TANZIA Msemaji wa M23, Willy Ngoma auawa kwa shambulio la Droni

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
33,612
Reaction score
40,158
FB_IMG_1771952211287.jpg

Msemaji wa kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Willy Ngoma, ameuawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani mashariki mwa DRC siku ya Jumanne.

Reuters imemnukuu mwanadiplomasia wa eneo hilo, afisa mmoja mwandamizi wa kundi hilo na mshauri wa serikali ya nchi za Magharibi akithibitisha kifo chake.

M23 inadhibiti maeneo makubwa ya majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini baada ya mashambulizi ya mwaka 2025 ambapo waasi hao waliteka miji ya kimkakati ya Goma na Bukavu.

Source Trt Africa
 
Kuna chip inasubiriwa kutoka NVIDIA, itawezesha drone kuwa na AI na kujiendesha, haitohitaji tena controller, hata kama kuna jammers za kukata mawasiliano eneo hilo hazitoweza kuidhibiti maana inajiendesha kwa akili zake haitegemei mawasiliano, ikitumwa inakutafuta , ukikimbia inakukimbiza, ukijificha inakusubiri... ni balaa...
 
Ukijiua inakuua
 
Nilisikia siku moja kule youtube Rc mmoja anadai anaogopa sana hii
 
Kifo cha Willy Ngoma ni cha kimkakati, Wamerekani wameua ili kuuhadaa umma kuwa wako serious kwenye vita hiyo. lakini ni ukweli kuwa m23 ni kundi la waasi lenye sapoti toka kwa haohao Wamarekani kupitia Rwanda. upo nyonyo?
 
View attachment 3548186
Msemaji wa kundi la waasi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Willy Ngoma, ameuawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani mashariki mwa DRC siku ya Jumanne.

Reuters imemnukuu mwanadiplomasia wa eneo hilo, afisa mmoja mwandamizi wa kundi hilo na mshauri wa serikali ya nchi za Magharibi akithibitisha kifo chake.

M23 inadhibiti maeneo makubwa ya majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini baada ya mashambulizi ya mwaka 2025 ambapo waasi hao waliteka miji ya kimkakati ya Goma na Bukavu.

Source Trt Africa
Hawa wasemaji nao maisha yao yanakuwa hatarini hata wasipoenda front line. Hivi yule msemaji wa wahouthi kule Yemen aliendaga wapi?
 
Back
Top Bottom