Msigwa akubali rasmi Magufuli ni Rais wa Jamhuri ya Muungano

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,282
38,359
Akijitetea kuhusu kupiga picha na Rais, amejitetea kuwa, alikuwa hana namna sababu ile ni nafasi adimu kupiga picha Na Rais/ Mfalme wa nchi...

Alipoulizwa kwa nini alisimama jirani Na Dr.Tulia Naibu spika, kwa nini asingesimama mbali....amesema Rais Mwenyewe ndio alimwita kuwa njoo usimame hapa....Na yeye sababu ameitwa Na Rais/Mfalme wa nchi alikuwa hana namna sababu Yule ndio Raisi wetu Na ile ni nafasi pekee.

Kuhusu ugomvi Na Magufuli.... amesema wao (UKAWA) hawana ugomvi Na Rais Magufuli.....ila wanaugomvi Na taasisi ya Urais.

My take.....
Siasa za Upinzani wa Tanzania ni zaidi ya Maigizo.!
 
Ndio wanaanza hivyo mmoja mmoja
Wanalazimisha watu wakose posho zitakazowasaidia kulipa madeni wakati wenyewe wana mihela ya kuuza chama wameficha nje ya nchi
 
13715971_1045083542250315_1601063364109782543_n.jpg
Hivi si walisema watasusia kila kitu cha serikali? Macho yote wamepiga kwake. Naye anajifanya kumwangalia Tulia, wasi wasi zake tu.
 
Wakati cdm na lowasa wakikomaa kuwa waliibiwa kura na edo ndo alishinda msigwa akasisitiza magu ni raisi halali aliyechaguliwa kidemocrasia
 
Mpinzani wa kweli hawezi kuwa kama nyasi kufuata upepo

Daima atasimama palepale hadi lengo litimie..!
 
Bado sijajua UKAWA wanasimamia Na kutetea nini ndani ya siasa za Tanzania.
hahaha kamanda. hukumsikia Lowasa anasema, wanataka na wao washike dola tu. tuonje utamu wa madaraka. hakuna cha sera wala sijui kusimamia nini. hayo yote yatajulikana baada ya kukamata dola.kamata dola kwanza kamanda. mengine baadae
 
Tz bado haijapata wapinzan wa ukwel! Asilimia 90 ya wapinzan ni wasaka tonge tu maana ukiwafuatilia historia zao asilimia kubwa wamehama kutoka chama kimoja kwenda kingine baada ya kunyimwa nafasi ya uongozi!!!
 
Na baya zaidi alimwamkia "shikamoo Rais" dah! Ama kweli mbayuwayu ana akili kuliko Ukawa!
wewe mnafiki na mpandikiza chuki ndio una akili za mbayuwai,sijui ulidhani kutomsalimia raisi ndio upinzani,jiongeze wewe,hata seif aliumwa na shein akamtembelea kumpa pole,mbona hakusema asije hapa.
 
Back
Top Bottom