Msichana wangu wa kazi kakutwa na VVU

Wewe unatakiwa ufunguliwe mashitaka ya kumfanyisha kazi mtoto mdogo wakati anatakiwa awe shule pili unatakiwa ushitakiwe kwa kumfanya kitega uchumi kwa kumuuza kwa wanaume mpaka amepata ugonjwa, serikali na wanaoshughulika na haki za watoto kuna mteja wenu hapa
Kwa meseji yako hii nimeamini JF kuna vichaa, nimuuze kwa wanaume?? yesu wangu!! Umenisikitisha anyway ni mawazo yako sikupingi!! Ubarikiwe!!
 
Kwa meseji yako hii nimeamini JF kuna vichaa, nimuuze kwa wanaume?? yesu wangu!! Umenisikitisha anyway ni mawazo yako sikupingi!! Ubarikiwe!!
Kichaa ameongea maneno mpaka umepanic,we subiri lazima useme ukweli tu, unafanyisha watoto wa watu udanguro
 
Habari wakuu, nina miez miwil toka nimchukue huyu binti wa kazi ili anilelee mtoto wangu mdogo, ila toka kafika ni mtu ambaye homa hazimuishi kuumwa kila siku....

juzi nikampeleka marie stopes, dr akanishauri nimpime na kipimo kikubwa. Majibu yakatoka kaathirika nililia mno kwanza sikuamin!!! nilimuhurumia ndiyo kwanza ana miaka 14, hata akili zake bado za kitoto.....jana nikachukua watoto na mdada mwingine ambae nipo nae muda mrefu nikawapima wapo salama.

Nilichokifanya nilimficha majibu, nikamuambia umekutwa na typhoid tu maana alikua nayo kweli, ninawaza sana je nimrudishe kwao,? Angekua ndugu yangu ningemrudisha?
Nafikiria risk kwa watoto wangu hasa haka kadogo yaan sielewi, naomba Mungu anisaidie niweze kufanya maamuzi sahihi.
Usisahau kumpima na mumeo
 
Kapima ni mzima, una lingine??
Ni tahadhari tu nilikuwa nakupa, kama kapima na yupo Salama ni kheri mkuu.Jingine labda nikushauri huyo dada umrudishe tu kwao maana wewe na mumeo munaweza kuishi kwa uangalifu lakini vipi kuhusu watoto? Mtoto hatajali kukatia kucha kiwembe alichotoka tumia dada
 
Sawa
 
Habari wakuu, nina miez miwil toka nimchukue huyu binti wa kazi ili anilelee mtoto wangu mdogo, ila toka kafika ni mtu ambaye homa hazimuishi kuumwa kila siku....

juzi nikampeleka marie stopes, dr akanishauri nimpime na kipimo kikubwa. Majibu yakatoka kaathirika nililia mno kwanza sikuamin!!! nilimuhurumia ndiyo kwanza ana miaka 14, hata akili zake bado za kitoto.....jana nikachukua watoto na mdada mwingine ambae nipo nae muda mrefu nikawapima wapo salama.

Nilichokifanya nilimficha majibu, nikamuambia umekutwa na typhoid tu maana alikua nayo kweli, ninawaza sana je nimrudishe kwao,? Angekua ndugu yangu ningemrudisha?
Nafikiria risk kwa watoto wangu hasa haka kadogo yaan sielewi, naomba Mungu anisaidie niweze kufanya maamuzi sahihi.
Usianze kumuhudumia kimya kimya tafuta mazazi wake au mlezi( uliko mtoa ) wajulishe kuhusu hilo na mbinu za kukabiliana nalo ili unapo lishughulikia km umehiyari basi ndugu walijue tatizo lake endapo lolote litatokea,

Lakin pia kuhusu yeye kupata tatizo hilo naweza sema labda kazaliwa nalo lakin pia huenda kalipata kwa njia ya ngono, hivi vitoto vya siku hizi vina anzishwa mapenzi vingali vidogo sana na ukikaona waweza dhan kabikra maana hata tumatiti hatupo lakin ukisikia mambo kanayo yafanya waweza pigwa butwaa, mf.vibint vya mikoa hii,mtwara,mwanza,tanga,songea,lindi, na mkoa wa arusha ukanda wa maasai, kwa sehemu kubwa mikoa hiyo vitoto vingi sana vinaanza kufanyishwa ngono vingali vidogo sana tena vinafanya na mibaba mijitu mizima.
 
Nahisi kazaliwa nao maana ni katoto yaan hata kuoga mpaka umuambie na ana mwili mdogo, namuonea sana huruma...
Mungu akubariki kwa moyo wa huruma mm nakushauri tafuta binti mwingine adili na watoto wako alafu yeye msaidie kumuanzishiaa dawa zao msaidie Mungu atakubariki
 
Back
Top Bottom