Mshahara wa polisi


Ahsante sana kwa kunifungua kichwa kwa mawazo yako. Kwa kweli ulichokisema kina msingi mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu anayejitambua. Siyo kila siku watu wanalia lia ilhali wana vichwa ingawa sijui kama vinafanya kazi vizuri.
 
Last edited by a moderator:

Kitu ambacho sijaelewa ni kwamba mwishoni mwa Miaka ya 90s TRA iliunganishwa na kuboreshewa Mishahara ili kuwafanya wafanye kazi kwa Morali na kutotamani Rushwa.Inasemekana mkakati huu uliboresha Makusanyo ya Kodi na Pato la Taifa.
Naomba Ushauri wako ili nijue kama aliyebuni mkakati huu alikosea.
Pili,Wabunge wanapokea 11,000,000/= kwa Mwezi na Posho kibao na Walimu wengi na Polisi wanapokea Chini ya Tshs.300,000/= kwa Mwezi,Unafikiri kwa nini wabunge walipwe mamilioni ya Pesa ilhali nao wanaweza kufanya shughuli za Ujasiriamali?
Mkuu nasubiri kwa hamu sana majibu yako ili niweze kutoa hukumu kwa Polisi,walimu,TRA na Wabunge.
 
Ahsante sana kwa kunifungua kichwa kwa mawazo yako. Kwa kweli ulichokisema kina msingi mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu anayejitambua. Siyo kila siku watu wanalia lia ilhali wana vichwa ingawa sijui kama vinafanya kazi vizuri.

Mkuu nisaidie na mimi nifunguke Kichwa.Bado sijaelewa
Ni kwa nini baadhi ya wafanyakazi walipwe Mapesa mengi mfano wabunge Tshs.11,000,000/=na Posho kedekede kwa mwezi ilhali kada zingine kama Polisi na walimu wambiwe wajisaidie wenyewe kupitia ujasiriamali?.
 

1. Mkuu hiyo uliyoiongelea ni paradox niliwahi kuisoma mahali...and it is worldwide. Siwezi kuiongelea maana si Tanzania pekee.


2. Kuhusu TRA ukweli ni kwamba wao kuongezewa mishahara hakujapunguza rushwa yoyote. Mishahara ya walimu na askari wetu iboreshwe si kwa minajili ya kuwazuia kula rushwa bali kwa lengo la kuendana na mabadiliko ya gharama ya kuishi.


3. Rushwa ni tabia induced...si mshahara..something else needs to be done ku-curb hilo la rushwa.

4. Kama nilivyosema hapo awali, tujitahidi kufanya kazi zile tuzipendazo na sio alimradi kazi. Unakuta mtu anamaliza chuo anatuma CV kwenye makampuni kama mia. Una lengo gani???!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…