Kwa wale wa dini tofauti wamelipandia suala hili ili wafanye crusade na Darwin naye kapata fursa ya kumshambulia Mwenyezi Mungu kwa kuwa haamini kuwepo kwake.

Sasa suala kubwa hapa ni uchafuzi wa mazingira ambao ni sawa kabisa na kuweka dampo la uchafu katikati ya jiji na harufu mbaya ikazagaa sehemu muhimu za huduma kama vile hoteli na maduka.

Hapa hakutakuwapo na Darwin,John au Ally.Wote tutahusika na kuikemea Manispaa kwa kutotimiza wajibu wake.

Na inatakiwa iwe hivyo hivyo katika eneo lote la Mtambani kwa sababu hapo ni mahali ambapo kuna kila aina ya watu.Msikiti ni eneo tu ambalo kero hii imejitokeza lakini ni sehemu kubwa ya jamii inayoishi maeneo hayo inajikuta na matataizo kama yale yanayoonekana msikitini.

Instead of condemning Muslims etc etc...let all the residents of the area come out and shout,"Fanyeni kazi yenu kama serikali kwa kuwa tunalipa kodi"
 
,"Fanyeni kazi yenu kama serikali kwa kuwa tunalipa kodi"


.....mambo mangapi hayafanyiki na kodi tunalipa ..tunavumilia..lakini hili la uchafu halivumiliki kwa kuwa linatuletea kipindu pindu na tb na kutuuwa....kuliko kuvumilia hili ni MUCH BETTER KU VOLUNTEER...KUFANYA KAZI HIZI KWENYE MAZINGIRA YANAYOTUZUNGUKA..
 
Darwin kama jina langu:

Swali nikujiuliza hapo

Nani wa kwanza? Msikiti au soko?

Kama msikiti ndio wa kwanza kujengwa kabla ya soko basi manispaa inahusika kuweka soko ambalo ninatoa uvumba kwahio watoe suluhisho.

Kama soko ndio la kwanza ukaja msikiti basi Msikiti waliyataka wenyewe kwani waliyajua hayo mazingira toka zamani.

Mwisho kama yaliwekwa yote kwa pamoja, manispaa kwa wakati huo waliweka uwiano gani?

Naona wengine hapa wanajibu tu kushabikia dini zao bila kufikiria cha kusema.


Darwin,Mtanzania ambaye anayejivunia kwamba hafuati dini za wakoloni.

Hapa kuna wanadhihirisha below pars zao..na posting ni ushahidi tosha.

1. Tatizo ni deen ya mkoloni au deen yenyewe?

2. Tupe unamaanisha nini unaposema deen za wakoloni..
 
Afadhali huyo Darwin anatoa nafasi ya watu kumchalenge vile wanavyoamini.
Je ni dini gani inayotoa nafasi hio?
Ndio maana nasema Darwin ni hero wangu

Suala la kuchallenge deen? ili iweje? deen ya kweli ni utaratibu walioupokea walioamini kutoka kwa Mola wao,ili kuzifaidisha roho zao... sasa uichallenge halaf ndio iwe nini?

Unadhani deen ni siasa?
 
Kwa wale wa dini tofauti wamelipandia suala hili ili wafanye crusade na Darwin naye kapata fursa ya kumshambulia Mwenyezi Mungu kwa kuwa haamini kuwepo kwake.

Kwa kuwa umependa kuweka generalization, nakujibu kama ifuatavyo:

Binafsi naipenda crusade ikiwa ni dhidi wa watu wagomvi, wavivu, wazembe, waoneao wenzao vijicho na walalamishi.

hakika mtu mwenye sifa nilizozitaja wasitegemee kwenda peponi, wanadanganyana tu na kupeana morali za kijinga..
 
Mbunge i dont see the connection between the story and SIASA KALI or was it intentional? Shame on you nungunungu for calling people of other faiths names, poeple like you give muslims a bad name.I have also detected religious overtones in some of the other posts.I wish we can discuss issues with an open mind,and by the way some of the suggestions are quite good.Let us the educated set an example and not be blinded by our religious leanings.For the record i dont support Kikwete's BEGGING trips[$22m on this last US trip]this is within our MEANS.
 
Maoni yaliyotolewa ni mazuri kwa uelewa wa kila mmoja aliyechangia. Ushauri wangu ni kwamba viongozi wa msikiti hua wa Mtambani wawasiliane na uongozi wa soko wajadili hali hiyo. Pili ikishindikana waende kwenye ngazi za juu. Kwani wafanyabiashara hapo sokani wanalipa kodi ambayo kazi yake mojawapo ni kulipia usafi. Na mwisho msikiti unaweza ukapanga siku moja waumini wajitolee kufanya usafi katika soko hilo kama fadhila kwa serikali yao na jirani zao mbao ni soko hilo linalonuka. Nawataika mfungo mwema. Kuwaita viongozi makafiri si...........
 
