Msikiti uliojengwa miaka 1000 wagunduliwa UAE

Msikiti uliojengwa miaka 1000 wagunduliwa UAE

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Msikiti uliojengwa miaka 1000 iliyopita wagunduliwa Imarati
TEHRAN (IQNA) - Wanaakiolojia huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) wamegundua msikiti unaokadiriwa kuwa uliojengwa miaka 1,000 iliyopita katika eneo unakojengwa Msikiti Mkuu wa Sheikh Khalifa mjini Al Ain karibu na mpaka wa nchi hiyo na Oman.
Magofu ya msikiti huo yametajwa kuwa ya zama za Ukhalifa wa Bani Abbas na yamepatikana karibu na falaj (njia za kumwagilia mashamba maji) na ulijumuisha kwa uchache majengo mtatu ya matofali.
Wanaakiolojia wa Idara ya Utamaduni na Utalii Imarati wanasema magofu ya msikiti huo yanaonyesha mihrabu ilivyokuwa na kwamba inakadiriwa kuwa waumini waliswali nje na ndani ya msikiti. Aidha wanaakiolojia wamepata mabaki ya vyungu ambavyo yamkini vilikuwa vikutumiwa kwa ajili ya maji ya udhuu au masuala mengine yanayohusiana na msikiti. Uchunguzi uliofanywa kwa kutumia mbinu ya radiocarbon umebaini kuwa msikiti huo ndio wa kale zaidi kuwahi kugunduliwa UAE hadi sasa.
 
Picha iko wapi ?
Habari nzito kama hii unakuja mikono mitupu bila Picha!!
Sawa ila Maneno matupu sawa na kutulisha matango
kama huna picha tafadhari futa uzi orait!
Bila picha habari hii haieleweki kabisa...
Siwezi kusoma thread haina picha . itakuwa ni nadharia tu
Ungetupiamo ka picha boss
20180909_153353.jpg
 
Daaah mbona kalikua kadgo sana watu ishirini wakipanga safu hapo hawatoshi
 
Back
Top Bottom