Umeandika kwa busara sana....
Ingawa nakiri niliolewa sababu ya kupenda; uamuzi nilochukua ulikuwa very risky...
Lazima kuwe na cha ziada...kilikuwepo ingawa by then hakikuwa that important ila kwa sasa nafurahia chaguo langu.
Ukute umeoa dad mzuri wa muonekano ...lakini anakupeleka puta...utavumilia ila ikifika pale umeanza kumuona kama dada yako; atakukomaje???
Unatakiwa uwe na sababu zaidi ya tatu za kumkubali mtu awe mwenza wako wa maisha...ukiona unajiuliza jibu linakuja moja tu 'Mzuri' jua unakoelekea kubaya.
Huwezi kumpenda mtu with no reasons. Vigezo vyote unavyovipenda awe navyo mwenzi wako ndio vinapelekea upendo uzaliwe kati yenu. Upengo huo unakamilishwa na satisfaction ya tendo la ndoa. Ndio mapenzi yenyewe.
Ukweli unabaki pale pale.. Hapa duniani hakuna mtaalamu wa ndoa.
Kuna wanaooana kwa mapenzi.. ndoa zinawashinda
Kuna wanaooana kwa mapenzi.. ndoa zinadumu
Kuna wanaooana bila mapenzi... ndoa zinawashinda
Kuna wanaooana bila mapenzi.. ndoa zinadumu
Kuna wanaoendana tabia kama mapacha.. ndoa zinawashinda
Kuna wasioendana kabisaaaaa.. ndoa zinadumu
Kuna wanaoishi kwa mazoea.. ndoa zinadumu
Kuna ambao hata hawajui kwanini walioana.. ndoa zinadumu!
Kuna wanaochunguzana miaka kumi.. ndoa zinawashinda
Kuna ambao hawaoani kabisa.. wanaishi tu.. miaka nenda rudi hawana tatizo.. wako happy
Kuna wanaokutana na kuoana ndani ya miezi miwili.. ndoa zinadumu.....nakadhalika.. nakadhalika.
AND VICE VERSA
Bottom line:
1. Kama unataka kuoa/olewa fanya hivyo pale utakapohamua. Kama hutaki/hujaamua ACHA.
2. Kama uko kwenye ndoa, live each day as it comes. Enjoy the moment
3. Kama ndoa yako ina amani, mshukuru Mungu wako.. usiseme ni kwasababu nilifanya hivi.. au nilifanya vile..
4. Ukioa/olewa ishi the best way unavyojua wewe. The end will justify the means
5. Mwisho, kumbuka ndoa ni ARTIFICIAL sio natural. Naturally, binadamu hauko wired kuishi na mtu mwingine for the rest of your life.
Wrong!
Kuna mapenzi
Kuna ngono
Kuna kupenda
Kuna maisha
Haya ni mambo tofauti sana inatakiwa ujifunze ili uweze kuyatofautisha
Unaweza kuwa na mapenzi na mtu lakini akawa sio mzuri kitandani[ngono]
Unaweza ukampenda mtu lakini usiwe na mapenzi nae
Unaweza ukawa na mapenzi na mtu lakini usimpende
Unaeza kuwa na mapenzi na mtu lakini akawa hajui lolote kuhusu maisha
Utakapoweza kuyatofautisha haya utajikuta unafnya maamuzi sahihi sana kwenye maisha yako!
Baada ya kusoma maoni ya watu nimebaki na swali...kwani ukimpenda mtu unakuwa umependa nini hasa?????????????
Unajua unaweza kumpenda mtu sababu ya tabia au muonekano au basi tu hata sababu huna.
Kumpenda mtu kwa muonekano mara nyingi ni kumtamani...lust...lakini ndio mwanzo wa mapenzi ya kweli au kuonjana tu.
Sidhani kama kuna mtu humu ata feel proud kujua mwenza wake alimtamani...kila mtu angependa kujua kuwa kuna cha ziada kilichofanya achaguliwe yeye badala ya yule...kama ni muonekano tuuuu; what if ataonekana mwingine?
Ukiwa na cha ziada unakuwa more secured.
Huyo anayejisifu kujua kugegeda...what if akiugua magonjwa yanayotumia dawa kali ulijali wake ukapungua...?
Marriage is not only about sex wajameni...ni union ya mambo mengi saana unless mnazungumzia hizi za dot.com
mi nilishakubali kuwa kilaza wen it comes ni wewe
lakini saasa sio kilaza kihivyo bana
Haya mama,hebu nielewesha hapa kweny bold unamaanisha nini!
elewesha mimi katika akili zangu za darasa la 2B sio za chuo kikuu kama zako!lol!
Unaweza ukampenda mtu lakini usiwe na mapenzi nae
AmpenziUnaweza ukawa na mapenzi na mtu lakini usimpende
hata hivyo ukimpenda mtu una vigezo vyako na ndio sababu zenyewe hizo.
Watu huwa wanaangalia sana mapenzi bila kukagua mabo mengine
Kuna ndoto zenu binafsi
Kuna ndoto za kifamilia
Kuna uwezo wa kukabiliana na changamoto
Kuna uwezo wa kutengeneza mahusiano mema na watu wengine
Ndoa ni maisha sio mapenzi!!
[SIZE=-1]
[/SIZE]:disapointed::disapointed:[SIZE=-1]
"It is commonly a weak man who marries for love."
[/SIZE]Samuel Johnson[SIZE=-1]
[/SIZE]
hivi unaweza kumpenda mtu bila kuwa na sababu mbili tatu zinazokuvutia kwa huyo mtu? basi wengine tuna vigezo vyetu vya kupenda. lolSijakuelewa
Kwanza kumpenda mtu hakuhitaji vigezo
Mapenzi nayo hivyo hivyo
!
Ndoa zina mambo mengi sana...kuna kaka mmoja mkewe ni mkarimu sana na alisomea kupika basi anajua kupika kupita Sheraton. Basi yule kaka kwa kukaribisha watu kwake...yani yuko proud sana na mkewe...tena anakwambia kabisa Nyumba kubwa karibuni dinner kwangu....mkisifia msosi basi utamsikia...'Panga siku wife akufundishe kupika' ...Huyu kaka mapenzi kwa mkewe hayachuji kwa kuwa hata jamii inamkubali mkewe...yuko proud saaana kwa watu...kwa ufupi anamringishia mkewe kwa watu vibaya mmno. Kwa hiyo nakubali jamii ikimkubali mkeo inakufanya kila siku nawe ukumbuke kuwa she is special
Dah!
Inaonekana hujasoma kabisa nilichoandika
Hebu rudia tena!