Msichana wangu wa kazi kakutwa na VVU

Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,663
2,000
Habari wakuu, nina miez miwil toka nimchukue huyu binti wa kazi ili anilelee mtoto wangu mdogo, ila toka kafika ni mtu ambaye homa hazimuishi kuumwa kila siku....

juzi nikampeleka marie stopes, dr akanishauri nimpime na kipimo kikubwa. Majibu yakatoka kaathirika nililia mno kwanza sikuamin!!! nilimuhurumia ndiyo kwanza ana miaka 14, hata akili zake bado za kitoto.....jana nikachukua watoto na mdada mwingine ambae nipo nae muda mrefu nikawapima wapo salama.

Nilichokifanya nilimficha majibu, nikamuambia umekutwa na typhoid tu maana alikua nayo kweli, ninawaza sana je nimrudishe kwao,? Angekua ndugu yangu ningemrudisha?
Nafikiria risk kwa watoto wangu hasa haka kadogo yaan sielewi, naomba Mungu anisaidie niweze kufanya maamuzi sahihi.
 
Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,663
2,000
Labda kazaliwa nao.. Mrudishe tu.. Kama ni mtu wa kuumwa mara kwa mara hata kazi hatoweza kufanya...
Nahisi kazaliwa nao maana ni katoto yaan hata kuoga mpaka umuambie na ana mwili mdogo, namuonea sana huruma...
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,972
2,000
Fanya maamuzi yatakayo upa moyo wako Amani, lakini UKIMWI ni ugonjwa sugu ambalo linaweza kudhibitiwa iwapo mgonjwa anakunywa dawa kikamilifu na kufuata ushauri wa wataalamu. Kwakuwa hayuko kwenye matibabu na kinga yake ya mwili imeshuka sana, lazima magonjwa nyemelezi yatamuandama.

Atakapoanza matibabu na kinga ya mwili kujirudi anaweza kuendelea na kazi kama kawaida na unaweza kumpa day off siku anazotakiwa kwenda kwenye kitengo.
 
Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,663
2,000
Fanya maamuzi yatakayo upa moyo wako Amani, lakini UKIMWI ni ugonjwa sugu ambao unaweza kudhibitiwa iwapo mgonjwa anakunywa dawa kikamilifu na kufuata ushauri wa wataalamu. Kwakuwa hayuko kwenye matibabu na kinga yake ya mwili imeshuka sana, lazima magonjwa tegemezi yatamuandama.

Atakapoanza matibabu na kinga ya mwili kujirudi anaweza kuendelea na kazi kama kawaida na unaweza kumpa day off siku anazotakiwa kwenda kwenye kitengo.
Asante kwa ushauri mzuri.
 
jje's

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
10,345
2,000
mm pia namwonea huruma, na maamuzi ya kufanya yaani kukushauri nimestaki

ila kiharaka haraka yabidi umrudishe na uwaeleze wazazi wake ulichokikuta, then wape ushauri wa kutumia ARV na wewe usiwaache uwe unawasaidia matumizi kidogo maana hizo dawa zinahitaji lishe na lishe ni hela pia dawa maana inasaidia kubust imunities.

kwa akili yangu finyu sikushauri ubaki nae.

am sorry kama nimekuwa too rude to her.
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,966
2,000
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiii mrudishe leo hii hii: nina ushuhuda wa hilo: ni hivi kuna dada hapa Mwanza aliajiri dada mwenye VVU lakini alikuwa hajui kuwa dada ni mwathirika, ila dada alikuwa anajua. sasa mtoto wa yule dada akawa anaumwa sana, walivyokwenda Bugando kupimwa mtoto akakutwa ana ngoma lakini wazazi wote hawana, walivyobana dada akasema ukweli kuwa kuna siku alikuwa anakata kucha akawa amejikata na mtoto akachezea ule wembe akajikata!
 
Niliweka thread hapa juu ya umuhimu wa kucheki afya za wadada na wakaka wa kazi kabla ya ajira.
 
Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,663
2,000
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiii mrudishe leo hii hii: nina ushuhuda wa hilo: ni hivi kuna dada hapa Mwanza aliajiri dada mwenye VVU lakini alikuwa hajui kuwa dada ni mwathirika, ila dada alikuwa anajua. sasa mtoto wa yule dada akawa anaumwa sana, walivyokwenda Bugando kupimwa mtoto akakutwa ana ngoma lakini wazazi wote hawana, walivyobana dada akasema ukweli kuwa kuna siku alikuwa anakata kucha akawa amejikata na mtoto akachezea ule wembe akajikata!
Ili ndiyo lipo kichwani mwangu la kumrudisha ila namuonea huruma nikiwaza maisha ya kwao.....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom