Maamuzi ya Mawazi

Maamuzi ya Mawazi

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
20,024
Reaction score
45,757
"Tukiangazia suala la msamaha ya kodi tunaona kuwa baadhi ya makampuni yamesamehewa kodi ya 'Import Duty' 35% na VAT 18% kwa sukari inayoagizwa kutoka nje ya nchi tani 410,000 wakati viwanda vya ndani havijapata msamaha huo wa kodi hali itakayopelekea kuzorota na kufungwa kwa viwanda vya ndani kutokana na kutokuwepo ushindani wa haki na usawa, pia msamaha wa VAT unaharibu utaratibu wa ulipaji wa kodi na kuvifanya viwanda vya ndani kulipa kodi zaidi, kusamehe 53% ya kodi katika tani 410,000 za sukari zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, serikali itapoteza mapato wastani wa Dola za Marekani Milioni 217.3 sawa na shilingi bilioni 580, hivyo kwa msamaha huu serikali itapoteza mapato ya shilingi bilioni 580" -Mpina

"Kwa vibali vya tani 410,000 vilivyotolewa wafanyabishara watapata faida kubwa (Super Abnormal Profit) ya jumla ya bilioni 465, mfano sukari iliyonunuliwa na kuingizwa nchini kwa bei ya USD 575 kwa tani na kuuza nchini kwa wastani wa USD 1000 kwa tani na kwa kuwa hakuna kodi yoyote wafanyabishara walipata faida ya USD 425 kwa kila tani 1 ya sukari, changamoto katika maamuzi haya ni pamoja na kwamba; Waziri wa Fedha (kwa sasa ni Dkt. Mwigulu Nchemba) na Waziri wa Kilimo (kwa sasa ni Hussein Bashe) hawana mamlaka kisheria kusamehe kodi iliyowekwa na sheria zilizotungwa na Bunge, haya ni matumizi mabaya ya madaraka na ni uhujumu uchumi wa nchi, hapakuwa na sababu za msingi za kusamehe kodi, kwani bei ya sukari nje ya nchi haikuwa kubwa kiasi cha kuhitaji msamaha, hivyo msamaha huu uliombwa kuwanufaisha wafanyabiashara na sio wananchi" -Mpina

"Sukari ya nje imefutiwa kodi ya VAT lakini viwanda vya ndani vya sukari vinatozwa VAT na kwa kuwa sukari inayoagizwa ni zaidi ya mahitaji, viwanda vya ndani havitaweza kushindana na hivyo kupelekea kuzorota na kufungwa na nchi kupata hasara kubwa, hapakuwa na usimamizi wa bei nchini kwani hata pale sukari ilipopatikana kwa bei ndogo nje ya nchi bado iliuzwa kwa kubwa hapa nchini ambapo mfuko wa kilo 50 uliuzwa Tsh. 145,000, kwenye eneo hilo nimemuomba Mheshimiwa Spika Dkt. Tulia Ackson arejee risiti yenye Na. ya TRA ya EFD Na. 32 ya tarehe 22 Februari 2024 na risiti yenye verification code Na.28630946606 ya tarehe 23 Februari 2024 zilizotolewa na kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited katika ofisi za Dar es Salaam, vielelezo ambavyo nimewasilisha kwake (Spika wa Bunge) kama sehemu ya ushahidi kuhusu namna Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alivyolidanganya Bunge" -Mpina

"Mawaziri hawa wawili (yaani Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe) walitengeneza uhaba wa sukari, kutoa vibali vya kuagiza sukari zaidi ya mahitaji, kuruhusu sukari inayoingizwa kwa msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei kubwa kinyume cha sheria, pia msamaha huo wa kodi unapelekea serikali kupoteza mapato ya shilingi bilioni 580 na kuwawezesha wafanyabiashara kupata faida ya ziada zaidi ya shilingi bilioni 465, kwa maoni yangu hizi ni njama zilizosukwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali kuiba mapato ya nchi" -Mpina

Ni sehemu ya hoja aliyozungumza Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina alipokutana na wanahabari jijini Dodoma Juni 14.2024 ambapo ametumia jukwaa hilo kufafanua hoja alizodai kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amelidanganya Bunge wakati akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha Bungeni hivi karibuni
 
Moderator naomba kichwa cha uzi kisomeke MAAMUZI YA MAWAZIRI YAIKOSESHA SERIKALI MAPATO YA KODI YA 580 BILION
 
Back
Top Bottom