Jay Milionea
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 1,185
- 154
Kwakweli kingunge kajipotezea heshima yake
Msekwa nilikuwa namheshimu sana lakini naanza kumdharau kama lapulapu la kudekia choo cha stendi
Mzee kazeeka huyo
Umejitahidi sana kumpigia chapuo huyo mzee mwenzako Mamvi na kalalamikia NEC kwa kukatwa jina lake sasa wewe mzee unahitaji kitu gani, maana kama kukatwa watia nia 37 wamekatwa
Ziba masikio! nani kakulazimisha usikilize yuko huru kuongea chochote anachojiskia, umechoka mwenzio nani hapa, wee tulia tu dawa ikuingie umechoka nin hatabado.Umejitahidi sana kumpigia chapuo huyo mzee mwenzako Mamvi na kalalamikia NEC kwa kukatwa jina lake sasa wewe mzee unahitaji kitu gani, maana kama kukatwa watia nia 37 wamekatwa pia iweje we uendelee kulalamika na kusema ni jambo haramu, wewe kwani Lowassa alikuahidi kitu gani mpaka umtetee hivo?
Naona sasa mzee umechoka bora upumzike tuachie Magufuli wetu, kama huna kazi bora uwe una lalala kwanza unajiaibisha tuu mzee mzima ovyooo!
Ndo maan Nape Nnauye kakujibu kwamba fanya unachotaka kufanya, sasa huoni kuwa ni fedheha hiyo? Dah aibu hiyo
Hongera kwa kuside na wahalifu!Mzee Kingunge amewavua nguo wanaCCM wenzake,kwa kuhanika madudu yaliyofanyika kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa ccm,jambo muhimu kwasasa wachutame-"msataarabu ukivuliwa nguo,huchutama"(kutafakari na kurekebisha kasoro huko waendako)
Huyo mzee ndo kachoka, hajui hata mabadiliko ya taratibu ndani ya chama chake.Muda si murefu ataitwa msaliti. Maana hawachelewi hawa magambawaz. Mzee anatoa ishara ya kuchoka kwa chama.
Ukisoma umetulia kauli ya Msekwa ni ya kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Kingunge kasema kanuni na taratibu zilizopo ambazo hazijahuishwa, mbona Msekwa hakusema zilibadilishwa lini?
Unataka kusema hata hao akina Nchimbi na wenzake ambao ni wajumbe wa kamati Kuu hawakufahamu hizo Kanuni zilizobadilishwa? Na hao akina Mtaturui wanaisdhi katika maisha ya zamani ambayo kilichosemwa adharani na mwenyekiti hapaswi kupingwa.
Ingawa mimi ni mmoja wa wale waliokuwa wanapinga kuteuliwa Lowassa lakini kwa maoni yangu huyu Mzee amejirejeshea heshima kwa jamii kwa kusimamia uvunjifu wa taratibu na kanuni.
"Ukiona mtu anabadilika , ujue amenunuliwa..."kingunge amejinajisi
Uhuru wa kusema ni wa kila mtu ndo maana Mungu kampa kila mtu mdomo wake.
Kingunge anafikiri hao 36 si watu?? maana Lowasa Lowasa imekuwa mpaka kero. Akumbuke walikuwa 38. Mmoja ni Magufuri kapita wamebaki 37. Mmoja ni Mr. White hair kakatwa wameki 36. Fagio la jumla puu..yameisha.
====Tunaenda kwenye kampeni za Magufuri bwana fungeni mijadala====.
Nafikiri na wewe ukumsoma vizuri na kumsikiliza vyema. Kama unayo video rejea tena alivyosema. Kawasemea wote. Kamati ya maadili kupeleka majina matano haikuwa sahihi haina madaraka hayo. Alisema wote 38 walipaswa kufikishwa kwenye kamati kuu n kuojiwa (tena akasema maswali sinzaidi ya matatu). Najua na yeye anajua hawakutaka jina la lowassa lifike hata Kamati Kuu maana hawakuwa na uhakika kama litaweza kukatwa huko! Lakini kama ni kusemea alisemea wote siyo Lowassa pekee.Kingunge anaweza kuwa sahihi..ila angeonekana nguli kweli kweli kama angekuwa anawaongelea watia nia wote walioachwa....yeye kaonekana kulalia upande wa kuaminisha jamii kuwa ni Lowassa ndiye aliyeonewa pekee...na kwa kuwa toka awali alionekana kuwa ni mtia nia aliyekuwa anamsapoti, tumeishia kujumlisha 1 + 1 = 3...
Kamsikilize vizuri, hakuongelea Lowassa tu bali wote 38 waliorejesha fomu. Najua wote mnafikiria alimwongelea Lowassa tu kwa sababu alidhajitanabaidha kwake na kwa sababu kupindishwa kwa kanuni (kwa mujibu wake) ililenga zaidi kutaka kumwondoa Lowassa. Alisema wote 38 walipaswa kufikishwa kwenye kamati kuu na kuhojiwa. Ni kamati kuu ndiyo ingetoka na majina matano baada ya mchakato huo, siyo kamati ya maafili!kwa nini kanuni zimhusu Lowasa tu? Babu amekula hela ya mamvi anatakiwa afanye chochote kionekane