Msamaria mwema aliyefichua siri ya ukwepaji kodi TRA aswekwa rumande, TRA yamdhulumu pesa yake

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
  • Alisweka rumande na polisi kituo cha Oyster bay alipofuatilia kupewa haki yake ya malipo kama msamalia mwema aliefichua ukwepaji kodi.
  • Kwa mujibu wa taratibu za TRA alistahili kupata mgawo wa Tsh210 milioni sawa na 3% ya pesa zote alizofichua.
  • Mpaka leo hajapewa pesa yake anazungushwa.
  • Amlilia Magufuli aingilie kati ili apewe haki yake.
Msiri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye alifichua ukwepaji kodi wa Sh7 bilioni, anasotea mgawo wake wa asilimia tatu kwa zaidi ya miezi sita sasa licha ya kodi hiyo kulipwa.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini taarifa hizo zilifunguliwa makao makuu ya upelelezi jijini Dar es Salaam kwa kumbukumbu CID/HQ/PE/151/2013 na alistahili kupata mgawo wa Sh210 milioni.

Kwa mujibu wa utaratibu wa TRA, mtu yeyote anayefichua ukwepaji wa kodi na kodi hiyo kukombolewa, hutakiwa kulipwa asimilia tatu ya kodi iliyolipwa kutokana na taarifa alizofichua.

Hata hivyo, tangu afichue ukwepaji huo na TRA kulipwa kodi iliyokuwa imekwepwa, bado mtoa taarifa huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa, amekuwa akizungushwa kulipwa mgawo wake.

Habari zinadai baada ya kufunguliwa kwa taarifa hiyo na TRA kufanya uchunguzi wa kina, ilibainika kampuni hiyo ilikuwa imekwepa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyofikia Sh7 bilioni.

“TRA wakaifanyia assessment (ukadiriaji) hiyo kampuni ikaonekana inatakiwa kulipa kodi pamoja na faini inayofikia Sh7 bilioni. Wao wakakimbilia mahakamani, lakini wakashindwa,” Mtoa habari alisema.

Chanzo hicho kilidokeza kuwa baada ya kushindwa, kampuni hiyo ilishalipa Sh5 bilioni kati ya Sh7 bilioni, lakini msiri huyo alipofuatilia mgawo wake akaswekwa rumande kituo cha Oysterbay.

“Alikamatwa na akazuiwa pale kwa saa kadhaa akihojiwa alijuaje ile kampuni inakwepa kodi. Vitendo vya aina hii vinaweza kuwakatisha tamaa watoa taarifa kushirikiana na TRA,” kilidokeza chanzo hicho.

Wakili Peter Mshikilwa anayesimamia maslahi ya msiri huyo wa TRA, jana alipotafutwa na gazeti hili alithibitisha mteja wake kuzungushwa kulipwa asimilia tatu licha ya ushahidi wote uliopo.

“Hivi tunavyoongea amenipa maelekezo nimuombe Rais Magufuli (John) aingilie kati suala hili, maana hii ni haki yake na kumbukumbu zote kuwa ndiye aliyetoa taarifa hiyo zipo,”alisema Mshikilwa.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo, alipoulizwa jana alimtaka msiri huyo kujitokeza akiwa na vielelezo vyote kuwa ndiye mtoa taarifa.

“Kama kweli kodi imelipwa ni haki yake kulipwa hiyo asilimia (asilimia tatu), lakini aje kuniona na vielelezo vinavyothibitisha ndiye mhusika. Aje kuniona nitampa mwongozo,”alisema Kayombo.

Kayombo alisema kwa zile taarifa ambapo kodi iliyokwepwa hukombolewa, watoa taarifa hulipwa mara moja lakini malipo yanaweza kuchelewa kama suala hilo linasubiri uamuzi wa mahakama.

Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa wanafikiria kuboresha mchakato wa utoaji wa mgawo huo kwa watoa taarifa za siri ili kuvutia watoa taarifa wengi zaidi kuweza kuwafichua wakwepa kodi.

Source: Mwananchi
 
Ndio maana hii nchi wazalendo wanapungua siku hadi siku .....huu ni uonezi wa Hali ya juu.!

Ipo siku mtu atajua njama za Kumdhuru Rais lakini atakaa kimya Kwa sababu za kipuuzi Kama hizi.

Kama Taifa tuwe na uzalenda wa kuwasitiri wazalendo Kama hawa japo wanazidi kupungua siku hadi siku.

Namwombe Rais amsaidie huyu Mzalendo Kwa maslahi ya Taifa.
 
Hapo wamempigia hesabu wakakuta hiyo pesa ni ndefu wanamlia timing wamdhulumu, kama ipo kisheria wampe kama ipo ki MCC wamwambie,Bahati ya mwezio usiilalie mlango wazi.
 
Watanzania bana hatupo serious kwenye kila kitu, mpeni haki yake bana
Naanza sasa kuona matunda ya kuwa na rais anayewajibika na kuithamini kazi yake. Huyo mkurugenzi wa TRA hilo jibu alilotoa ni la kuua soo! Ameona uzembe ulikwishafanyika na naona ameogopa kutumbuliwa jibu ndio maana akaja na jibu la kimkakati namna hiyo. Ingekuwa enzi za Kikwete daa... jibu la jeuri na nyodo lingetoka...
 
Mpeni haki yake, ukute alikuwa muajiriwa wa hiyo kampuni iliyokuwa inakwepa kulipa kodi, kama ameweza wasaidia mkapata kodi kwanini mshindwe kurudisha fadhira? Ndio maana wananchi muda mwingine tunaacha uhalifu kama huu upite kutokana na mambo kama haya.
 
Yaani wanamnyima Na pia wanamuweka ndani.....?!!! Wanashangaza sana....!
 
Back
Top Bottom