Mshtuko wa ugaidi, 11 wanaswa Mwanza

Mshtuko wa ugaidi, 11 wanaswa Mwanza

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 15 wakiwemo watoto 11 wenye umri wa miaka 10 wakidaiwa kufundishwa ‘ugaidi’ katika nyumba moja iliopo Kishiri nje kidogo ya jiji hilo,

Kabla ya kufika kwenye nyumba waliyokuwemo watuhumiwa, polisi walimkamata kijana mmoja kwenye Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana ambaye alidaiwa kuhusika.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kueleza kuwa, walifanikiwa kuwakamata baada ya taarifa kutoka kwa kijana huyo.

Msangi ameeleza kuwa, baada ya taarifa za kijana huyo ambaye aliyeongozana na polisi hadi katika eneo la tukio, waliwakuta watuhumiwa hao.

Amesema, watuhumiwa hao baada ya kugundua kuwa ni polisi, walirusha bomu moja jambo ambalo liliwasukuma polisi kuanza kujibu mashambulizi kwa kupiga risasi hewani na kuwamuru kujisalimisha.

Kamanda Msangi amedai kuwa, baada ya watu hao kujisalimisha, polisi walianza kufanya ukaguzi katika nyumba hiyo na kufanikiwa kukuta bunduki aina ya SMG na magazine tano zilizokuwa na risasi 150.

Ameeleza kuwa, polisi pia walifanikiwa kukamata vitabu viwili vya Dini ya Kiislamu na kofia moja ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Na kwamba, kitendo hicho amedai kinashabiana na vitendo vya ugaidi na matukio mengine yaliowahi kufanyika jijini humo.

“Kama mtakuwa mnakumbuka vizuri kuna matukio ambayo yalishawahi kutokea hapa Mwanza yakiwemo ya msikitini watu kuchinjwa, na watu wanaodai inaweza ikawa ndio hao wahusika,” amesema Msangi.
 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, akionyesha silaha kwa waandishi wa habari jana zilizokamatwa eneo la Bukaga Kata ya Kishiri Wilaya ya Nyamagana katika moja ya nyumba ya mtuhumiwa wa ujambazi.


MWANZA ni hatari. Ndivyo alivyosema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, baada ya matukio mawili yaliyotokea usiku wa kuamkia jana, likiwamo la nyumba moja kukutwa silaha za kivita, za jadi na watoto 10 waliokuwa wakifundishwa mafunzo yanayoashiria kuwa ni ya kigaidi.

Silaha zilizokutwa katika nyumba hiyo iliyopo Bugaka, Kata ya Kishili jijini Mwanza, ni bunduki aina ya AK 47, mabomu ya kurusha kwa mkono, bunduki aina ya Maker 4, risasi zaidi ya 150, majambia na visu.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili katika mahojiano maalumu, Kamanda Msangi alisema kuwa aliongoza vijana wake kufika katika nyumba hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya watuhumiwa wanaowashikilia kwa matukio mbalimbali, kwamba wafadhili wao wapo Kishili na Buhongwa.

Msangi alisema kutokana na taarifa hizo, aliunda vikosi viwili kufanya operesheni maalumu usiku wa kuamkia jana, kimoja kilikwenda eneo la msitu wa Deo uliopo Buhongwa na kingine Kishili.

Akizungumzia kikosi cha Kishili alichokiongoza, alisema walipofika katika nyumba hiyo waliizingira na watu waliokuwamo ndani wakaanza purukushani za kutaka kujihami ndipo askari walilazimika kufyatua risasi moja kuwatuliza.

Kamanda Msangi alisema wakati wanatafuta namna ya kuingia ndani ya nyumba hiyo iliyo na uzio, kijana mmoja alifanikiwa kuruka ukuta kwa upande wa nyuma na kutoroka, lakini wakafanikiwa kuwadhibiti wenzake zaidi ya 15.

“Baada ya kuwadhibiti na kuingia ndani, tulifanya ukaguzi na kufanikiwa kupata mabomu ya kurusha kwa mkono yaliyokuwa yameandaliwa kwa matumizi, bunduki za kivita aina ya AK 47, magazine tano na kila moja ikiwa na risasi 30, majambia, bunduki ndogo aina ya Maker 4, visu na gari moja ambayo inawezekana ndiyo wanayotumia kufanya doria zao kabla ya kufanya matukio.

“Tulipoingia tumewakuta watoto wadogo 10 waliokuwa wakifundishwa mafunzo maalumu ya namna ya kutumia silaha walizokuwa nazo na namna ya kujilinda na adui, pia kulikuwa na wanaume wanne wakubwa na wanawake wawili ambao inaelezwa ndio watoaji mafunzo kwa watoto hao.


“Katika mahojiano ya awali, tumeelezwa kwamba watu hao wana vikosi katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa, ikiwamo Tabora, Mwanza na Kigoma,” alisema.


Kamanda Msangi alisema wakati wanapambana na watuhumiwa hao, wananchi walijikusanya eneo hilo, wakiwa na nia ya kutaka kuwaua watuhumiwa hao, lakini askari walisimama imara na kufanikiwa kuondoka nao wakiwa hai.

Alisema baada ya kuondoka na watuhumiwa hao, baadaye alipata taarifa kwamba wananchi waliamua kuteketeza nyumba hiyo kwa moto alfajiri ya jana.

WAWILI WAUAWA

Akizungumzia kikosi cha pili kilichokwenda msitu wa Deo, alisema kiliambatana na vijana wanne ambao baadhi yao ni waendesha bodaboda, waliokuwa wakishikiliwa kwa matukio ya hivi karibuni.

Alisema walipofika katika msitu huo, walionyesha silaha zilipo na katika ukaguzi walifanikiwa kupata bunduki moja aina ya SMG, magazine mbili huku moja ikiwa na risasi 15 na nyingine 30, pia walikamata bastola moja.

“Wakati askari hao wakifanya upekuzi katika msitu huo, ghafla watuhumiwa hao walianza purukushani ya kutaka kutoroka, ndipo askari waliwafyatulia risasi na kuwaua wawili.

“Tunaendelea kuwahoji watuhumiwa ili kupata mtandao wote, lakini hapa Mwanza ni hatari, kibaya zaidi vijana hawa wa bodaboda wanajihusisha na vitendo hivi, tunaomba wananchi kuwa makini na kundi hili,” alisema.

Chanzo: Mtanzania
 
Hivi polisi wanaelewa maana ya ugaidi au wanadhani ni kukutwa na kilipuzi tu? Wanajua ni athari gani zinazoweza kuikumba nchi kwa kutamka msamiati wa "ugaidi"?

Mimi nafikiri, kwa kuwa polisi hawana uelewa kuhusu mambo ya hujuma za kigaidi, ni bora wangepigwa marufuku kabisa kutamka hilo neno maana linaweza kuathiri hata shughuli za utalii nchini.
 
Kazi nzuri imefanyika ,pongezi kwa jeshi LA police.
 
Serilikali iwaangalie sana hawa watoto wa mitaani maana hawa watu wanauwezo wa kuwarubuni kirahisi zaidi
 
Hayo ndio majukumu ya Polisi, nashauri waongeze msako dhidi ya magaidi hao.!
 
Ivi ni kweli vijana wawili wanaweza kuwakimbia polisi?kuuwa mumeshauwa lkn ukweli hawakustahiki kuuwawa.jela ipo kwa ajili ya watu kama hao.
 
Kazi nzurii kweli mwanza kwa sasa inatisha tena wanaiba mchana kweupee
 
Eti smg kwa mujibu wa kamanda ni silaha za kivita.
 
Back
Top Bottom