Naungana na mleta uzi juu ya kufanyika jitihada za kuenzi kipaji za Mzee Tofi, ni kweli amenza kuonekana kwenye screen akiwa tayari mtu mzima ila muda mrefu alikuwa anashiriki michezo ya jukwaani wakiwa na mzee Majuto pale Tanga.
Kuna baadhi ya michezo ilirekodiwa enzi hizo, ila ipo kwenye poor quality, ile ya VHS kabla hata ya kuibuka Bongo Muvi....ipo moja inaitwa "Mume wangu mlevi"
Inawezekana Mzee Tofi anakosa fursa kwa sababu makazi yake zaidi ni Tanga, fursa ni chache, tofauti na mwenzake Mzee Majuto ambaye mambo yanamuendea tambarare.
Naungana na wazo la mleta uzi juu ya kuenziwa kwa mzee Tofi, ana kipaji karibu hata sawa na Mzee Majuto kwa aliyewahi kuona michezo yake ya enzi hizo.
Tusisubiri akishafariki ndio tuwasikie akina Mzee Majuto wanamlilia kwenye media....."Mzee Tofi tumetoka naye mbali" blah blah blah...
Nadhani waandishi wa habari za burudani na michezo wamfuatilie, kama kuna uwezekano hata Majuto abanwe amkumbuke mwenzake....ila kama labda anasumbuliwa na tatizo la ulevi, au matumizi mabaya ya pesa...hiyo ni ishu nyingine...ila pia bado anaweza kusaidiwa/kushauriwa kwa hilo.