Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Kwa hiyo Lissu asingelisema hili ndo hizo dola zisingeenda nje? Au huo mfumko wa bei kutokea?Jamani tujitahidi kushughulika na tulipojikwaa badala ya kushughulika na tulipo angukia

Furahieni mjichongee unafikiri mna deni hilo tu, mna madeni mengi mno jishitakini ninyi kwa ninyi. Ha ha ha JUST ha ha ha
 
Kitu siyo uzalendo, kitu nikuwa traitors. Aliyewaambia hawa wazungu ni akili za mwafrika kabisa kachongea. Mzungu akikaa miaka 2 ana rwite off deni, bad debt anaachana nalo. Ila hii mbinu ya kufufua makaburi ya miaka 10 iliyopita ni mzungu kashawishiwa na akili za kiafrika, wicked one.

Hiii inaonekana aliye initiate ni kutoka ndani after all chief Magungo hawakuanza leo. Waambieni wazungu madeni yenu yote mwalipe mkatwe kodi ili myalipe ili mfurahie.

Hebu toa mfano wa kampuni binafsi iliyosamehe deni baada ya miaka uliyosema wewe?

Unafikiri wazungu wanaokota fedha tu na kuja kuzitupa Tanzania.

Acha kujidhalilisha.... hoja hapa tulikosea kama nchi tusahihishe twende mbele tusitafute mchawi

Kama ni uchawi basi aliyevunja mkataba bila kufuata sheria ndio mchawi mkuu. Badala yake tuombe radhi wananchi twende mbele
 
Hebu toa mfano wa kampuni binafsi iliyosamehe deni baada ya miaka uliyosema wewe?

Unafikiri wazungu wanaokota fedha tu na kuja kuzitupa Tanzania.

Acha kujidhalilisha.... hoja hapa tulikosea kama nchi tusahihishe twende mbele tusitafute mchawi

Kama ni uchawi basi aliyevunja mkataba bila kufuata sheria ndio mchawi mkuu. Badala yake tuombe radhi wananchi twende mbele

Lipeni madeni yote mkajishitaki madeni yote. Ili mfurahie. Ha ha ha Just ha ha ha
 
Serikali yamjibu Lissu kuhusu ujio wa Bombadier
By Contributor | August 19, 2017 - 3:13 pm

Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa ,imejibu madai yalitolewa jana na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissukuwa ndege ya Tanzania, Bombadier kuwa imeshikiliwa nchini Canada kutokana na serikali kudaiwa.

Soma taarifa kamili:

Mnamo tarehe 18 Agosti, 2017 siku ya Ijumaa, kuna taarifa zimetolewa kwenye vyombo vya habari kwamba kuna mgogoro wa utekelezaji wa ununuzi wa Ndege ya tatu inayonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kampuni ya Bombadier ya Nchini Canada.

Taarifa hiyo iliendelea kudai kwamba kuna wanasheria wa Kampuni fulani ya Nchini Italia, walioweka zuio la ununuzi wa Ndege hiyo kwa maelezo kwamba, wanakamata mali hiyo ya Serikali kwa kuwa kuna Kampuni inayodai Serikali ya Tanzania.

Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali inapenda kuufahamisha Umma kuwa mgogoro huo upo ila kimsingi ni mgogoro ambao umetengenezwa na Watanzania wenzetu ambao kwa bahati mbaya sana wameweka maslahi ya kisiasa na ya binafsi mbele zaidi ya maslahi ya Taifa.

Mambo Muhimu ambayo Umma Ufahamu

Ndege zinazonunuliwa ikiwepo hii ambayo imetengenezewa Mgizengwe na hao Watanzania wenzetu sio ya Rais Magufuli bali ni za watanzania wote.

Hawa baadhi ya viongozi wa kiasiasa wanaoshabikia migogoro inayokumba jitihada za Rais wetu, za kutuletea maendeleo, hawana Uzalendo.

Serikali imesikitishwa sana tena sana kwa hujuma zinazofanywa waziwazi tena kwa ushabiki wa hali ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa chama hicho, kupingana na mwelekeo mzuri wa Mhe. Rais kutuletea maendeleo
Kwa mtu yeyote mwenye uchungu na Nchi yake,angepambana ili jambo linalohusu maslahi ya Taifa, likiwepo la kununua Ndege, lisikwame na kama kuna mkwamo basi ashilirki kukwamua badala ya kushabikia.

Serikali pia ina fununu kwamba watu hawahawa wanaohujumu jitihada za kimaendeleo, pia wanahujumu hata hali ya usalama wa raia wetu kwenye baadhi ya maeneo ya Nchi yetu. Hili nalo linaendelea kufanyiwa kazi kwa kina.Wanaopinga mambo ya Maendeleo hawapingani na Mhe. Magufuli bali wanapingana na Watanzania wote kwa ujumla.

