Msichana aomba fedha za ada mitaani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAFUNZI wa Shule ya sekondari Ntare, wilayani Karagwe, Swabilath Hussein (17),amesafiri hadi mjini Bukoba na kuanza kuzunguka katika mitaa mbalimbali akidai anatafuta fedha ya kukidhi mahitaji ya shule pamoja karo.

Akihojiwa na Mwananchi jana , binti huyo ambaye anaingia kidato cha pili alisema aliruhusiwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza baada ya bibi yake kuomba apewe muda wa kumtafutia mahitaji wakati akiendelea na shule.

Hata hivyo bibi yake aliyemtaja kwa jina moja la Zainabu alishindwa kupata mahitaji aliyoahidi na kuwa ameambiwa hataruhusiwa kuendelea na masomo kwani ana deni la mwaka uliopita na bibi yake amemwambia aache masomo.

Kwa mujibu wa maelezo yake binti huyo amepata hifadhi ya muda kwa mmoja wa wasamalia wema eneo la Kashenyi mjini hapa na kudai kwa zaidi ya wiki moja anazunguka mitaani na ofisi mbalimbali akitafuta zaidi ya Shy 300,000 ingawa hajapata msaada wowote.

"Napenda kuendelea na masomo nisipopata mfadhili sitarudi tena Karagwe kule hakuna mtu wa kunisaidia, nitatafuta hata kazi za ndani hapa mjini'"alisema Swabilath kwa masikitiko

Pia mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Nusuru kilichoko Kata ya Kashai, Khadija Khalphan aliithibitishia Mwananchi kuwa binti huyo alilelewa kituoni hapo baada ya wazazi wake wote kufariki na alipofika darasa la sita shule ya msingi Kashai mmoja wa watu waliodai ni ndugu yake alimchukua.



Baada ya kuhamishwa binti huyo aliendelea na masomo katika shule ya msingi Muleba iliyopo Kata ya Rwabwele wilayani Karagwe na baadaye kufaulu mtihani na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shule ya Sekondari Ntare.

Pia kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mwaka jana, Fabian Massawe tatizo la kukithiri kwa mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani huo lilichangiwa pia na wasichana kushindwa kuhimili vishawishi pale wanapokosa mahitaji ya shule.
 
kilimasera asante sana,sasa hii habari in case one wants to help verifying na contacts za kumsaidia tunafanya vipi?
 
Back
Top Bottom