Msando kuchangisha hela alizoahidi kutoa Rais ni halili??

Msando kuchangisha hela alizoahidi kutoa Rais ni halili??

samesame

Senior Member
Joined
Jul 21, 2019
Posts
143
Reaction score
324
Albert Msando anayo haki ya kumwombea mchango mtu yeyote yeye binafsi, lakini je ni halali yeye kupinga Rais kama taasisi isitoe mchango. Ila yeye ndio aitishe mchango kwa wananchi kwa kutatua tatizo lile lile ambalo Rais kama taasisi alishatoa maamuzi kulimaliza?

Huu si utapeli kwa kutumia mgongo wa taasisi ya Ikulu maana Rais taarifa yake inafika mbali na kutumia taarifa ya Ikulu kuombea michango ni kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu. Kumbuka kaweka namba yake na si ya mhusika je huu si utapeli? Je, Rais kamtuma amwombee na kwa taratibu gani za ofisi ya Rais?

Swali kubwa ni, je ni halali kuingilia maamuzi ya Rais?? Yeye kasema atalipa yeye. Je, ni raia gani anaweza kumpinga Rais?

Rais anaweza kusamehe kijiji kizima kisilipe kodi je kuna mwingine anaweza sema tuwalipie Rais asiwasamehe??

Huku sio kumpinga Rais?

Angalizo: Tusiidhalilishe taasisi ya Urais kwa kuamini ni maskini haiwezi kumlipia mtu milioni tano. Siami kama Msando hajui Rais ni nani na kama anajipendekeza atafute njia nyingine.

Ombi langu kwa msemaji wa Rais amkataze Msando kwa kile anachokifanya maana ni utapeli na udhalilishaji wa ofisi kubwa ya nchi.

IMG_2017.JPG
 
Msando na taaluma yake hajui km hilo tatz ni la mfumo
Inasokitisha sana naona na kina Mwana fa nao wamegeuka wapiga Matarumbeta wa Rais ni mwendo wa kujipendekeza tu
Xax hyo mama ni wa Muhimbili, vp wale wa Tandahimba, Katonto-Sumbawanga sauti zao nan anawaskiliza!?
Vip kesho akitokea na mwengne Teule, Muheza Msando ataitisha tena michango!?
Tumekuwa watu wa kujipendekezapendekeza tu km Mazombie
Ww Msando km unautaka Ubunge kuna haja gn ya kujitoa ufahamu km kweli unajiamin.
Sisitiza Bima ya Afya nchi nzima
Piga Kampeni hata ya Mtaa wako wawe n Bima ya afya cyo Michango
Yn wakt mwengne wanatua kinyaa sana hawa jamaa
Jitu somi lkn linakuwa pumbavu
Badala ya kudeal na tatizo yey anahangaika na matokeo
 
Utawala wa Jiwe ni wa hovyo. Anapenda Kusifiwa sifiwa na Kuona wanahuruma wakati ni Unafiki tu.
Watanzania Kibao wana Matatizo mazito hata kuzidi huyo mama, acheni cheap Popularity.
 
NINGEMUELEWA...ANGESEMA NIMEENDA HOSPITAL KUFUATILIA TAARIFA ZA MAREHEMU NA WAGONJWA WOTE WANAODAIWA KIASI KWAMBA WAKASHINDWA KURUHUSIWA KUTOKANA NA MADENI...

NIKAONA HILI SUALA NILILETE KWENU...TUWASAIDIE MASKINI HAWA WA MUHIMBILI KUWALIPIA MATIBABU YAO WATOKE...NA ATUSAIDIE KUFUATILIA ZA UHAKIKA JUU YA KUSHINDWA KWAO KULIPA MATIBABU YAO NA MUDA WALIOKAA HOSPITAL...

SASA HUYO MAMA ALISHASAIDIWA...SIO MAHALI PA KICK HAPO...TUENDE PENGINE...
 
