kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Msemaji wa Rais wa Russia: Msisome habari za vyombo vya habari vya Israel
Jan 10, 2019 02:49 UTC
Msemaji wa Rais wa Russia amejibu taarifa zilizotangazwa na vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba Moscow inaingilia uchaguzi wa utawala huo kwa kusema: Msisome habari za vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni.
Dmitry Peskov ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, Russia katu haijaingilia na wala haitaingilia uchaguzi wowote ule.
Peskov ametoa kauli hiyo baada ya shirika la intelijensia na usalama wa ndani la utawala wa Kizayuni wa Israel, Shin Bet kutangaza siku ya Jumatatu kwamba, kuna nchi ya kigeni ambayo imekusudia kuingilia uchaguzi wa bunge la utawala huo utakaofanyika Aprili mwaka huu.
Pamoja na hayo, shirika hilo la Kizayuni halikuashiria wala kutaja jina la nchi yoyote ile, lakini gazeti la Kizayuni la Haaretz limetoa ripoti likinukuu taarifa za shirika moja la intaneti la Israel na kudai kwamba China, Iran na Russia ndiyo tishio kubwa zaidi la hujuma za intaneti katika uchaguzi wa utawala huo wa Kizayuni.
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vinazituhumu nchi nyingine kwamba zinaingilia uchaguzi wake pasi na kutoa nyaraka wala ushahidi wowote wa kuthibitisha madai hayo.../
Tags
RUSSIA