Msamaha kama wa JK kwa wezi wa EPA waleta kizaazaa Pakistani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msamaha kama wa JK kwa wezi wa EPA waleta kizaazaa Pakistani.

Discussion in 'International Forum' started by Patriote, Jan 14, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Serikali ya Pakistani imejikuta ikiingia katika mgogoro mkubwa baada ya kutofautiana na Mahakama Kuu pamoja na jeshi la nchi hiyo baada ya Serikali kuwapa msamaha wanasiasa mafisadi. Mahakama Kuu ya nchi hiyo ilitupilia mbali msamaha huo uliotolewa na Serikali kwa wanasiasa mafisadi na kuitaka Serikali ya nchi hiyo kufikisha wahalifu hao kwenye Court of Law kama sheria inavyotaka. Msimamo huo wa mahakama umesuppotiwa na jeshi la nchi hiyo na hivyo kuifanya Serikali ya Pakistani kuwa katika hali ngumu na hivyo kujikuta ikitegemea huruma ya Bunge kwani siku ya Jumatatu Kura ya Kutokuwa na imani na uongozi wa nchi hiyo inatarajiwa kupigwa.

  Wapembuzi wa mambo wamabaini kuwa Serikali ya nchi hiyo ilisamehe mafisadi hao kwa kuwa na Rais wa nchi pia ni mshiriki wa Ufisadi huo hivyo kutoa msamaha huo ni janja ya kutaka naye asibananishwe. Kama ilivyo ada Rais wa nchi hiyo anajificha kwenye kichaka cha demokrasia ili jeshi lisimuondoe madarakani, Swali ni je Democrasia inaruhusu Rais kuwaibia wananchi wake?????????????????

  Hapa nchini kwetu mambo ni tofauti sana kwani tumeshuhudia mara kadhaa Jeshi letu likipakwa matope na Serikali kuwa ni sehemu ya wizi wa Meremeta. Mara kadhaa jeshi halijaweza kusema lolote kama vile halina msemaji wa jeshi na badala yake Waziri mkuu ndio kageuka msemaji wa Jeshi. Pinda alisema hata tukimuua hawezi kutoa Siri za Jeshi wkt ushahidi upo kuwa hakuna cha siri za jeshi wala nini ni wiiiiiiiz mtupu. Siri za jeshi zipi mbona bajeti yao inajadiliwa ndani ja Bunge kwa uwaz kabisa????

  Kwanini Bunge letu nalo halikuitisha au lisiitishe kura ya kutokuwa na imani na serikali ilihali hakuna kitu cha maana kinachofanywa na serikali zaidi ya kutumia nguvu kubwa na muda mwingi kukingia kifua mafisadi???kwanini wabunge mnaonyesha uzalendo kwa chama badala ya nchi na wananchi waliowachagua???Je wabunge mnaona hali inavyokwenda ndivyo mlivyotaka iende??Kila siku ni visa juu ya vituko, ni wizi juu ya ufisadi. ukigeuka huku Jairo kakusanya michango isiyo halali, ukigeuka huku Twiga wametoroshwa Bila vibali, mara Rada ilihusisha ufisadi, mara UDA iliuzwa kifisadi mara misamaha ya kifisadi mara tenda za kifisadi. Mbona wahusika hatuwaoni wakipelekwa mahakamani???au hayo yanayofanyika si makosa ya kisheria????Ni nani sasa anatakiwa apelekwe mahakamani???Wabunge haya mnayaona ila Hoja kuu ni Posho. Badilikeni ni aibu kwenu.

  Kuhusu suala la Rais kutoa msamaha kwa wezi wa EPA, hii ni kinyume cha sheria kwani Rais hayupo juu ya sheria. Ila hatujasikia mahakama kukemea hilo wala vyombo vya usalama wala mwanasheria mkuu kukemea hilo. Sababu za kutokufanya hivyo vyombo hivi ndivyo vinajua.

  Nashauri vyombo vetu (MAHAKAMA, BUNGE, POLISI NA JESHI) vibadilike na kutambua kuwa wao wameajiriwa kumlinda na kutetea wananchi wema na sio chama cha siasa/Rais aliyepo madarakani pamoja na wahalifu/uhalifu. Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vetu vya usalama na kisheria vimeshiriki kwa kiwango kubwa kumkandamizi mwananchi kwa manufaa ya uongozi uliopo madarakani. Nawashauri muige misimamo ya wenzenu wa Pakaistani ambao wanaona kuwa vyama vitapita na kufa, Marais watapita na kufa ila nchi yao itaendelea kuwepo hivyo wameamua kuwa Wazalendo wa kweli na hata kupingana na Serikali dharimu na ya kifisadi katika upumbavu inaoufanya wa kutetea Mafisadi na kukandamiza Raia wema.

  Source: BBC News
   
Loading...