Hivyo basi ni vyema Watanzania mkaelewa ukweli wa hali halisi na mkapuuzia mambo ambayo yanashabikiwa na baadhi ya viongozi hao wa kisiasa wanaotafuta umaarufu rahisi (Cheap Popularity). Endeleeni kumuombea Rais wetu na Tanzania kwa Ujumla kwani Chini ya Uongozi wake, amedhamiria kwamba hakuna kurudi nyuma (no reverse gear).
Serikali ilikuwa inawahisi baadhi ya wanasiasa kuhusika na hujuma hizi na sasa sio hisia tena bali baadhi yao wameshaanza kujitokeza hadharani.

Hatua za Kuchukuliwa/Zianzochukuliwa:
Kuhusiana na Mgogoro kwenye ununuzi wa Ndege, hatua za Kidiplomasia na za kisheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili. Aidha kwa wale wanaoshabikia na kutengneza migogoro na hujuma mbalimbali dhidi ya maendeleo ya Nchi yetu, Serikali itaendelea na taratibu za kiuchunguzi na haitasita kuchukua hatua za kisheria zinazostahili.

Serikali inatumia pia fursa hii kuwaomba Watanzania wasiwe na wasiwasi wala tashwishi kuhusu mpango wa Ndege kununuliwa na kwamba waendelee kuiamini Serikali yao iliyopo madarakani inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Uzalendo wetu uwe ndio mtaji mkubwa kuliko siasa, dini au ukabila.

Serikali ilikuwa na fununu kwamba kuna viongozi wa baadhi ya Vyama vya Siasa ambao kwa namna moja au nyingine wangependa kuhujumu jitihada za Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuwaletea Watanzania (hasa wanyonge) maendeleo.

Wanasheria hao waliokwenda kufungua madai kwamba Serikali yetu inadaiwa na kwamba Ndege hiyo ishikiliwe, hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo na ni matapeli tu ambao wamesukumwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wasioitakia mema Nchi yetu.

Kwa kuwa Serkali ilishapata fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wana mpango huo, sasa watu hao wamejidhihirisha hadharani kwamba wao ndio wako nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa maslahi yao ya kisiasa.

Serikali ya awamu ya Tano Inawahakikishiwa Watanzania kwamba Ndege itakuja. Wanaokwamisha jitihada za Serikali za kuleta ndege watapanda na ndugu zao watapanda na wafuasi wao watapanda .

Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli haibagui watanzania kwa itikadi za Kisiasa, Dini, Kabila, rangi au utofauti wowote.

Kundi hilo la baadhi ya Viongozi wa siasa walishatoa maelezo ya kuvuruga au kukejeli jitihada za Serikali. Mambo ambayo wanasiasa hao walishayakingia kifua ni pamoja na;

Kushawishi wafadhili wasilete misaada tena Tanzania.Watu hawahawa walishawahi kuomba kwamba Washirika wetu wa Maendeleo wasilete tena misaada Tanzania.

Tunachojiuliza kama Serikali, hivi misaada isipoletwa anayekomolewa ni Rais Magufuli? Au ni Watanzania wanyonge ambao wangekosa madawa, Huduma za Maji, Umeme, n.k.

Jambo la kutia faraja ni kwamba pamoja na jitihada za hali ya juu za watu hao, Washirika wa Maendeleo sasa wameongeza kasi ya ushirikiano na Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Mifano ya wazi ya hivi Karibuni ni tamko la Serikali ya Marekani kupitia Balozi wake kwamba Marekani itaogeza kiasi cha Misaada Tanzania, Ziara ya Tajiri Masuhuri Duniani Bill Gate ambaye pia ameonyesha kuguswa na kasi ya uongozi wa Mhe. Magufuli na kuahidi kutoa fedha zaidi, Ujio wa Viongozi wakuu wa Nchi 15 ndani ya muda ambao Mhe. Magufuli amekuwa Madarakani na mambo mengine mengi.

Kubeza Juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli; Imekuwa ni hulka ya hao baadhi ya viongozi wa siasa kufanya kila jitihada za kubeza jitihada za dhati ambazo Mhe. Rais anafanya kuwaletea Wananchi Maendeleo tena hata bila kujali kwamba eneo husika linaongozwa na Kiongozi wa Chama gani. Hata tukio ka Kihistoria lililofanyika hivi karibuni Jijini Tanga, la kuweka jiwela msingi Ujenzi wa Bomba la Mafuta, Mhe. Rais alionyesha dhahiri kutobagua hata maeneo yale ambayo hayaongozwi na CCM. Tulitegemea huu uzalendo wa Mhe. Rais Ungeungwa mkono na watanzania wote.

