Msemaji wa Wizara ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msemaji wa Wizara ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAGL, Mar 19, 2011.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naomba kuelewesha hapa, kati ya katibu mkuu wa wizara na waziri, ni nani msemaje wa wizara? Hii itanisaidia mimi na wengine wasioelewa kama mimi, kuweza kutofautisha kati ya katibu mkuu na waziri, nani ni political figure na anaewajibika kwa wananchi moja kwa moja. Nimestushwa kidogo kwa vitendo vya makatibu wakuu kuwasemea mawaziri kuhusu masuala yao kisiasa. Ref: katibu mkuu mambo ya nje kumsemea Membe na katibu mkuu ujenzi kumsemea Magufuli.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hili ni swali la hovyo, kutoka kwa mtu wa hovyo na mwenye fikra hovyo. Hivi wewe hujui kwamba katibu mkuu wa wizara ndiye mtendaji mkuu wa wizara na ndiye accounting officer? Huyu ana mandate ya kuzungumza lolote kuhusu wizara husika. Katika mazingira ambayo hata waziri ameridhia yeye kutoa taarifa, ni lazima waziri mhusika aongee. Najua wewe ni kati ya wale waliovumisha kujiuzulu kwa Magufuli na ulitaka hilo litimie lakini hukufanikiwa.
   
 3. G

  GAGL Senior Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tukianza kudharauliana na kutoleana maneno ya kashfa na kuona kuwa watu flani ndo wanapost mada za maana hapa, tutakuwa tunavunjiana heshima. Wewe jibu swali na kama huna jibu, usitoe kashfa na usijifanye unajua sana. Kwa taarifa yako katibu mkuu sio political figure, ni mwajiriwa wa serikali chini ya ofisi ya katibu mkuu kiongozi. Hoja ya magufuli kujiuzuru si msimamo au masuala ya kiutawala ya wizara husika. Waziri ni political figure kwa katiba ya sasa, hivyo anapoongelea masuala ya nafasi yake kama waziri, si suala la wizara kumsemea. Katibu mkuu kukanusha mpango wa magufuli kujiuzuru kunahusiana vipi na nafasi yake kama mfanyakazi wa serikali? Msipende kutetea mambo yasiyokuwa na tija katika maendeleo ya taifa, ni ufisadi huo.
   
 4. M

  MASOKO Senior Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  HEE!inatisha
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hawana wasemaji wa wizara? makatibu wakuu si wasemaji ila ni watendaji.
   
 6. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />

  Walisema kila wzr itakuwa na salva reymamu wake sijui kama limetekelezwa! Kurugenzi ya mawasiliano wzr ndio wasemaji
   
Loading...