singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
MSAJILI wa Vyama Siasa, Jaji Francis Mutungi amevipa vyama vya siasa miezi mitatu kukamilisha hesabu zao.
Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge jana, Jaji Mutungi alisema ukaguzi wa fedha katika vyama ni suala la sheria na lina mchakato.
Jaji Mutungi aliyasema hayo siku chache baada Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kutoa ripoti yake ya mwaka 2014/15.
Alisema ofisi yake imeisoma taarifa ya CAG na inaifanyia kazi kwa kuvipa vyama hivyo miezi mitatu kukamilisha hesabu zao.
“Kwa mujibu wa sheria tunatakiwa kuvikumbusha vyama kufanya ukaguzi na tulifanya hivyo mwanzoni mwa mwezi huu (Aprili).
Tuliviandikia barua vyama vyote. Lakini kutokana na kuibuliwa kwa suala hili tumeviandikia barua na kuvipa miezi mitatu kukamilisha hesabu zao,”alisema.
Alisema ofisi yake haiwezi kuvilazimisha vyama kuhusu suala hilo kwa vile jambo hilo linafanyika kwa matakwa ya sheria.
“Baada ya CAG kukagua hatua inayofuata ni kuchukua taarifa na kuangalia hatua gani zifuatwe kwa kuzingatia maelezo yake.
Mfano, kama kuna sintofahamu kwa hesabu za vyama vinavyopata ruzuku hatua mojawapo ni kukata kile kiwango kinachodaiwa katika hesabu za CAG kutoka katika ruzuku,” alisema.