Msanii wa kimataifa Alikiba azindua rasmi Television yake "ALIKIBATV"

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
5,047
Habari wakuu!

Huku wengine wakiendelea kujivunia kuchora mitattoo ya bei ghali na meno ya dhahabu.

Msanii wa kimataifa Alikiba yeye aendelea kuitumia vyema karata yake baada kupata Shavu la sony global deal, hii leo amezindua rasmi televevision yake "ALIKIBATV" ambayo itaanza kupatikana kwny DSTV pamoja na ving'amuzi mbalimbali. Dunia nzima watu mbalimbali watapata access ya kuitazama channel hiyo.

Hongera Kiba, gooo King Kiba..


AlikibaSigning-660x400.jpg


#Repost @officialalikiba with @repostapp
・・・
Caption: MAJOR ANNOUNCEMENT #5: ALIKIBA LAUNCH ALIKIBA TV IN GLOBAL PARTNERSHIP WITH ROCKSTARTV

ALIKIBA channel to give fans, broadcasters, platforms and content licensors an All Access Rockstar Pass to everything in the world of Alikiba, world class around-the-clock content.

Subscribe to the official Alikiba YouTube and Facebook Channels, Rockstar TV channels, SoundCity and several other channels around the world to be announced soon...

@RockstarTelevision #RockstarTV #KingKiba #AlikibaTV #ROCKSTAR4000 @ROCKSTAR4000 @SoundCityAfrica #Aje #KingKiba
===============

Meneja wa Alikiba, Seven Mosha, afanunua nini kitakachokuwepo kwenye Alikiba TV

Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi naye, Rockstar4000 imetangazakuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’

Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi.

“Alikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.

“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga dunian ivitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.

Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje, amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita ‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.


Chanzo:Bongo5
 
Ametisha sana...

Ila meneja wake wafanye kazi, msanii anatoa hit songs za kutosha kwanini hawamtafutii shows? Mapato ya msanii kwa kiasi kikubwa yanatokana na shows, wanategemea awe bilionea kivipi?

Alikiba anatoza dau kubwa ndiomana show zake nyingi anapigia kenya, za bongo nyingi dau dogo, ndiomana mwaka jana kwa mujibu wa utafiti wa msetoa tv Alikuwa ni msanii wa 3 kwa kuingiza pesa nyingi East africa kupitia show, Alifanya show chache lakin za mpunga mrefu mfano show kwenye uzinduz wa safaricom kenya, koroga festival etc, Pia mwaka jana kaamua kuja na mpango wake kuwa anaandaa show mwenyewe ili maximize profit mfano show ya "funga mwaka na kingkiba, pia mwaka huu vile vile atakuwa anasimamia show zake mwenyewe, tofaut na yule mwenzake anayeitwa na mapromota kwa tu million 20 per show.
 
Hizo ulizozutaja ni online tv, Huwez kuipata dstv au azam, ila hii ya kiba sio Online tv, ni tv kama Cloudz tv, East Africa tv, itv, mtv etc
Tujuze mkuu uzinduzi wa hiyo tv utafanyika wapi na lini na itakuwa saa ngapi? Tusemezane
 
Back
Top Bottom