Msichana wa ndani (Housegirl) anatafutwa

Serena

Senior Member
Apr 4, 2014
124
125
Msichana wa kazi anatafutwa hapa Dar es Salaam. Anaweza kutoka Mikoani pia, cha msingi awe na nia thabiti ya kufanya kazi zake kwa ufanisi na kwa hiari siku zote bila kushurutishwa. Suala la yeye kuja Dar kama anatoka mkoani linaongeleka na linawezekana. Ningependa awe Mkristo na hasa wa dhehebu la SDA kama atapatikana. Hatahivyo, hata wakristo wa madhehebu mengine pia wanapewa kipaumbele. Kwa upande wa ndugu zetu Waislamu, ningependa asiwe wa wale wenye imani kali au awe na background ya familia yenye imani kali. Familia yangu ni ya watu wanne, i.e. Baba, Mama, na watoto wawili wa umri wa kwenda shule ya msingi. Sifa zingine ni:
1. Asiwe na background ya mambo ya uchawi kwenye familia yake.
2. Awe msafi wa muonekano (nguo na mwili) na pia apende kuona nyumba inakuwa safi mara zote.
3. Awe tayari kutimiza majukumu yake kikamilifu bila kushurutishwa.
4. Asiwe na kiburi na dharau.
5. Awe na upendo kwa watoto na kwa watu wote.
6. Awe na nidhamu.
7. Asiwe na magonjwa ya kurithi kama Kifafa, n.k.. Asiwe pia muhathirika wa Ukimwi. Hapa ni kwamba awe na afya nzuri, asiwe na magonjwa ya kudumu.
8. Awe tayari kutufahamisha kuhusu familia yake na tufahamu familia yake.
9. Asiwe mama mtu mzima na wala asiwe na mtoto.
10. n.k.

Offer yangu:
1. Mshahara wa TZS 50,000/= kwa mwezi. Mshahara unaweza kuongezeka ikiwa atatimiza majukumu yake ipasavyo na kuzingatia sifa hizo hapo juu (namba 1 hadi 8). Mshahara wake atalipwa kila mwisho wa mwezi bila kukosa.
2. Matibabu yake kwa kipindi chote anachokaa kwangu.
3. Chakula na Malazi ni kwangu kwa kipindi chote atakaachokaa kwangu.
4. Atakaa kwa amani sana cha msingi masharti hapo juu.
5. Barashishi zingine kutegemeana na mafanikio ndani ya nyumba.

Kwa yeyote yule mwenye uhitaji, au kama kuna mtu unamfahamu tafadhali mwambie awasiliane nami kupitia pm hapa Jamii Forums au kwa njia ya mail: lindinachingwea@gmail.com

Natanguliza shukrani.
 
ninao wengi sana... tena ni waaminifu coz hizo ndo kazi zangu.. fanya kunicheck pm nikupatie hadi picha zao uchague
 
Hiyo No. 7 imekaa vyema. Unataka na kuntafuna nini?
 
duuu masharti kibao utafikiri unamlima 200000
Halafu SDA hatuna Habari hizo, yoyote atakaye kuja atakuwa mwanafamilia, zaidi munatakiwa mumuhubirie mpaka aelewe abatizwe,zaidi kama kweli u msabato hebu huo mshahara ulio offer uongeze walau 80000 hiyo 50000 yakitambo sana
 
ninao wengi sana... tena ni waaminifu coz hizo ndo kazi zangu.. fanya kunicheck pm nikupatie hadi picha zao uchague
Kweli au magumashi maana hizi deals zimekuwa nyingi sikuhizi na za kisanii unatoa pesa anasepa nayo
 
uhakika kaka.. hata ukihitaji kitambulosho cha uraia utapatiwa.. hiyo ndio kazi inayoniweka mjini
 
Bado napokea maombi.

Mshahara wako ni wa Kitumwa.

Shame on you.

Naomba serikali ya Dr. Magufuli iweke sheria ya kuwalipa wafanyakazi wote wa nyumbani kima cha chini.

Mnaonea wanyonge.
 
