Msichana wa miaka 10 kutolewa mimba

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Msichana wa miaka 10 aliyebakwa ameruhusiwa kutolewa mimba hiyo.

Madaktari nchini India walikubali ombi la msichana huyo mkazi wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India.

Dk Ashok Chauhan aliiambia BBC kuwa hatua hiyo sasa inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano iliyopita baada ya kubakwa na baba wa kambo ambaye hata hivyo amekamatwa.

Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba baada ya wiki 20, bila ya idhini ya madaktari kwa kuwa huweka maisha ya mwanamke hatarini.

Uamuzi wa kumruhusu msichana huyo kutoa mimba ulichukuliwa baada ya mahakama kuwaambia madaktari kuwa itakubali.

Idadi kubwa ya watoto wadogo hubakwa nchini India.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom