Kanyunyu
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 335
- 495
MSANII maarufu wa muziki nchini Kenya,Charles Kanyi alimaarufu JAGUAR ameangua kilio kizito baada kushindwa kwenye kura za maoni akigombea Ubunge jimbo la Starehe kwa tiketi ya chama cha JUBILEE.
Matokeo ya kura za maoni yaliyotangazwa mapema leo yamempa ushindi mwanasiasa Maina Kamanda kupeperusha bendera ya chama cha JUBILEE Jimbo la Starehe, Hata hivyo kuna madai kwamba JAGUAR amechakachuliwa ili kumpa Maina Kamanda ushindi kwa mkakati wa siasa za 2022.
Mfumo wa kura za maoni unaotumika kwenye vyama ni ule mfumo unaoruhusu wanachama wote kupiga kura za maoni (Primaries). Hata hivyo JAGUAR ana uwezekano mkubwa kugombea Ubunge akiwa Mgombea binafsi kutokana na wapambe wake kumshauri asikubali kuchakachuliwa.
Wakenya watapiga kura za Uchaguzi mkuu mnamo Agosti 8 mwaka huu kuchagua Rais wa nchi hiyo, Magavana, Maseneta, Wabunge, Wawakilishi wa wanawake na Madiwani (MCA).