Mshike mshike TRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshike mshike TRA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 17, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280
  Mshike mshike TRA

  na Alfred Lucas
  Tanzania Daima

  HALI ya kutoaminiana imeibuka ndani ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kiasi cha maofisa kutoka makao makuu kuwatuma wakaguzi maalumu waliovamia ofisi moja ya tawi na kufanya ukaguzi wa ghafla mapema wiki iliyopita.
  Hatua hiyo inafuatia wimbi la shaka, linalotokana na kuwepo kwa taarifa za hujuma nzito inayofanywa na mtandao wa baadhi ya wafanyakazi ndani ya mamlaka hiyo nyeti.

  Taarifa za hujuma hizo nzito zinahusu kutolewa kwa leseni batili za magari, yaani 'Road Licence Stickers' katika ofisi ya TRA, tawi la Samora, jijini Dar es Salaam.

  Inadaiwa kwamba wafanyakazi hao wanatengeneza stika hizo na kuwauzia wateja ambao hawana ufahamu mkubwa wa kuweza kubaini tofauti kati ya stika hizo bandia na zile halali.

  Hata hivyo, taarifa kuhusu hujuma hiyo ambayo inadaiwa kuendelea kwa muda sasa, zilifika makao makuu ya TRA na mabosi wa mamlaka hiyo wakachukua uamuzi.

  Uamuzi huo ulihusisha uchunguzi wa ghafla, uliofanywa katika ofisi ambazo watumishi wake wanatuhumiwa kutengeneza nyaraka bandia ukiongozwa na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidus Luoga.

  Kutokana na taarifa hizo, Luoga aliongoza operehseni hiyo ya ghafla Desemba 12 mwaka huu katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo Mtaa wa Samora, Dar es Salaam karibu kabisa na makao makuu ya TRA.

  Operesheni hiyo ilianza majira ya saa 2.30 asubuhi na kusababisha kusimama kwa huduma za kawaida kwa takriban saa mbili, hali iliyozua manung'uniko kutoka kwa wateja ambao walikuwa hawafahamu kilichokuwa kinatokea ndani ya ofisi hizo.

  Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi waliopekuliwa, walilalamika kuwa zoezi hilo liliendeshwa kinyume cha taratibu na kwa kiasi fulani lilisababisha udhalilishaji.

  Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mmoja wa wafanyakazi wa taasisi hiyo, alilalamika upekuzi huo kufanywa na wanaume waliowapekua pia wanawake.

  Alisema kuwa kutojali jinsi katika masuala ya upekuzi ni udhalilishaji.

  Mfanyakazi huyo alisema: "Ilikuwa ni kama vurugu. Tulishitukizwa. Tulisimama kufanya kazi tukidaiwa kufanya hujuma. Cha ajabu ni kwamba hawajakuta lolote kuhusiana na tuhuma zilizotolewa."

  Kadhalika, mmoja wa wateja, alilalamika akihoji: "Sasa kama uongozi wa TRA hauwaamini watumishi wake, itakuwaje kwa sisi wateja?"

  Tanzania Daima lilifanya juhudi kumtafuta Luoga ofisini kwake ili aelezee kwa kina zoezi hilo, lakini halikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa ofisa huyo alikuwa amesafiri kikazi.

  Ilielezwa na wasaidizi wa bosi huyo kwamba, yu safarini mkoani Arusha, anakohudhuria mkutano na alipopigiwa simu yake ya mkononi, hakuipokea.

  Alipohojiwa, Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipa Kodi, Protas Mmanda, alikiri kufanyika kwa ukaguzi huo.

  Alisema ukaguzi huo wa ghafla ulifanywa kutokana na wasiwasi na taarifa zilizoenea kwamba leseni hizo feki ziko nchi nzima.

  "Ni kweli ukaguzi ulifanyika. Lakini hakuna upekuzi uliofanyika kwa kumshika mtu mwili. Ilikuwa ni kila mfanyakazi anafungua kabati, droo yake ya meza. Walifungua wenyeweÂ… hakuna mfanyakazi aliyelazimishwa," alisema Mmanda.

  "Tulikuwa tukikagua document (nyaraka) tu," alisema Mmanda alipohojiwa na Tanzania Daima Ijumaa iliyopita.

  TRA imetangaza mikakati ya hujuma katika ofisi yake ikiweka taratibu za kupambana na kila aina ya hujuma katika ofisi zake Tanzania nzima na inaaminika kuwa operesheni hiyo ni moja ya utekelezaji wa mikakati hiyo.
   
 2. J

  Jafar JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2007
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wachaga hawaaminiani tena ?
   
 3. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hao wakubwa wa TRA ndio namba moja kwa UFISADI wanatishia tu kwani wanaokwepa kodi wote wanawafahamu na wanakula nao.
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Of course wezi huwa hawaaminiani siku zote, hata iweje! Hizo ni tiktak tu kama zilivyo nyingine!
  Naona wakubwa walizidiwa kete, wakaamua kukomaa!
  Tutajua hatima yake tu, sisi ni JF bwana!
   
Loading...