Mshahara wa mwezi Juni kuchelewa

Mshahara wa mwezi Juni kuchelewa

Status
Not open for further replies.
Mie a/c ilishasoma, inategemea na sehemu ufanyiapo kazi
 
Natamani mishahara itoke tarehe 20 july ndio akili zitakaa sawa kwa watumishi wa umma mkiambiwa ccm ni janga hamsikii

Mkuu tumeishakoma ila tunachofanya ni kulipiza tu, serikali ya ccm inatuua na njaa na sisi tunajenga chuki kwa wapiga kura,
 
ni kweli mpaka sasa balance zina 2,011.09
duu sijui nitafika vp hiyo tarehe 5; nimesha kopa sana na wengingine nimewaahidi leo nitawapelekea hela zao na sijui nani atanielewa nikisema mshahara bado kwa sababu mara zote nimekuwa nikopa nakuwalipa tarehe 26.
Nafikiria jinsi ya kuandika dokezo la uongo aka kufisadisha ofisini kama bosi ataelewa (samahani watanzania wenzangu sina jinsi)

Kichwa Ngumu mi napiga vita sana hayo maisha, ya kusubiri mishahara au safari ya kazini, jifunze kuanzisha kitu chako, hata kama unapata kidogo itakupunguzia makali ya nauli.
 
Mmh hiyo ilikuwa tetesi tu na sio taarifa rasmi mkuu, watu wameshaingiziwa salary tangu jana.
 
Kichwa Ngumu mi napiga vita sana hayo maisha, ya kusubiri mishahara au safari ya kazini, jifunze kuanzisha kitu chako, hata kama unapata kidogo itakupunguzia makali ya nauli.

unawafundisha watu kuiba ela za umma.
 
kujiajiri ni kuiba hela za umma?au hujaelewa? ukiwa umefuga kuku nyumbani unakuwa umeibaje mali ya umma?
huo mtaji wa kuku unautoa wapi? na je kuwahudumia hao kuku? mshahara wenyewe kcc, na matumizi ni mengi, hapo hata hilo wazo la kufuga kuku litakuja kweli ndugu?
 
Ndebile hilo salio umeangalia kwenye akaunti yangu nini? Mbona zafanana?

Zinafanana mkuu, watumishi wasio na ten percent huwa tunakomba zote, utabakiza 'hela ya kulinda kitabu' wakati mshahara wenyewe ndio hivyo!
 
Last edited by a moderator:
hela za kuchangia arusi na send off unapata za kufugia? kuundoa umaskini kunaanza kwanza na wazo, siyo hela. ufikiri wako una sehemu kubwa sana kwenye mafanikio yako.
huo mtaji wa kuku unautoa wapi? na je kuwahudumia hao kuku? mshahara wenyewe kcc, na matumizi ni mengi, hapo hata hilo wazo la kufuga kuku litakuja kweli ndugu?
 
hela za kuchangia arusi na send off unapata za kufugia? kuundoa umaskini kunaanza kwanza na wazo, siyo hela. ufikiri wako una sehemu kubwa sana kwenye mafanikio yako.

nafahamu kuwa wazo ndio mwanzo wa kutengeneza shabaha ya mafanikio, lakini ki uhalisia ni vigumu sana, kwa mtu kufungua biashara kwa mshahara hasa sisi wa kcc. mfano angalia mtu akipiga dili la ela fulani ndio utamuona anakamilisha mambo yake. kuhusu michango ya harusi huo ni mfumo ambao leo hii watu huchangia harusi kuliko maendeleo ya elimu. lakini kuna wachache sana ambao si kila harusi tunachangia.
 
usishtue watu mishahara iko tayari

Kuna watu mishahara yao hainaga longolongo, jwtz, tra etc,! Muulize nesi, mwalimu,walio halmashauri za miji, wilaya nk.kama wamepata mishahara.

Kuna jamaa namuona sasa hivi amevaa tshirt yenye nembo ya TALGWU anaiangalia ATM mashine ya NMB Kenyatta rd hapa Mwanza kwa masikitiko makubwa, nadhani kakuta haisomi.
Mchawi wa CCM ni CCM yenyewe, hivi jiulize kama huyu jamaa ni Clinician wateja wake watapata huduma bora kweli?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom