Habari zenu wakuu,
Hivi karibuni kaka yangu ametoka kumfuata mkewe(shemeji yangu) ukweni baada ya kuuza vyombo vya ndani na kutokomea nyumban kwao! Leo hii ninavyoandika huyu mke amefungasha kila aina ya samani iliyomo ndani(sofa+vitanda+meza navingine vingi) kiasi kwamba nyumba imebaki nyeupe pe!
Kisa matatizo ya kifamiliya baina ya kaka na shemeji! Sasa kwa hali hii maendeleo yatapatikana maana kila jamaa akijaribu kujikwamua mke anazuia kwa kuiba na kutokomea nyumbani kwao! Sasa swali ni kwamba jamaa amfuate tena huyu mke au apige chini?
NB: Wana watoto wawili kwa sasa