Mshahara wa Rais kaa la moto

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331

Rais Jakaya Kikwete PICHA|MAKTABA
Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Posted Oktoba19 2013 saa 10:8 AM


Dar es Salaam. Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaja hadharani mishahara ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, serikali imekataa kuizungumzia mishahara hiyo.

Msimamo wa Serikali kutotaja mishahara ya viongozi wakuu unatofautiana na utamaduni wa nchi nyingine kama Marekani, Afrika Kusini, Ufaransa na Kenya ambazo mishahara ya wakuu wake huwekwa wazi kwa umma.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema akiwa wilayani Igunga Mkoani Tabora, alisema Rais Kikwete anapokea zaidi ya Sh30 milioni kwa mwezi (sawa na Sh360 milioni kwa mwaka) ikiwa ni marupuru na mshahara kwa mwezi bila kodi, huku Pinda akipokea Sh 26 milioni kwa mwezi.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kiongozi yeyote haruhusiwi kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.

"Kuutaja mshahara wa mtu mwingine ni kinyume cha sheria na kosa, siyo utaratibu. Kwani wewe upo tayari watu waujue mshahara wako?" alihoji.

Aliongeza kuwa ingawa mishahara ya viongozi hao inatokana na kodi za wananchi, sheria ndiyo inayozuia watu kuyataja malipo hayo hadharani na kwamba hayupo tayari kuutaja mshahara wa rais au kiongozi mwingine labda mtu huyo autaje yeye mwenyewe.

"Siwezi kutaja mshahara wa bosi wangu wala wa kwangu mwenyewe. Wewe unaujua mshahara wa Obama (Rais wa Marekani)?" alihoji tena.

Akizungumzia mishahara ya marais wa nchi nyingine duniani kuwekwa wazi, Kombani alisema kila nchi ina utaratibu wake na kwamba Tanzania haijafikia hatua hiyo.

Alipotafutwa kulizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa. Gazeti hili pia liliwasiliana na Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo Ofisi ya Rais Ikulu, Peniel Lyimo ambaye alisema yeye si mhusika. "Masuala yote yanayohusu utumishi yapo Wizara ya Utumishi," alisema Lyimo.

Akianika mshahara wa Waziri Mkuu, Zitto alisema kwamba kiongozi huyo analipwa Sh11.2 milioni kama mbunge, Sh8 milioni kama waziri na Sh7 milioni kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu, hivyo, kumfanya kupokea zaidi ya Sh300 milioni kwa mwaka.

Hata hivyo, Kombani alilionya gazeti hili kuandika taarifa za mishahara ya watu kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bashiru Ally alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kutaja mshahara wake hadharani na kuhoji viongozi wanaotaka mishahara yao isitajwe wanaficha nini.

"Hata wakificha mishahara yao bado wananchi wataona maisha wanayoishi kuwa si safi," alisema. Wanaharakati pia wahoji

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba alisema siyo kosa kwa mtu yeyote kutangaza mshahara wa viongozi wa umma kwa kuwa wanalipwa kutokana na kodi za wananchi.

Aliongeza kuwa kuanzisa sasa atakuwa balozi wa kutangaza mishahara ya viongozi hao, ili kila mwananchi aweze kufahamu kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika nchi nyingine duniani.

"Ninachojua mimi ni kuwa dhana ya mshahara inataka kuwepo na siri baina ya mwajiri na mwajiriwa, lakini si kwa viongozi wa umma ambao wanalipwa na kodi za wananchi. Kuanzia sasa hivi nitakuwa balozi wa kutangaza mishahara ya viongozi hao ili kila mtu ajue," alisema Kibamba.

Katibu Mkuu wa Tanzania Labor Party (TLP), Jeremiah Shelukindo alisema ni vyema kila mtu akaheshimu sheria inayozuia kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwaudhi baadhi ya viongozi wa umma.

"Si vizuri kuingiza siasa kwenye mambo ya mishahara. Siyo mara ya kwanza kusikia watu wakijaribu kutaja mishahara ya watu wengine huko ni kukiuka sheria," alisema.

Naye Mkurugenzi wa asasi ya Sikika, Irenei Kiria alisema umefika wakati ambapo inabidi uanze kufanyika mchakato wa kuzibadili sheria zinazolenga kulinda masilahi ya viongozi wa umma.

"Tunataka kujua viongozi wanalipwa shilingi ngapi na kwa nini wanalipwa kiasi hicho," alisema Kiria

Nchini Marekani, mshahara wa rais unajulikana tangu mwaka 1789 kiongozi wa nchi hiyo alipokuwa analipwa Dola 25,000 kwa mwaka.

Kuanzia 2001 hadi sasa, Rais wa Marekani analipwa Dola 400,000 (Sh 640 milioni) kwa mwaka, sawa na Sh 53.3 milioni kwa mwezi.


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma analipwa Randi 2 ,917 038 sawa na zaidi ya Sh400 milioni za Kitanzania kwa mwaka, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande Sh475 milioni, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Sh338 milioni, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Sh277 milioni na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba Sh226 milioni kwa mwaka.

Wengine na malipo wanayopata kwa mwaka ni Marais wa Urusi, Vladimir Putin, Sh174 milioni, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia Sh137 milioni, Michael Satta wa Zambia, Sh126 milioni, Rais wa Angola, Jose dos Santos Sh91 milioni, Rais wa Lesotho, Profesa Pakalitha Mosisili Sh88 milioni, Armando Guebuza wa Msumbiji, Sh84 milioni na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping Sh60 milioni.

