Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,858
Nashindwa kabisa kumuelewa Msajli wa Vyama vya Siasa nchi,Jaji Mtungi kwa kukaa kimya huku vyama vya siasa vikinyimwa haki ya kikatiba ya kufanya mikutano na sasa hata makongamano jambo ambalo sidhani kama linaendana na sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini.
Vile vile kama sikosei,Msajili wa Vyama vya Siasa ndie mlezi wa vyama vya siasa hapa nchini(kama siko sahihi nirekebishwe) lakini yuko kimya tu kama hakuna linaloendela.
Waandishi hebu mumshitue japo kwa kutaka maoni yake juu ya hatua ya serikali kupiga marufuki mikutano ya vyama vya siasa na hata Kongamano lililokuwa limepangwa kufanywa na chama cha ACT-Wazlendo kwa lengo la kujadili Bajeti ya Serikali.
Kwa maoni yangu,nilitarajia Ofisi ya Msajili ingekuwa imetoa tamko kuhusu chama cha ACT kuzuiwa kufanya kongamano lake siku ya Jumamosi kwani swala la ACT bado hata halijatinga rasimi mahakamani.
Mh.Msajili,kauli yako inaweza kuwa msaada mkubwa na kuepusha mengi kwa ustawi wa nchi hii na zaidi katika kusaidia kukua na kuimarika kwa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.
Hata hivyo,ili taasisi hii iwe huru, sheria ilioanzisha chombo hiki inapaswa ibadilishwe ikiwemo kipengele kinachoelekeza kuwa Msajili atateuliwa na Raisi.