Msichana ajirusha kutoka ghorofani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msichana ajirusha kutoka ghorofani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 31, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 25 na 30 amekufa baada ya kupasuka kichwa ikidaiwa kuwa huenda kifo chake kimetokana na kurushwa au kujirusha kutoka ghorofa ya kwanza ya jengo la Benjamin Mkapa lililopo mtaa wa Azikiwe Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na baadhi ya wafanyakazi wa jengo hilo waliozungumza na HABARILEO ambao hata hivyo hawakupenda kutaja majina yao na kazi zao, tukio hilo lilitokea jana saa tisa alfajiri.

  Walidai kuwa mwanamke huyo kabla ya kifo hicho alionekana akiwa na rafiki yake wa kiume wakinywa pombe katika baa ya Savannah, ghorofa ya tatu ya jengo hilo na kisha rafiki yake huyo aliondoka bila kulipa bili za vinywaji walivyokunywa, huku akimwacha mahali hapo.

  Waliendelea kusimulia kuwa baada ya rafiki kuondoka bila kulipa, mwanamke huyo aliondoka pia huku akionekana kumfuatilia na baada ya muda baadhi ya watu waligundua maiti nje sakafuni akitokwa damu nyingi.

  “Hatujui kama alijirusha mwenyewe au alirushwa kutoka juu, kwa sababu hakuna aliyeshuhudia tukio hilo, pia tunashindwa kukupa taarifa ipasavyo kwa kuwa sisi si wazungumzaji wa suala hilo,” waliongeza mashuhuda hao.

  Akithibitisha tukio hilo jana, Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Ilala, Duwan Dila, alisema Polisi ilifika na kuuchukua mwili huo mapema alfajiri kwa ajili ya uchunguzi na taarifa zaidi za kifo chake zitatolewa baada ya uchunguzi.

  “Tumewasiliana na uongozi wa jengo hilo ili watupe picha za tukio hilo walizozipata kutoka kamera zao za ndani ya jengo hilo ili tujue undani wa kifo chake, kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” aliongeza Dila.

  Hata hivyo uchunguzi zaidi ulibaini kuwa baada ya mwili huo kupekuliwa, ulikutwa na kondomu mbili ambazo hazijatumika, sigara tatu aina ya Marlboro na mswaki na dawa ya meno.

  Jengo la Mkapa Towers liko mkabala na ofisi za Posta Mpya na ndilo linaloonekana kuwa refu kuliko majengo mengine ya Dar es Salaam likiwa na zaidi ya ghorofa 20 na awali lilijulikana
  kama Mafuta House.

  Ndani ya jengo hilo pamoja na kuwa na ofisi za Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) pia ndimo ilimo hoteli mashuhuri ya City Paradise inayomiliki mgahawa huo ambao wawili hao walikuwa wakistarehe usiku wa jana.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sna aisee pumzika kwa amani dada wa watu, sheria ichukue mkondo wake jamni
   
 3. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Pumzika kwa amani japo kifo chako kimeacha maswali mengi kwetu tuliobaki.
  Kama Vile zile Condomu zilikuwa zako kwaajili ya kujikinga?
  Mswaki ulikuwa ni wanini wakati huo?
  Je ulijitupa mwenyewe au ulitupwa?
  Ulitupwa na nani? na kwasababu gani?
  Je aliyekuwa akinywa na wewe na kuacha kulipa bili ni nani yako?

  Pumzika kwa Amani haya maswali ni yetu sisi na wewe Unayako pia ya kujibu huko .
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  RIP! Ameshindwa kuvumilia...maskini siku mbili tu angeuona mwaka mpya!
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  alijua mwaka mpya kwake utaendela kuwa kwenye kalenda tu bali yeye ataendelea kutembea na kondomu+mswaki+ dawa. Nadhani huyu jamaa aliyekuwa naye alimkwepulia ka akiba kake akayoyoma..........
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  fundisho kwa wengi!
  RIP
   
 7. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Zipuwawa

  Huyu dada hakutaka shida ya kutafuta duka la kununa mswaki au dawa asubuhi, Mara nyingi hulala pale usingizi unakomkuta, RIP sister
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Uchunguzi yakinifu ufanyike ili kujua chanzo cha ajari hiyo!!
   
 9. B

  Biro JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 331
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Sitaki kumhukumu ila machangu wengi wanatembea na boot hajui atakayekutana naye anayo au la, na pia anatembea na mswaki kwa vile hajui kutakucha akiwa wapi, ila nayo ni style ya maisha.
   
 10. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Savannah Lounge haimilikiwi tena na Paradise Hotel... Ipo chini ya mmiliki mpya...
   
Loading...