Wengine ni Rais wa India, Pranab Mukherjee Sh49 milioni, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Sh27 milioni, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Mothlanthe Sh331 milioni, Waziri Mkuu wa Namibia, Nahas Angula Sh160 milioni, huku Baba Mtakatifu wa Kanisa la Romani Catholic, Papa Benedict XVI akifanya kazi bila kulipwa mshahara.

 
Hivi hao wa china, zimbabwe nk hizo milioni ni za tshs au ni za fedha gani?
 
Umeona eeh!...Mie nimebaki mdomo wazi kuona Kikwete anavuta pesa ndefu kuliko Rais wa India na Urusi na marais wengine. Kwa maoni yangu hata mshahara wa milioni 5 tu unamtosha Rais wa Tanzania maana kila kitu anafanyiwa na pesa za walipa kodi na anapomaliza Urais bado walipa kodi wanamtunza hadi kufa kwake na mshahara wao hauna kodi hata ya senti moja. Kuhusu kodi hili halikuwekwa wazi ila najua Obama na Cameron (UK) mishahara yao hutozwa kodi kila mwaka.

Aisee Mugabe ni milioni 2 na kidogo kwa mwezi, halafu ndiye dikteta huyo.
Takwimu muhimu sana hizi.
Vipi kuhusu kodi, maraisi wengine nao hawakatwi kodi?
 
Daaah nimebaki kutingisha kichwa tu. Huu ni uchoyo na ubinafsi kabisa.

Hospitali hazina dawa, mashuleni watoto wanakaachini miundo mbinu dunii, halafu mafisadi bado ni wao wao.
 
Reactions: BAK
Ni miongoni mwa majitu manyang'anyi haya.

Watumishi wengine wa serikali wakiomba mishahara angalau ya kukidhi kiwango cha kununulia nyanya yanakuwa ni majitu ya kwanza kudai eti serikali haina pesa huku wao wakichota watakavyo na kodi hayalipi
Uzalendo gani huo?

Unachuma pesa zaidi ya nchi zilizo na uchimi zaidi yako.

Duh kweli taifa limevamiwa na majambazi!!
 
LOL, Za ndege gan yule uchanganye na zako! kwan yule ndege naye analipwa sh'ng ngapi?
 
KOKUTONA wabonaki waitu? Ija nikugambile ebigambo.

Btw huyo jamaa mropokaji achana naye ana laana ya kula rambirambi ya mjane wa Mwangosi!

Wabona kantu mtani umepoteea poti.

Hata mm nimemshtukia...something wrong kabisaa.

Yaani hasikitiki hata nchi inavyotafunwa na wachache wengi wakiangamia.

Umzima lakini mtani?
 
km ni siri mishara yao kati ya mwajili na mwajiliwa sasa mwajili wa mwanasiasa ni nani???? jibu ni mwananchi na sasa mwananchi ambae ndie mwajili anataka kujua tafadhal
 
Reactions: BAK
km ni siri mishara yao kati ya mwajili na mwajiliwa sasa mwajili wa mwanasiasa ni nani???? jibu ni mwananchi na sasa mwananchi ambae ndie mwajili anataka kujua tafadhal
 
Rafiki KOKUTONA ndio maana hawataki Watanzania tuijue mishahara yao. Muajiri wao ni Watanzania halafu mishahara wanajipangia waajiriwa tena kwa siri halafu hawataki muajiri wao ajue mishahara waliyojipangia!!!! Wakati huo huo hawataki kuongeza mishahara ya Walimu na Madaktari kwa kisingizio Serikali haina pesa!!! Ila pesa ya kujilipa wenyewe mishahara minene siku zote haikosekani!!! Eti ni kosa kutangaza mshahara wa wanene hadharani!!! Walifungie tena Mwananchi kwa kuvunja sharia ya kuanika mishahara ya wanene hadharani.

Daaah nimebaki kutingisha kichwa tu. Huu ni uchoyo na ubinafsi kabisa.

Hospitali hazina dawa, mashuleni watoto wanakaachini miundo mbinu dunii, halafu mafisadi bado ni wao wao.
 
Last edited by a moderator:
Tena ni majambazi ya hali ya juu hata aibu hayana. Kama mshahara wako ni wa halali nawe unaona unastahili kulipwa mshahara kama huo, kwanini ufanye juu chini kuuficha usijulikane!?

 
Wabona kantu mtani umepoteea poti.

Hata mm nimemshtukia...something wrong kabisaa.

Yaani hasikitiki hata nchi inavyotafunwa na wachache wengi wakiangamia.

Umzima lakini mtani?


Asikitike nini wakati yeye ni mwizi wa mbao mufindi? Kelele zoote anazopiga anataka wajue amerudi kuisaidia CCM. Kisha nao wampe tenda.
 
Reactions: BAK
Mishahara ya hao viongozi, serikali inaifanya siri kwasababu wanajua utendaji wa hao watu hauendani na wanacholipwa. wanalipwa kingi ila utendaji madudu matupu .. Imagine unaingiza mia mbili alafu mwisho wa siku unalipwa mia nane.. kuna mtu atakubaliana na huo ujinga?
 
Reactions: BAK
"Katibu Mkuu wa Tanzania Labor Party (TLP), Jeremiah Shelukindo alisema ni vyema kila mtu akaheshimu sheria inayozuia kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwaudhi baadhi ya viongozi wa umma."

What stupidity kutoka kwa eti mtu wa chama cha wafanyakazi!!!
Nilitegemea huyu kilaza ,ashtuke na mshahara huu,GAP kubwa iliyopo kati ya mfanyakazi wa serikali na RAIS(wote wanalipwa na walipa kodi )

Tuna shida na hivyi vyama vya ruzuku.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…