Msichana aliye karibu nami chuoni, hataki tuwe na mahusiano ya kipamenzi

martial jb

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
864
1,456
Habari wakuu,

Mimi ni mwanachuo, na ni kijana wa umri wa wastani tu. Nilikutana na msichana mrembo tu hapa chuoni. Kiukweli tulianza kuwa marafiki na most of the times urafiki wetu uliunganishwa na masomo kwani tunasoma kozi moja na pia tupo class moja. Mara nyingi nimekuwa kama mwalimu wake kwani humfundisha vitu vingi ambavyo class huwa haelewi na pia huwa ana appreciate sana bond yetu.

Kiukweli sikupanga kuwa nae kwenye mahusiano na msichana huyu , but alikuwa akionyesha sana dalili za kimahusiano kwangu. Namaanisha zile dalili za mtoto wa kike kumpenda mwanaume.

Ilifikia hatua nikaanza kupendezwa nae kwa ukaribu wake, upendo wake, na uhusiano wake kwangu. Nilijaribu kuongea na baadhi ya watu kuhusiana na situation inayoendelea kati yangu me na yeye, most of them waliniambia kuwa kwa dalili anazoonyesha kwangu ni kudhihirisha mapenzi yake kwangu.

Basi niliamua kumtongoza kwani hata mimi nilishampenda tayari. Sasa katika kumtongoza first time alidai anapendezwa zaidi na urafiki wetu kuliko uhusiano wa kimapenzi. Sikumuelewa kwa nini alijibu vile coz alijionesha kuwa ni mtu mwenye mapenzi na mimi.

Licha ya jibu hilo, alikuwa ni mtu aliyeniruhusu kupapasa mwili wake na kumpiga mabusu. Hili pia lilinishangaza sana. Ila baada ya kuendelea kufosi sana baadae akaniambia kuwa anataka tusome kwanza mapenzi tufanye baada ya kuhitimu masomo yetu ya chuo. Baada ya kumaliza chuo ni kama miaka 2 mbele.

Sasa najiuliza hivi kweli elimu ya chuo inaweza ikawa ni sababu ya mimi na yeye kutokuwa pamoja kwa sasa!!? Na pia inawezekana vipi kwa kipindi chote tuwe marafiki then tukimaliza ndo tuanze moja kwenye mahusiano!? Na kwa nini anaruhusu nimshike mwilini kama hataki mahusiano!!??

Naomba uzoefu wenu wakuu kuhusu huyu binti, maana me na mapenzi ya kweli na yeye ila sijui yeye mwenzangu maana sababu zake haziniingii akilini.
 
Acha mazoea ya kufanya urafiki na wanawake utakosa vingi.

Ukishakua na urafiki na mwanamke anakuweka kundi moja na mashosti zake. Siku ukimtongoza hakukubalii ng'oo labda upite ki-Mockery!🏃🏃🏃

70% Wanaume waliotongoza marafiki zao wa kike hawakukubaliwa.
#Usirudie kufanya urafiki
 
Soma, acha umalaya
Hapana hapana, tumetofautiana uelewa mkuu. Elimu ya chuo ni elimu ya juu na ni ya kujitegemea kaka. Haimaanishi nisiwe kwenye mahusiano kisa nasoma na haimaanishi nisifanye mambo mengine kisa nasoma.
Kuna watu wameoa na wapo chuo na kuna watu wanaendesha maisha yao na bado nipo nao chuo. Hiyo inaonyesha jinsi gani Elimu ya chuo kutonizuia kufanya mambo mengine.
 
Acha mazoea ya kufanya urafiki na wanawake utakosa vingi.

Ukishakua na urafiki na mwanamke anakuweka kundi moja na mashosti zake. Siku ukimtongoza hakukubalii ng'oo labda upite ki-Mockery!

70% Wanaume waliotongoza marafiki zao wa kike hawakukubaliwa.
#Usirudie kufanya urafiki
Mkuu hujanielewa mkuu.
Hakuwa rafiki yangu but alikuwa mtu wa karibu yangu tu.
Na sidhani tulikuwa karibu kiasi cha yeye kunikataa mimi au kutaka niwe rafiki yake.

Hapana kaka, nahitaji ushauri wako mzuri kaka.
Wewe ni mtu mkubwa hapa JF
 
Back
Top Bottom