Inaonekana huelewi nini maana ya matumizi. Kwa mfano ; nikimlipa 150,000 au 200,000 kwa mwezi halafu apange chumba, alipie maji na umeme, anunue chakula, sabuni, alipie usafiri wa kuja kazini na kurudi, akiugua ajilipie, anunue mahitaji ya nyumba kama godoro, kitanda, nk. Hivi, kwa hesabu zako unafikiri mwisho wa mwezi atabaki na shilingi ngapi katika huo mshahara wa 150,000 au 200,000 atakuwa amebaki na shilingi ngapi??? wewe ni aina ya mtu unayeangalia gross bila kuangalia uhalisia wa matumizi ya hicho kiwango unachoongelea. Wewe kama kwako ni ngumu , nenda katafute kazi kwingine. Mimi naelewa ninachoandika hapa na ndiyo maana kuna nafasi ya malipo kuongezeka based on utendaji wake na tabia kwa ujumla. Kwa taarifa yako naweza kumlipa hiyo pesa unayowaza kwa kuangalia figure bila kujali uhalisia na ninakuhakikishia kwamba huyu mtu hataweza kusevu hata 20,000 mwisho wa mwezi tofauti na kwangu atakapopokea 50,000 cash mwisho wa mwezi. Pole sana.
 
Kiongozi hiyo namba 7 haijatulia sana, mbona wapo wahathirika wa ukimwi na wanafanya kazi vizuri tu au unataka kumfanyeje house girl wako?
 
Wewe unaonyesha unadharau wafanyakazi wa ndani ndio maana hata wanaokujua wameshindwa kukusaidia kupata hadi ukaja humu.

Na hayo unayotaka na kulea watoto juu umenichekesha sana, unataka first class service ongeza pesa. Wanakuja na clasa siku hizi hiyo bei ndogo ya kibahili kwa ulivyojiandika.
 
Inaonekana huelewi nini maana ya matumizi. Kwa mfano ; nikimlipa 150,000 au 200,000 kwa mwezi halafu apange chumba, alipie maji na umeme, anunue chakula, sabuni, alipie usafiri wa kuja kazini na kurudi, akiugua ajilipie, anunue mahitaji ya nyumba kama godoro, kitanda, nk. Hivi, kwa hesabu zako unafikiri mwisho wa mwezi atabaki na shilingi ngapi katika huo mshahara wa 150,000 au 200,000 atakuwa amebaki na shilingi ngapi??? wewe ni aina ya mtu unayeangalia gross bila kuangalia uhalisia wa matumizi ya hicho kiwango
ww mbuzi nini hapo umeandika nn?? Mshahara wa mfanya kazi wa ndani kima cha chini ni 80 elfu!! Halafu inaonekana una dharau sana tafuta mmeo afanye Hizo kazi!! nataman ningekujua nikupasue huo ubongo wako niwape mbua wangu wale
 
ahsante kwa tusi na kila la kheri. kosa sio lako, bali kosa ni upeo wako na malezi uliyopewa.
 
Inaonekana huelewi nini maana ya matumizi. Kwa mfano ; nikimlipa 150,000 au 200,000 kwa mwezi halafu apange chumba, alipie maji na umeme, anunue chakula, sabuni, alipie usafiri wa kuja kazini na kurudi, akiugua ajilipie, anunue mahitaji ya nyumba kama godoro, kitanda, nk. Hivi, kwa hesabu zako unafikiri mwisho wa mwezi atabaki na shilingi ngapi katika huo mshahara wa 150,000 au 200,000 atakuwa amebaki na shilingi ngapi??? wewe ni aina ya mtu unayeangalia gross bila kuangalia uhalisia wa matumizi ya hicho kiwango unachoongelea. Wewe kama kwako ni ngumu , nenda katafute kazi kwingine. Mimi naelewa ninachoandika hapa na ndiyo maana kuna nafasi ya malipo kuongezeka based on utendaji wake na tabia kwa ujumla. Kwa taarifa yako naweza kumlipa hiyo pesa unayowaza kwa kuangalia figure bila kujali uhalisia na ninakuhakikishia kwamba huyu mtu hataweza kusevu hata 20,000 mwisho wa mwezi tofauti na kwangu atakapopokea 50,000 cash mwisho wa mwezi. Pole sana.

Bado nasema 50,000 ni mshahara wa kitumwa.

Huwezi pia kumpangia maisha ya mtu, mpe mshahara unayoweza kumudu maisha yake.

Hao wanaolala nyumbani ni watumwa hasa! Mnawafanyisha kazi bila mapumziko kisa mmempa chumba cha kulala na chakula.

Kama unaheshemu haki ya binadamu na si mnyonyaji wa wanyonge, huwezi kumpa mshahara mdogo hivi mfanyakazi wa nyumbani.
 
Mkuu @serena,masharti yote hayo kwa mshahara huo? Jisahihishe. Halafu,mambo ya UKIMWI si ya kuyatangaza hivyo. Waweza kujifanyia taratibu za vipimo mwenyewe. Tena,uchawi utaujuaje ili uridhike?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom