Msekwa: Wanaotumia silaha hawafai kuwa viongozi! CCM kwisha!!!

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Apr 18, 2009
1,195
232
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa amesema wananchi wanapaswa kuwapima wanasiasa wanaotumia silaha wakati wa kuomba kura kama wanafaa au hawafai kuwa viongozi.

Lakini akaeleza kuwa
taratibu za CCM zinasema wanaotumia silaha au kushiriki vurugu kwenye mikutano ya kuomba kura au kufanya kampeni, hawafai kuwa viongozi kwa kuwa wanaleta taswira mbaya kwa wananchi.

Kauli hiyo ya Msekwa imekuja takriban juma moja tangu Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangwalla na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Hussein Bashe kudaiwa kutishiana bastola hadharani, huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msekwa alisema vitendo hivyo vinasababisha wanasiasa kujenga chuki hivyo wanaohusika wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine. "Tumesikitishwa sana na vitendo vya kutishiana bastola wakati wa kufanya kampeni.

Hii inaleta taswira mbaya kwa wananchi na wanasiasa, kutokana na hali hiyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu kitendo hicho ni kosa la jinai kisheria," alisema Msekwa. Msekwa alisema CCM hakiwezi kuwaonya makada hao kwa maneno na wakaelewa hivyo sheria inapaswa kuchukua mkondo wake. Alisema, kiongozi bora ni yule anayetoa hoja na kuzijibu bila ya kuwekeana chuki.

Ugomvi au kutoleana maneno ya kebehi vinadumaza chama na haviwezi kukuza demokrasia. "Hoja zinajibiwa kwa hoja na si kutumia silaha, matusi au maneno ya kusababisha ugomvi. Nawataka wapiga kura wawapime wagombea wa namna hiyo ili wasichague kiongozi ambaye anatumia mabavu kupata madaraka, kwa sababu mwisho wa siku anaweza kusababisha matatizo," alisema. Source: http://mwananchi.co.tz/habari/-/25955-msekwa-wanaotumia-silaha-hawafai-kuwa-viongozi

Maoni yangu:
Kweli CCM haina muelekeo. Wanaona kabisa madhara ya kutumia vurugu (Polisi) ili kukandamiza watu bado unakuta hao hao wanalaani. Nadhani kuna umuhimu CDM kila wanapofanya M4C wawaeleze wananchi kuwa CCM na polisi ni wauaji na waandae CD 2015 waziuze ili uma wa watanzania waelewe 2010-2015 jinsi ambavyo CCM imeshiriki kuua watu wasio kuwa na hatia.

Lets put this way... Chama kinachotumia polisi kuua raia ambao awana hati kwasababu ya kuzuia vyama vingine kufanya siasa nacho hakina sifa ya kushika dolla.
 
Hata Serikali inayotumia silaha na nguvu badala ya sheria kutawala haifai kuongoza
 
Kama mtoaji na mpokea rushwa wote ni wakosaji, hawa wafanyafujo wanafumbiwa macho kwa nini!

"maadili" ni elimu mpya kwa ccm.
Anaebisha amuulize mccm yeyeto popote.
 
Msekwa anazeeka vibaya anaona ya akina Kingwangwala tuu,CCM kuua watu kwenye chaguzi,mikutano ya vyama vingine vya siasa hayaoni CCM ndio sera zao ua ua ua basi
 
Tatizo la viongozi wa ccm ni kama huwa hawana kumbukumbu na yale yatokayo kinywani mwao na kama hii ndiyo aina ya viongozi tulionayo sishangai kuona nchi inakuwa ya namana hii.Ukiangalia maneno ya Msekwa hapo juu na matendo yanayofanywa na polisi chini ya serikali ya ccm utagundua kuwa kuna mechanism huwafanya waongee kwa kujishitaki kwa wananchi na kama kauli hizi zikiingia vichwani mwa watu wenye akili timamu, ccm si iliisha poteza sifa za kuwa chama tawala. Najaribu kulink maneno ya msekwa na maneno ya Sita majuzi kati akituhumu chadema kutokuwa na safu ya viongozi wakati huohuo akidai kuwa serikali inaweza kutoa huduma za afya na elimu bure kama mianya ya rushwa na ufisadi vitadhibitiwa na rasilimali za nchi kutumika vizuri (Karagwe) lakini akimjibu silaha bila kukumbuka aliyokwisha yasema suara la elimu na afya bure likawa tena ni ahadi za alinacha!God is with us now kwa kuwa kila wanapoongea vigogo wa ccm sasa wameanza kuiponda ccm na serikali yao bila ya wao kujua na kama tukiweka kumbukumbu zetu vizuri sioni kiongozi ndani ya ccm mwenye positive determination ya taifa hili! Kwa nini Msekwa asisema CCM tumeshindwa kuongoza na sasa tunaongoza kwa mabavu kwa kuwa tuna polisi na jeshi? Na kwa nini sits aseme ccm imeshindwa kutoa huduma za afya na elimu bure kwa kushindwa kuthibiti mianya ya rushwa na ufisadi? Haya ndiyo maneno yanayotoka vinywani mwao lakini kwa kuwa si waungwana pamoja na uzee wao bado wanazunguka mbuyu wakidhani bado watanzania ni wa 1947! Heri kijana masikini mwenye akili kuliko mfalme mzee mjinga asiyeweza kutoa hata tahadhari!
 
