Mshana Witch project

Mshana Witch project

Nina mchango mkubwa sana kwenye kufisha na kufifisha nyota ya chama pendwa
Nimeroga sana hapo kabla lakini mwaka huu nimeroga mpaka jasho langu likawa linanuka uchawi
Nilijenga vilinge majini
Nikajenga vilinge ardhini
Nikajenga na angali
Nimepandikiza gundu kwenye rangi za chama
Wagombea nikawatupia gundu la kinyesi..mkubwa kabisa nikampiga jini kisirani
Nimeroga wala sijisifu ..nimeroga mpaka uchawi ukanikifu

Malighafi zangu maarufu zilikuwa ni
Maji ya gundu
Maji ya janaba bichi
Damu Chafu
Majani ya mkafiri
Nyota ya nuksi
Kinyesi cha popo/ngozi ya kinyonga
Mizizi ya mti chonganishi

Nikavaa koti la ugaguzi..walipokuja nikawapiga gundu wajumbe wakawaona kama maliwato ya jiji
Nikavaa koti la ulokole walipokuja kwa maombi nikawapiga muhuri wa upofu na kuzima nyota zao...walipojitokeza upenuni wajinadi wakakimbiwa na kuzomewa...

Nimejenga madhabahu za giza nyuani mwao
Nikajenga zingine kondeni
Na zingine kwenye mapito yao..hakuna nilipobakisha...na kila waliporudi kwangu kulalamika nikawaambia wamekosea masharti

Project inaendelea..huu ni mrejesho sehemu ya kwanza...mkiona wanakimbiwa..tambueni kuna miba za nungunungu zimetegwa kila pahala...
Ila Mshana sijui hata nikuweke category ipi, kumbe mpaka kuroga unajua
 
537175.jpg
 

Attachments

  • 537175.jpg
    537175.jpg
    30.4 KB · Views: 18
Kwakuwa Mungu wetu ni mmoja na katika yeye kila goti litapigwa kwakuwa msalaba ndio asili ya mema yote na hapo ndio tunatua mizigo yetu yote ikiwemo ushirikina ndumba na ulozi

hakuna mtu mbaya asiye na mazuri yake wala mzuri asiye na mabaya yake. Wote tunayo aidha tunayafanya kizani au hadharani, kinachojalisha ni kuelewa state uliyopo na kufanya mabadiliko bhasi maana Mungu si kama mwanadamu katika hukumu zake
 
Back
Top Bottom