Anataka kutumia jina la rais kutapeli, kuna watu walishawahi kukamatwa kwa utapeli wakitumia jina la mama Salma Kikwete na mama Janeth Magufuli, na huyu naye yuko kwenye aina hiyo hiyo ya utapeli.
 
Albert Msando anayo haki ya kumwombea mchango mtu yeyote yeye binafsi, lakini je ni halali yeye kupinga Rais kama taasisi isitoe mchango. Ila yeye ndio aitishe mchango kwa wananchi kwa kutatua tatizo lile lile ambalo Rais kama taasisi alishatoa maamuzi kulimaliza?

Huu si utapeli kwa kutumia mgongo wa taasisi ya Ikulu maana Rais taarifa yake inafika mbali na kutumia taarifa ya Ikulu kuombea michango ni kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu. Kumbuka kaweka namba yake na si ya mhusika je huu si utapeli? Je, Rais kamtuma amwombee na kwa taratibu gani za ofisi ya Rais?

Swali kubwa ni, je ni halali kuingilia maamuzi ya Rais?? Yeye kasema atalipa yeye. Je, ni raia gani anaweza kumpinga Rais?

Rais anaweza kusamehe kijiji kizima kisilipe kodi je kuna mwingine anaweza sema tuwalipie Rais asiwasamehe??

Huku sio kumpinga Rais?

Angalizo: Tusiidhalilishe taasisi ya Urais kwa kuamini ni maskini haiwezi kumlipia mtu milioni tano. Siami kama Msando hajui Rais ni nani na kama anajipendekeza atafute njia nyingine.

Ombi langu kwa msemaji wa Rais amkataze Msando kwa kile anachokifanya maana ni utapeli na udhalilishaji wa ofisi kubwa ya nchi.

View attachment 1179205
Rais (president) siyo yaasisi ni kiongozi tu wa taasisi na anaweza kupingwa au kukosolewa na MTU yeyote. Urais (presidency) ndo taasisi yenye viongozi wengi wakiongozwa na Rais ambaye a naweza kuwa msukuma, mugogo nk.
 
Badala apambanie system ya kudai maiti iondolewe?Wasomi msimu huu wamekuaje sijui
Juzi jumamosi mjomba wetu ameenda Mwananyamara kuchukua maiti Ya mwanae ana umri wa miaka mitatu na nusu, Yule mtoto alizidiwa, kapelekwa pale daktari kasema mtoto ameshakufa uyu, basi maiti ikachukuliwa ikapelekwa mortuary,
Asubui wanaifuata eti maiti ya mtoto inatakiwa ilipiwe efu thelasini ya mortuary,, walilipa ikawa hamna jinsi, hii nchi kwakweli
 
Akawasaidie na wengine pale hadi leo wameshindwa kutoa maiti deni milion 17 kwa mwezi ..
 
Utawala wa Jiwe ni wa hovyo. Anapenda Kusifiwa sifiwa na Kuona wanahuruma wakati ni Unafiki tu.
Watanzania Kibao wana Matatizo mazito hata kuzidi huyo mama, acheni cheap Popularity.
Msando anatafuta uteuzi. Apuuzwe tu!
 
Yaani achangiwe kwenye hiyo namba yake ya simu?

Asije akazila hizo hela huyo.

Bora kama hata wangemwanzishia huyo mama GoFundMe account.
 
Khaa sasa kujipendekeza huko kumezidi kuna watu wanatamn hata wasaidie kunya kwa niaba ya, ikiwezekana huyo mtu asikanyage ht chooni kbsa
 
Rais (president) siyo yaasisi ni kiongozi tu wa taasisi na anaweza kupingwa au kukosolewa na MTU yeyote. Urais (presidency) ndo taasisi yenye viongozi wengi wakiongozwa na Rais ambaye a naweza kuwa msukuma, mugogo nk.
so unataka kuniambia ile misaada anayoigawa anaigawa kama mtu au taasisi?? meens rais wetu kawa billionaire ghafra eeh! ninavyojua ahadi zote zinazotolewa na rais ni za taasisi yeye anatoa kwa niaba tuu
 
Back
Top Bottom