..akili zangu ni kali kama wembe ..nafikiria miaka 20 ijayo....

....soko ni public utility...linatumiwa na watu wote.....sasa soko limekuwa chafu...tufanyeje???....halmashauri zetu tunazijua ...ina malori ya taka hayazidi 10...kuwahudumia wana kinondoni say milioni 2.....soko letu wote ...je tunangoja hadi halmashauri ipate uwezo wa kununua magari ya taka ya kutosha ....au tunachukua machepe na kuwaalika majirani wote wakiwemo wa dini nyingine kufanya usafi ...ili tusife kwa kipindu pindu ..na magonjwa ya hewa ie tb.......nadhani jibu nirahisi ......tunayo kazi ya kufanya ...,tusisubiri serikali......sisi tulioamini kwenye ujamaa..tunaami kwenye kazi za kujitolea.....

.....naomba nitoe changamoto..je tunawalea watoto wetu kuamini kuwa hata usafi ni jukumu la kwanza la serikali???..miimi nimefundishwa ..usafi ni jukumu la mtu binafsi[mwili wako],familia [nyumba yenu],mtaa[mtaa wenu],jumuia [kanisa lenu,msikiti wenu,shule yenu]..ets ..serikali ni ya mwisho kwenye mlolongo[provides inftrastructures]

..laiti maeneo yenye misikiti mingi jijini kama buguruni,temeke,tandale ,vingunguti,ilala,mtambani,msasani-maandazi rd,..etc.....yangeamua kusisitiza juu ya usafi na afya ya jamii...basi serikali ingekuwa na kazi rahisi sana ya kuongezea pale juhudi zao zinapoishia...kipindu pindu kingekoma.....najiuliza kwanini kila mara kipindu pindu huanzia maeneo haya ...kama kila msikiti ungepata kisima kirefu,kituo cha afya,kituo cha elimu jamii,...na kuhimiza usafi basi mwelekeo wa wakazi wa maeneo haya ungejikita kukataa uchafu.....

Sio kila jambo wanalofanya wakristo ..halifai kwa wenzao...makanisa yote huwa na zamu za kaya kusafisha mazingira.....huwa na vituo vya afya,na malezi [early child hood]...huwa na utaratibu wa kutembelea familia zote duni.......sasa kwa sababu watanzania niu ndugu ..kuna haja ya kubadilishaana uzoefu..ili kuhimiza nyumba zote za ibada zitoe huduma ya mwili na roho kwa jamii.....badala ya kudhani kila wazo lina nia mbaya ..tu kwa sababu limetolewa na dini tofauti..we sail in the same boat!!!

sasa kama umekubali soko ni public utility hao wauza soko wanalipa kodi hiyo kodi inafanya nini ?
Sisi hayo magari 10 hayatuhusu tunahitaji huduma isitoshe hata hao majiarani wanalipa kodi jiji kwa ajili gani? Au kudumisha ufisadi
mbona zamani kodi ilikuwa kidogo na walikuwa wanasafisha kama utakumbuka enzi zile yale mafiat kama ya ulaya yalikuwapo dar

kuhusu usafi kwa taarifa yako msikiti ni msafi kuliko kanisa kama ufahamu
kama akili zako kama wembe basi uwe una fikiri kama mtu mzima
[/size]
 
kuhusu usafi kwa taarifa yako msikiti ni msafi kuliko kanisa kama ufahamu
kama akili zako kama wembe basi uwe una fikiri kama mtu mzima

Punguza jazba..


Mimi siamini Msikitini kama kweli ni Nyumbani kwa Mungu, yet siwezi kuja na comparisons za kipumb-avu kama hizi..

Sasa ukiwa hujafunga huwa unakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
kuhusu usafi kwa taarifa yako msikiti ni msafi kuliko kanisa kama ufahamu
kama akili zako kama wembe basi uwe una fikiri kama mtu mzima[/size][/size]
mkora eti kama hujafunga huwa unakuwaje???? kama kwenye mfungo unatoa matamshi kama haya......je ikifika mwezi wa 12 si balaa
 
kama muumini nadhani hoja ya usafi wa msikiti na maeneo yanaozunguka iwe juu yetu, hapa hoja si srikali, mana uchafu ni makruuh, na ni vyema tukazingatia maoni na maagizo ya kiongozi mkuu wa dini ya kiislam aliyesema, " AL ISLAAM NADHIIF FATANADHAFUU FAINNAHU LAA YADKHULU LJANNA ILLA NADHIIF
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom