Habari wakuu,
Vijana wanaume jifunze kitu hapa, yamkini hata na wewe siku yakakutokea, haijalishi hata kama umewahi kuona mkasa kama huu we tulia tu, wengine watajifunza.Hii ni serious ilimtokea kaka yangu. alimpenda mdada miaka michache iliyopita, alimpenda na dada akasema pia
Anampenda walipendana sana kaka yangu alijitoa kwa kila nanma kwa huyu dada, ambaye kwao ni kijijini huko Kigoma,siku moja yule binti akasafiri kwenda kwao kwa lengo tu kuwaambia wazazi rasmi zaidi ili mipango ianze kuelekea ndoa.
Kufika kwao sijui yule binti ilikuaje, gafla kamkana my kaka kabisa na live akasema sikutaki tena kaka yangu akabembeleza sana hadi akakata tamaa, wazazi wa binti ndio walikuwa chanzo cha haya japo zawadi zote alizopewa
binti awapelekee wazazi walizipokea.
Nikamwambia kaka achana nae na ukubali ukweli unaouona ndio hivyo. akatulia na maisha yakaendelea. baada ya kama mwaka hivi yule binti alikuja kwa spidi kali sana akiomba radhi, jamani wakaka hapa ndio pa kujifunza msiwe wepesi sana kurudiana na binti katika mazingira kama haya, chunguza kwa undani kwanza.
Nilimwambia kaka msamehe ila usimrudie, akaelewa, baada ya muda tukajua kumbe yule binti kwao wachawi noma, kaka alishukuru sana. akatulia katika maombi na Mungu akampatia mke wa ukweli ana 6 yrs katika ndoa na maisha ya furaha.
Binti naye akaolewa na katika harusi tulienda maana tulialikwa nakumbuka nilikaa siti moja na kaka akimuangalia binti ndani ya shela, badae binti mimba zikawa zinaharibika tukapata tetesi kuwa bibi
anachuka watoto kafara.
Wakaka kuweni na maamuzi ya moja kwa moja pindi ufanyapo maamuzi hasa katika hili suala la kuoa, binti akikukataa kwa jeuri akirudi usiwe mwepesi kumpokea,si kwamba nawaponda wanawake wenzangu, no ila unatakiwa kuwa mwangalifu tu.
Kinyume chake kwa wanawake.Mungu awabariki na kwa wale wanaotafuta wenza wa maisha (sio michepuko) nawatakia mafanikio mema muwaone wa kwenu na si wa rafiki zenu.