GE2025 Msako magari yenye 'plate number SSH 2530' wanasa 15 Dar

GE2025 Msako magari yenye 'plate number SSH 2530' wanasa 15 Dar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za kukutwa wakitumia namba za SSH 2530 kwenye magari. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni sehemu ya utekelezaji onyo la kutotumia namba hizo baada ya Septemba Mosi, 2025.

Awali, Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Msemaji wake David Misime, lilipiga marufuku matumizi ya namba hizo kwenye magari na kutoa hadi Septemba 1, 2025 wahusika wawe wamezitoa.

Alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakibandika namba hizo kwenye magari yao kinyume na sheria, jambo ambalo lilizua sintofahamu kwa watumiaji wengine.

“Mtu yeyote anayebandika namba hizo baada ya kufuatiliwa kwenye mifumo ya usajili, itahesabika hilo ni kosa la kisheria na atakayekamatwa atakuwa na kosa la kuendesha chombo cha moto bila usajili wa namba rasmi,” alisema Misime.

Leo Alhamisi Septemba 4, 2025 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu 10 huku msako ukiendelea.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 Marejeo ya Mwaka 1973 yaliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, mtu yeyote anayeendesha chombo cha moto bila kuwa na usajili rasmi na namba halali za usajili anatenda kosa la jinai.

Soma zaidi
 
Mpaka watu walalamike ndiyo wanachukua hatua! Mambo ya ajabu kabisa haya kwa jeshi la polisi kufanya kazi zake kwa kusikilizia matamko ya wanasiasa, badala ya kutumia weledi.
 
Maigizo hz namba hazina matundu Sasa zilifungwaje?jiulize
 
Wajinga namba alizitoa m.kiti wa CCM Samia, wakamkamate, na Samia ataenda Jela 2031 wakati Lissu akiwa rais
 
Back
Top Bottom