Msikilize Lusinde akiuza sera za CHAMA CHA MAPINDUZI

Ni heri nikae choo cha kiswahili hata siku nzima kuliko kusikiliza utumbo wa Lusinde. Aiseeee, kumbe ndiyo ndiyo maana ccm walishindwa uchaguzi. Hivi waliokuw wanashangilia hotuba ni wameruuuuuu au ni wanamuziki w TOT?
 
Yaani inasikitisha kuna watanzania walikaa wakimshangilia hadi akamaliza.
Hii ni aibu.
 
Amedhihirisha kuwa yeye ni unsound mind
 
kifaa cha ccm hicho, tena mjumbe wa halmashauri kuu!
sisi cuf na cdm tunamshukuru ametuongezea credt
 
huyu jamaa ashtakiwe!! amedhalilisha wanawake!!kwani mimba dhambi..eti wanunulie maembe mabovu, duh!!
 
WALIOKUWA WANASHANGILIA LAZIMA WATAKUWA WANAMUZIKI HAO tu...
Ni heri nikae choo cha kiswahili hata siku nzima kuliko kusikiliza utumbo wa Lusinde. Aiseeee, kumbe ndiyo ndiyo maana ccm walishindwa uchaguzi. Hivi waliokuw wanashangilia hotuba ni wameruuuuuu au ni wanamuziki w TOT?
 
Hadi aibu, ptuuuuuuu! Mtu mzima Hovyooooooo!
 
hahahaahah Nimecheka kuisikia hii hotuba ya Mzee Lusinde Kudadeki kweli hii kali hata haijazimuliwa hata kidogo kama ni pombe itakuwa ni Gongo wacha weee.............. Luuuuuuuuuuusiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ndeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Yesu na maria. Hayo ndio maneno ya kampeni ya kuomba kura? Duu yanatia aibu. Nilidhani nasoma matusi ya wale wa uwanja wa fisi manzese siamini yametoka kwenye kinywa cha mheshimiwa mbunge! Hakuna sera wala ahadi ni matusi tu hapo.
 
Yesu na maria. Hayo ndio maneno ya kampeni ya kuomba kura? Duu yanatia aibu. Nilidhani nasoma matusi ya wale wa uwanja wa fisi manzese siamini yametoka kwenye kinywa cha mheshimiwa mbunge! Hakuna sera wala ahadi ni matusi tu hapo.
 
Nimesikitishwa sana na speech ya Matusi ya Lusinde maana dhamira yangu inakataa hata kumwita Mheshimiwa!!!!!!!!!!
Alipokuwa anagombea ubunge mtera nilijua watanzania tumepata kifaa tumaini letu jipya. Kijana smart, msomi na very challenging, lakini sikujua kuwa Lusinde hafai hafai hafai hafai namna hii?!!!!! Usomi na uheshimiwa wote akaweka kando akaanza kubwabwaja matusi kama vile mbele yake hakukuwa na watoto na watu wanaomzidi umri!!!! Heshima gani hii tujifunze kwa chama kikongwe kama ccm!!! Naanza kuamini sasa kuwa ukimuona mtu mzima analia ujue mambo ni magumu. Chadema kinawakosesha usingizi ccm. Lakini kosa si la chadema bali ni la ccm wenyewe. Waungwana waliwaambia kuwa chama ili kirudi kwenye mstari kinahitajika kufanyiwa overhauling. Lakini asiyesikia la mkuu................ cha ajabu hasira zote chadema. Jirekebisheni tu hata bila kuwataja chadema wananchi watakiamini chama. Mzee Butiku kaongea na wengine wameongea lakini hamuwasikii kuwa ccm kinaelekea kufa. Bila kujitakasa na dhambi ya miaka mingi hamtatoka wananchi wameshaamka. Poleni kwa kutukana.

USHAURI KWA CHADEMA:
1. Mfungulieni mashtaka Lusinde maana ushahidi upo tena very valid.
2. Acheni ccm watukane nyie elezeni mapungufu yao kama ufisadi, ubabe, kulindana, ahadi nyingi zisizotekelezeka nk.
3. Anzisheni vyombo vya habari kama TV ili kuwafikia wananchi wengi. Propaganda dhidi yenu ni kubwa
4. Vijijini mwamko bado si mkubwa sana. na huko ndo mtaji wa ccm. wale wakiamka ccm hawawezi kutoka.