Msekwa anazeeka vibaya anaona ya akina Kingwangwala tuu,CCM kuua watu kwenye chaguzi,mikutano ya vyama vingine vya siasa hayaoni CCM ndio sera zao ua ua ua basi

Hawa wanasiasa wa einzi hizo akili zimepiga "brake" Mkuu!
Nawashangaa sana kuwa hawaoni kuwa watanzania wamechoshwa na mbinu za kipuuzi wanazotumia kuwahadaa wananchi na kujaribu kunyamazisha upinzani.
Chama makini ambacho hakijalewa madaraka hakiwezi kuruhusu Mawaziri waache kazi waende kutishia wananchi/wapiga kura kwenye jimbo lenye uchaguzi mdogo na kuwatishia kuwa hawatapata huduma au kujengewa daraja, hakiwezi kunyamaza kimya waalimu wakinyimwa haki zao, madaktari wakinyimwa haki na kupigwa hovyo. Kila kinapokuwa na mkutano hakuna Polisi anayekwenda kuwachokoza bali huchokozwa upinzani peke yao, hapo lazima pana walakini.
Ukishaona chama kilichotawala nchi miaka 50 kinaanza kuogopa mikutano ya chama cha upinzani ambacho hakijawahi hata kushika dola, ujue kinasambaratika! nakisambaratike! Hakina maana, kilishalaaniwa na mwenye kukianzisha, NAKISAMBARATIKE TU!
 
Sema na umasikini na elimu duni ya watanzania navyo vinachangia sana. Mtu yupo tayari kukubali kushiriki kuiba kura kisa kapewa laki moja, hajui gharama ya hiyo laki ni umasikini na kuzidi kumuongezea aliyeitoa.
 
Iwapo mnakubali hawafai, mmechukua hatua gani? Au ndio ile style aliyoisema EL, ya kulia lia?
 
Sema na umasikini na elimu duni ya watanzania navyo vinachangia sana. Mtu yupo tayari kukubali kushiriki kuiba kura kisa kapewa laki moja, hajui gharama ya hiyo laki ni umasikini na kuzidi kumuongezea aliyeitoa.

Na huo ndiyo mtaji wao! Sasa wapo watu jasiri ambao wamejitolea kuwaelimisha wananchi. Wao wapo mbioni kubuni mbinu za kuwamaliza.
 
Serikali ya CCM ndiyo imetoa kibali kwa hao wanasiasa kutumia kuwa na silaha! Tanzania kwa sasa ni inanuka silaha - everywhere!
 
Na huo ndiyo mtaji wao! Sasa wapo watu jasiri ambao wamejitolea kuwaelimisha wananchi. Wao wapo mbioni kubuni mbinu za kuwamaliza.
Na hapo ndipo tunapohitaji strategic thinkers (wenye mbinu zenye ushawishi wa ushindi ktk kufikia malengo ya kuelimisha wananchi) ndani ya CDM, otherwise nchi itaendelea kuwa masikini na ndugu zetu wataendelea kubeba mabox ulaya na kwingineko kisa mifumo mibovu ya nchi yetu. Tunahitaji fursa za kiuchumi ziwe wazi zenye kufaidisha kila mtanzania, na siyo akina J Makamba amboa wameingia kwenye system na kugeuka kuwa mabwanyeye wenye kukumbatia mifumo kandamizi ya kuua watu(mfano migodini alipokuwa mwenyekiti pia comments za juzi jimboni kwake). Vijana tuungane kuwaelemisha vijana wenzetu kila mahali waondokane na giza, ila wale wasiotaka kuelewa tuwache kwani wengi wao ni wanufaika (walishapewa vyeo) au wanatarajia kunufaika (kama akina mwigulu labda anategemea siku moja atakuja kuwa waziri).
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa amesema wananchi wanapaswa kuwapima wanasiasa
wanaotumia silaha wakati wa kuomba kura kama wanafaa au hawafai kuwa viongozi.

Lakini akaeleza kuwa taratibu za CCM zinasema wanaotumia silaha au kushiriki vurugu kwenye mikutano ya kuomba kura au kufanya
kampeni, hawafai kuwa viongozi kwa kuwa wanaleta taswira mbaya kwa wananchi. Kauli hiyo ya Msekwa imekuja takriban juma
moja tangu Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangwalla na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Hussein
Bashe kudaiwa kutishiana bastola hadharani, huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake.
 
Back
Top Bottom