dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,209
- 49,669
... nikuerekebishe hapo red; hiyo italeta shida; itampa adui nafasi! Maisha yake yote akiwa duniani Yesu alijua yeye ni Mungu hivyo ndiye mmiliki wa vyote....
Mimi ni mkristo. Hii nailinganisha na historia ya Bwana Yesu Kristo. Alipitia njia hii hii bila kujua kuwa yeye ndiye mmiliki wa vyote...
"Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."; Mt. 28:18-20
Anyway, unaweza ku-argue mstari huo ni baada ya kufufuka kutoka wafu hivyo kwa vyoyote wakati huo alisharudi katika uungu wake. Ile sala maarufu ya Yesu katika Yohana 17 ambayo alisali kabla ya kuteswa kwake imeeleza mengi aliyoyajua katika "ubinadamu" wake. Mfano, "Nimelifunua jina lako kwa watu ulionipa kutoka ulimwenguni. Walikuwa wako, nawe ukanipa, nao wamelishika neno lako." Yoh 17:6