Kazi njema
 
kwa kweli ndugu yangu hii uliyosema ni kweli kabisa..! unajua sio kwamba viongozi hawajui matusi..! sio kwamba viongozi hawafahamu lugha mbaya..! lakini kama kiongozi tena ambaye ameaminiwa na wananchi kupewa jukumu kubwa la kuwa wakilisha tena sio sehemu ya muhimu kama bungeni..! hata mkiwa watu watatu tuu..! na ukachaguliwa kiongozi..! inabidi uwe na uchaguzi wa neno lipi uliongee wapi..! laa sivyo wewe unakua hufai kuwa kiongozi..! hata watu walio kua wanatetea haki za watu huko zamani kwenye historia mfano Martin Luther king jr. ambao walikua na reason kabisa ya kutoa maneno machafu..! sio kwamba walikua hawajui maneno machafu ya kutumia..! lakini kwa sababu walikua viongozi wanao jua nini maana ya kua viongozi..! walijua ni maneno yapi ya kuyatumia na wakati gani..!

picha aliyo ionyesha huyu kiongozi..! kwa kweli hata mimi ninasita sana kumuita kiongozi..! maana hata ukiangalia hii clip mwishoni kuna watoto wa shule ya msingi nadhani kama sikosei wanaonekana wanashika midomo kushangaa kwamba "hivi huyu ni mtu mzima kweli..!? ukiambia analingana na baba angu..!? na hivi ni kweli ninayasikia haya kutoka kwa mtu kama huyu..?" yani tuna kipa kizazi kijacho mfano ambao ni utata mtupu..! mtoto kama yule anapata shida kujua afanye nini..!? nyumbani mzee anamwambia matusi ni dhambi halafu akija anakutana na mtu wa heshima anatoa matusi halafu akirudi nyumbani unategemea atajisikiaje akimkuta baba yake anamshabikia lusinde..? si atapata utata mkubwa sana....?

jamani uongozi sio huu..! mimi siandiki haya kushabikia chama chochote ila nadhani hata wale watoto wameona kua hiki sio chama..! sasa kama mtoto anaweza kun'gamua suala kama hili hivi mtu mzima unaposhindwa wewe si ni kama kichaa tu..!? kwa sababu ninaamini kua vichaa wanauelewa uliopo chini kidogo ukilinganisha na watoto..! jamani mimi nadhani huyu hafai kua kiongozi hata wa familia yake..! sisemi hivi kumdhalilisha ila unadhani watoto wake wanajifunza nini hapa kutoka kwa baba yao (kama ameoa)..?

nilimsikiliza juzi wakati anahojiwa clouds.. kitu alichosema mwisho baada ya kuulizwa na kibonde kua "kama mwerevu... kichaa akikuvua nguo na kukimbia nazo utamfukuza au utakaa..?" lusinde alijibu kua "utakaa"

jibu hili lilimfunga mwenyewe na kumuonesha kwamba sio muerevu hata kidogo kwasababu alisema kua aliyaongea yale maneno ili kuwajibu chadema ambao walikua wanawatukana... sasa kama chadema wamekutukana wewe kama mwerevu unawatukana pia au utakaa..! yeye aliwatukana pia so hapo hajaonesha uerevu wowote na yeye amekua kichaa.. hata hivyo ni kama tu chadema nao walitoa maneno machafu kama aliyo yatoa

inasikitisha sana...!
 
Kweli CCM mna sera nzuri, lakini hazina tija kwa Mtanzania wa leo wala yule wa kesho
 
Kweli CCM mna sera nzuri, lakini hazina tija kwa Mtanzania wa leo wala yule wa kesho

Umeona eeeh! sijui Rejao,ritz,mafilili huwa wakisoma hii wanajiskiaje?
 
Huu ndio ujumbe muruwa kwa ccm

"The hand writing on the wall" (or "the handwriting on the wall" or "the writing is on the wall" or "Mene Mene"), an idiom, is a portent of doom or misfortune. It originates from the Biblical book of Daniel chapter 5 in which the fingers of a supernatural hand write a mysterious message in the presence ofBelshazzar, king of Babylon, who is meanwhile drinking at a major feast. It is revealed by Daniel that the writing foretells the demise of the Babylonian Empire and the story concludes with the Persians capturing Babylon. The phrase "the writing is on the wall" is now a popular idiom for "something bad is about to happen.
 
CCM wanajivunia na wanamwita LUSINDE kuwa ni JEMBE la CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…