Kubeza jitihada za Kunusuru madini yetu na Maliasili. Mhe. Rais Magufuli anafanya jitihada za dhati kabisa kunusuru mali asili zetu na ndio maana akasimamia kwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji suala zima la Makinikia. Hii ilimfanya hata Rais wa Kampuni ya Barick kukodisha Ndege kuja kumuona Mhe. Rais, na tunaamini jitihada hizi zitazaa matunda. Lakini baadhi ya viongozi haohao wa siasa wamekuwa mstari wa Mbele kupingana na jitihada hizi kwamba tutashitakiwa kwa hiyo bora tuache makinikia yapelekwe tukiendelea na majadiliano.

IMETOLEWA NA

Idara ya Habari (MAELEZO)

19/08/2017.


Serikali iache usanii na kukejeli wananchi,isiwafanye "wapumbavu" kama baadhi ya mawaziri wake.

Ni nani asiyejua kuwa migogoro na wawekezaji imetengenezwa na serikali ili waliopewa jukumu la kuongoza wanufaike?

Ni nani asiyejua kuwa kutofuata na kuheshimu sheria ndiyo chimbuko la migogoro ya ndani na nje?
Ni nani asiyejua kuwa kauli zitolewazo majukwaani na yanayotendwa ni kama mbingu na nchi?

Migogoro na wawekezaji "imetengenezwa" vipi na waliokuwa wanapiga kelele za tahadhari kabla,baada na hadi leo dhidi ya matendo na mienendo ya "watawala" na wakala wao kuhusu ushirika huo mwovu?

Inashangaza kama si kukera na kuudhi kusingizia wengine kwa mambo ya kujitakia.Ni sawa na mtu anayekata tawi la mti alilokalia pembezoni mwa shina.Akianguka asingizie uchuro wa waliomsihi abadili namna akakaidi.

Mikataba mfunge nyie,kuivunja kiholela nyie,lawama mtoe nyie! Ni aina gani ya viumbe hao mnaoitwa serikali:uwezo wa kufikiri umegota au?

Uzalendo ni zaidi ya kupiga kelele za kurubuni wapiga kura. Mnaowalaumu hawajakamata wavuvi,hawajawaleta IPTL,SIMBION,ACACIA/BARICK,WACHINA,WAAFRIKA KUSINI wala MORROCO. Na hawajawashauri mvunje mikataba kihuni na kibabe kama mnavyowafanyia watanzania kuwanyima haki za msingi kama "uhuru wa kujieleza,maoni,mikutano,stahiki za watumishi n.k wakakaa kimya! Ipo siku nao watapaza sauti kukataa. SHAME UPON YOU the so called "spokeswoman". Yawezekana historia yako inakufanya usiuone ukweli.
 
Tutayasikia mengi sana.
Ila mwishowe ukweli tumeshaujua. Tatizo kubwa ya Serikali zetu za dunia ya tatu ni kukosekana kwa uwazi 'transparency'
 
Serikali dhalimu ndivyo ilivyo badala ya kumkoromea fisadi na dikteta uchwara aliyetuingiza kwenye huu mkenge wa kudaiwa $38.7 million wanatafuta mwingine wa kumbebesha lawama. Dikteta uchwara ni janga kubwa kwa Taifa huyu hafai kabisa kuiongoza nchi yetu huyu fisadi na mkurupukaji.

"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" >>> SERIKALI YAMPA MAJIBU HAYA LISSU - Manyangumbishi.com


a3cd947cbc1125fa4c6e041a871272d0.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo akili yako hiyo. Nakwambia utayeumiia ni wewe. Unajidunga mshale unafurahia. Ha ha ha ha
Serikali watachofanya ni kubana kodi wananchi walipe ili walipe hilo deni. Na bado unafurahia. Wicked people.


Who is wicked? a wicked person is the one who is supporting the evil Government. haiwezekani wafanye uovu wao halafu waendelee kuficha,sasa kuambiwa ukweli wanatuletea utetezi wa kijinga.
 
Who is wicked? a wicked person is the one who is supporting the evil Government. haiwezekani wafanye uovu wao halafu waendelee kuficha,sasa kuambiwa ukweli wanatuletea utetezi wa kijinga.

wicked ni yule ambaye anaumizwa mwenyewe na anafurahia hayo maumivu kwa shangwe.
 
Sisi watu weusi tuna akili, lakini tunakosa hekima na busara.
  • Watawala hawataki kufanya kazi na wapinzani wao kisiasa ili maendeleo yakipatikana sifa wapate wao peke yao. Hivyo haijalishi wapinzani wana mawazo mazuri kiasi gani, yatapingwa tu.
  • Wapinzani nao wako tayari kuwasaidia watu waliotunyonya kwa karne kadhaa, ili tu kuwathibitishia wananchi kuwa watawala wanakosea.
Mwisho wa siku ni vita ya nzige tu.
 
Back
Top Bottom