acha ungese dogo
Ukitaka kujua mshahara wa rais wa nchi muulize maana yeye ndio shahidi, usiwaulize wengine watakudanganya.
Wakuu tukiwa kama waajili wa hawa Viongozi ni shurti na haki yetu kujua malipo yao, hapa naongelea Mishahara yao, Posho zao, Marupurupu na Pension.
Tumejua ya wawakilishi wetu bungeni, na sasa ni hawa viongozi waandamizi wa Serikali.
Tumepiga kelele na kupinga ongezeko la sitting allowance (Posho) za wabunge na nadhani kwa kiasi kikubwa tuko mbioni kufanikiwa sasa ni wakati wa kuangalia malipo na posho za hawa viongozi wengine, hali ya maisha kwa mtanzania wa kawaida ni ngumu huku asilimia kubwa ikiishi chini ya Usd 1 kwa siku.
Mwenye hizi data atuwekee hapa, tuzijue na kuzipitia.
Asalaam
MODs Please msiunganishe thread hii na nyingine yeyote please.