Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Naam wapendwa,,, baada ya kalikizo kangu ka machungu nimerejea rasmi katika kijiji changu,,,, Moshi. Siku iliyofuta tu napata sms toka kwa mtu nisiyemfahamu anaomba kuniona,,, nilisita kidogo lakini nikasema sina budi kumwona. Anafika ofisini kwangu mida ya saa 5 asubuhi. Ni binti mdogo wa miaka kama 18 au 19 hivi. Ananisalimu anajitambulisha kisha ananielezea shida yake.
Binti huyu yupo kidato cha sita MUKONO HIGH SCHOOL UGANDA. Alipelekwa huko na mama yake na kwa sasa ameshindwa kurejea shule kwa kuwa mama yake ni mgonjwa na hivyo hawezi kuendelea na shule maana anatakiwa alipe ada ya takribani dola 400. Hivyo ananiomba nimsaidie. Namuuliza alipataje jina na namba yangu ya simu,,, anajibu kuwa aliwahi kunisikia katika kipindi fulani cha redio kuhusu masuala ya elimu. Well,,, ni kweli niliwahi kuchukua vijana ambao niliwasaidia na kwa sasa wengi wao ama wako vyuoni ama wamemaliza kidato cha nne na wanaedelea form 5. Nilikuwa na wadhamini fulani huko nyuma waliokuwa wananisaidia kuwalipia,,, lakini kwa sasa hawa waliobakia (ninao watoto 4 ninaowasaidia) ninajinyima na kutoa fungu mfukoni mwangu. Sina msaada wo wote kwa sasa.
Ombi la kwenu wana JF, ni taasisi gani ambayo naweza kuwasiliana nayo ili imsaidie huyu binti. Kwangu anaonekana kama ana kiu ya elimu. Na hata kama sio lazima arudi Uganda basi asidiweje ili atimize hiyo kiu yake.
Tushauriane na tuone tutamsaidiaje.
Nwatakia weekend njema