Msiende kukopa benki mikono mitupu JK

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,904
21,992
Msiende kukopa benki mikono mitupu – JK
Shadrack SagMsiende kukopa benki mikono mitupu – JK
Shadrack Sagati, Simanjiro
Daily News; Sunday,September 14, 2008 @00:02

Habari nyingine
Ulanga kuua mbwa wanaozurura ovyo
Kibaka akatwa masikio na kuuawa Dar
TRL yapata mabehewa mitumba
Pinda ataka Rukwa waache ushirikina
Msiende kukopa benki mikono mitupu – JK
Mambo yaiva Tarime
Mwanafunzi agongwa na kufa
RC ashukuru madhehebu
Wakimbizi zaidi wa Burundi warejea kwao
Albino aliyenusurika ashukuru vyombo vya habari

Rais Jakaya Kikwete amewataka wananchi wa Wilaya ya Simanjiro, Manyara, kubuni miradi ya biashara itakayowawezesha kupata mikopo katika benki ya NMB badala ya kwenda kukopa mikono mitupu. Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati alipofungua tawi la NMB mjini Orkesumet hivyo kuwa benki pekee itakayoanza kutoa huduma wilayani hapa.

Alisema benki hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali waweze kukopa pamoja na wafanyakazi kupitishia mishahara yao. “Nendeni na michanganuo ya miradi sio mikono mitupu eti kwa kuwa Rais kasema mpewe mikopo,” alisema Rais Kikwete wakati akiwahutubia wananchi hao.

Aliwataka waache kuweka fedha kwenye mitungi na kuchimbia ardhini badala yake waitumie benki hiyo. Awali Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Misheck Ngatunga alisema tawi hilo limefunguliwa kutokana na mazungumzo kati ya NMB na serikali ili ifungue matawi katika wilaya mpya 15 kuwarahisishia wananchi kupata huduma ya kibenki.

Ngatunga alisema tawi hilo litakopesha wajasiriamali, kuwasaidia wakulima kwenye shughuli ya kilimo na biashara. Alisema matawi mengine saba yatafunguliwa mwezi huu katika wilaya za Kilindi, Ruangwa, Kilolo, Misenyi, Mvomero, Bukombe na Longido. Kufunguliwa kwa tawi la Simanjiro kunaifanya NMB kuwa na matawi 121 na mashine za ATM 108. Ngatunga alisema watafunga ATM 25 wiki chache zijazo na hadi kufikia mwisho wa mwaka watakuwa na ATM 180
ati, Simanjiro

Back
Top Bottom