Msiba wa kitaifa ni wa taifa na Vyama vyote vya Siasa

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Na: Sauti ya Mdodomia
24/07/2020

Nimeshangazwa na utovu wa nidhamu ambao umefanyika na bila shaka utaendelea kufanywa na baadhi ya watu nchini, na sio wengine ila ni hawa viongozi wa vyama baadhi vya upinzani.

Leo Taifa limepata pigo kubwa mno! Na mara ya mwisho kabla ya pigo hili la sasa, ni msiba ule wa Baba wa taifa Mwl. JK Nyerere mnamo miaka 21 iliyokwishapita, na msiba ule wa Sheikh AA Karume miaka takribani 48 iliyopita. Ndio kusema ndani ya Miaka 48 Tanzania na watanzania wanaomboleza kifo Cha Mzee wetu, Rais wetu mstaafu, Kiongozi wetu wa nchi mstaafu na Mkuu wetu wa serikali mstaafu na pia Amiri Jeshi Mkuu wetu mstaafu ndugu Benjamin Mkapa, Buriani Mzee wetu!

Tunafahamu misiba imekuwa ikitokea kila siku na watanzania wengi wanafariki kila siku, hii haina maana kwamba taifa haitambui michango yao kama wananchi kwenye nchi yao, la hasha! Michango yao inatambuliwa na inathaminiwa sana, suala li wazi.... Mzee wetu Mkapa nje ya majukumu na madaraka aliyowahi kuyashika pia alikuwa ni mtanzania mwenzetu ambaye ameshariki kwa ukamilifu katika ujenzi wa nnchi yetu Tanzania.

Mzee Mkapa atunaye tena katika nchi na Dunia pia, ametangulia. Hatutakuwa naye tena kama ambavyo alituacha mzee Karume na Mzee wetu Nyerere. Hili ni pigo kubwa. Tunafahamu kawaida ya maaskari vitani, ni kweli wanakufa maaskari wengi katika uwanja wa medani lakini kiongozi anawajibika katika kujenga hali na morali wa kupigana vita bila kurudi nyuma, na kuwaonesha njia ya kumshinda adui kwa waredi mkubwa mno.

Na hiyo ndio kazi hasa ya kiongozi katika mapambano ya Vita, na kwa hakika hali ni tofauti inapotokea kiongozi anauawa. Wapiganaji wote wanapoa wanpoteza hali na morali wa kupigana vita vyenyewe. Ndio kusema kuna mambo mengi ya muhimu na yenye tija kwa kiongozi kwa wale anaowaongoza na kusema kweli ni mwenye kujenga umoja hali na morali wa kufanya kazi kwa juhudi na weredi kwa watu wake.

Kwa mujibu wa sheria zetu za nchi, Rais ni kiongozi mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu. Kwa jinsi hiyo Rais ni mwenye dhamana ya kuongoza watu wote wa kada zote wa vyama vyote na dini zote, Rais ndiye mlezi wa katiba. Katiba ambayo inaowajibu wa kuvilea na kuvisimamia vyama vya siasa ni katiba hii ambayo imetenganisha mambo ya siasa na mambo ya dini. Kwa hiyo Rais ni mlezi wa katiba na mlezi wa vyama vya siasa vilevile. Na kwa kuwa moja ya tamaduni za nchi nyingi Duniani hutumia nusu mlingoti kwenye bendera za nchi na za vyama vya siasa kama ishara ya kuomboleza msiba mkubwa ndani ya nchi.

Sasa kumekuwa na tabia ya ovyo ovyo kwa baadhi ya vyama vya siasa na hapa niseme wazi ni CHADEMA na ACT vimekuwa ni vyama vya ajabu, hata kufikiri wao si sehemu ya nchi ya Tanzania. Nimeshangaa utovu huu wa nidhamu, wao wameacha kutoomboleza msiba wa aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa kabisa wa nchi na ambaye pia ni mlezi wao! Wanafikiri kufanya hivyo ndio kujiweka keleleni katika siasa za nchi, huu ni utovu wa nidhamu. Kuacha kuomboleza msiba wa kiongozi wa nchi ni dharau mbele ya katiba ya nchi na wananchi!

Niseme tu, wajibu wetu kama sehemu ya nchi ni kutambua viongozi wetu kama sehemu muhimu ya alama ya nchi yetu, na huko ndio kutekeleza katiba ya nchi na ndio mwanzo wa kujenga jamii yenye usawa na haki. Lai yangu kwa viongozi wa vyama vya siasa ni lazima watekeleze kwa vitendo ile tamaduni ya nusu mlingoti ikiwa ni sehemu ya kutambua mamlaka ya wananchi hata katika misiba na maombolezo ya viongozi wakuu wa nchi. Rais mstaafu Mkapa alikuwa ni Rais wa nchi pamoja na wananchi ambao wanajiita ni viongozi wa upinzani.

Haijalishi ni CHADEMA, ACT, CUF n.k ni lazima ziweke nusu mlingoti katika bendera zao kama ambavyo CCM imetekeleza.
 
CORONA imewapiga sasa mtakiona cha moto. Huzuni inategemea na aliyekufa kama unauhusiano ama la. Wengine kutokana na ugumu wa maisha wapo hapa City Pub Mwanjelwa wanakula bia. Yaani hakuna hata dalili za kuonyesha kama kuna mtu maarufu wa ccm kafa kwa ugonjwa usiotajwa na hospitali isiyojulikana
 
Uzi umefutwa unaupandisha tena. Huna adabu kwa kutumia msiba wa Mzee Mkapa kujipatia kiki. Yote uliyosema ni uongo na mods sijui wanakustahi nini Kwa jeuri unayowafanyia. Ofisi zote za Chadema tangu jana bendera ziko nusu mlingoti.
FB_IMG_1595649462320.jpg
 
Mkuu, licha ya kuzunguka mno ktk kuzungumzia suala la umuhimu wavbendera kushushwa nusu mlingoti ikiwa kama ishara ya maombolezo ya kitaifa kwa msiba mkubwa uliolipata taifa kwa kutokana na msiba wa Mzee Mkapa. Lakini pia umekwepa kuwagusia viongozi wa Zanzibar waliokwisha kutangulia mbele za haki.

Katika orodha hiyo kumbukizi ya viongozi waliowahi kuongoza Zanzibar, yupo Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Abdul Jumbe, na pia yupo wa awamu ya nne, Mzee Abdulwakil. Viongozi hawa nao ni muhimu kuwataja, hapo ni bila hata ya kuwazungumzia wale waliowahi kuwa makamu wa rais na mawaziri wakuu.
 
Mbona uliwasahau wale waliouliwa na huyu Laanatullahi Mkapa huku Unguja na Pemba yake ?? Au wao si binadamu walistahiki kuuliwa ??

Mwache aende akahukumiwe kwani hapa tulikuwa hatuna mahakama ya kumshitaki .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom