Msamaha wa kodi kwa watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi...

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
UFAFANUZI KUHUSU
MSAMAHA WA KODI
KWA WATUMISHI WA
UMMA
Image
Watumishi wengi wa Serikali na
Mashirika na taasisi za Umma
wamekuwa wakiuliza mara kwa
mara kuhusu msamaha wa kodi
katika ununuzi wa magari yao
kwa ajili ya kuwasaidia usafiri wa
kwenda kutekeleza majukumu yao
ofisini na kuwasaidia nyumbani
katika shughuli zao mbalimbali za
kijamii. Yafuatayo ni maelezo ya
utaratibu wa kupata msamaha wa
kodi kwa magari yatakayoingizwa
au kununuliwa hapa nchini na
watumishi wa umma au Serikali.
Msamaha huu unatolewa kwa
mujibu wa GN. Na. 520 na 522 za
mwaka 1995
Mtumishi wa umma ambaye kwa
mujibu wa sheria anafaidika na
msamaha wa ushuru katika
vyombo vya usafiri ni mwenye
ngazi ya mshahara ya TGS D au
zaidi kwa upande wa serikali au
inayolingana na hiyo kwa upande
wa Taasisi zingine za serikali na
mashirika ya umma. Mtumishi wa
umma ambaye anaendelea na
masomo yake hapa nchini au nje
ya nchi haruhusiwi kupewa
msamaha wa ushuru hadi pale
atakapomaliza masomo yake na
akaendelea na utumishi wa umma.
Aina ya vyombo vya usafiri
vinavyohusika na msamaha
(a) Magari
Magari madogo aina ya saloon,
Magari aina ya pick – up yenye
uwezo wa kubeba mzigo usiozidi
uzito wa tani mbili, Magari
mengine ambayo hayabebi zaidi ya
abiria tisa.
(b) Pikipiki za aina zote.
Ushuru wa bidhaa
(Excise duty)
Aina ya kodi/ada zinazotakiwa
kulipwa (Hakuna Msamaha)
Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT)
Ada za usajili
Pia ushuru wa bidhaa
maalumu kwa magari
yenye umri wa miaka
kumi au zaidi toka
kutengenezwa
Gharama za bandari
Taratibu muhimu za
kufuataKujaza fomu ya maombi
(Nakala nne) ambayo ni lazima
iambatane na:-
Uthibitisho wa mwajiri
Nakala ya kitambulisho
cha kazi
Kumbukumbu za
ununuzi au uingizaji wa
chombo husika cha
usafiri hapa
Picha nne (4) za
“passport size “ kwenye
fomu ya maombi.
Baada ya kupata fomu za maombi
TRA inatakiwa kuzifanyia uhakiki
na iwapo ni sahihi hupelekwa
Hazina kwa kwa ajili ya kuandika
hundi kwa kiasi cha ushuru
uliosamehewa na kuwasilisha TRA
Baada ya TRA kupata hundi toka
Hazina taratibu zingine
zitaendelea za kuruhusu chombo
cha usafiri kutolewa kwa mwenye
nacho baada ya kulipa kodi zingine
na ada kama vile Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) na
ada ya usajili wa gari.
TAHADHARI! Kwa wale ambao
wanaagiza vyombo vya usafiri toka
nje wanashauriwa
kufanya utaratibu wa kupata
msamaha wa ushuru kabla ya
chombo husika hakijafika hapa
nchini.
Ni kosa kisheria kuuza chombo
cha usafiri kwa mtu mwingine
ambaye hastahili
msamaha bila kwanza kulipa
Ushuru/kodi iliyokuwa
imesamehewa. Pia ni kosa
kutumia kwa shughuli za
biashara.
Epukana na matapeli wakati wote
wa kushughulikia msamaha
unashauriwa kutumia mawakala
wa forodha wanaotambuliwa na
TRA
Kwa maelezo zaidi wasiliana
na :
Mkurugenzi,
Idara ya Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi
SIMU 2119343
Barua pepe info@tra.go.tz
 
aisee umeshindwa hata kupanga hiyo post yako kutoka huko ulikokopi? ungesamarize basi angalau hata mistari miwili kwa wale wenye haraka wapate angalau picha ya kilichopo.
 
Msamaa huu uwepo kwa vijana wote wa kitanzania wanaoshiriki kwenye shughuli rasmi la kuliongezea taifa uchumi. Siku hizi ajira nyingi zimo kwenye sekta nje ya serikali na sioni kwa nini msama huu uwe kwa wafanyakazi wa serikali tu. Otherwise futa misamaha yote ili watanzania wafaidi raslimali za tz kwa usawa
 
Msamaa huu uwepo kwa vijana wote wa kitanzania wanaoshiriki kwenye shughuli rasmi la kuliongezea taifa uchumi. Siku hizi ajira nyingi zimo kwenye sekta nje ya serikali na sioni kwa nini msama huu uwe kwa wafanyakazi wa serikali tu. Otherwise futa misamaha yote ili watanzania wafaidi raslimali za tz kwa usawa
Sasa hivi tunataka misamaha ya kodi ifutwe. Kila mtu alipe kodi.
 
Basically serikali inahimiza ukwepaji kulipa kodi.

Why should they be exempt frm paying the tax?
 
aisee umeshindwa hata kupanga hiyo post yako kutoka huko ulikokopi? ungesamarize basi angalau hata mistari miwili kwa wale wenye haraka wapate angalau picha ya kilichopo.

Mkuu kama una haraka haikuhusu kabisa!
 
sio wote tunaolipwa posho za kuposti kama nyinyi. wengine tunakazi zetu zinazotuweka mjini/kijijini

Hizi ni zaid ya ndoto! Eti mna kazi zenu???!!!! Du, kweli ujinga ni janga! Ungekua na kazi usingejibu kama ulivojitanabaisha. Mkuu una akili ndogo mno, na possibly huna mawasiliano kati ya ubongo wako na unachoandika. Endeleeni na kazi zenu mkuu zinazowanyima hata nafasi ya kutafakari maisha yenu ya kawaida!! Unasukuma mkokoteni nini mkuu?
 
Back
Top Bottom